POOL PARTY

POOL PARTY

Monday, February 24, 2014

WOLPER GAMBE AJIANIKA LIVE AKIFANYIWA MASAJI

 
MAKUBWA! staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejianika akifanyiwa masaji laivu. Wolper a.k.a Gambe ‘alifanya yake’ ndani ya saluni (massage parlor) moja iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar. Mara baada ya tukio hilo huku akiwa ‘amefotolewa mapicha’ ambayo aliyatundika kwenye ukurasa wake wa Instagram, mwanadada huyo alielezea jinsi alivyohisi raha ya ajabu wakati akifanyiwa masaji. “Asante…(akitaja jina la saluni), kwa raha niliyopata leo…, mi siyo mchoyo kwa kweli karibuni nanyi mpate afya. Nimefurahia walah,” aliandika Wolper. Hata hivyo, tukio hilo liligeuka gumzo huku baadhi ya mashabiki wakimsifia na wengine wakimponda.

No comments:

Post a Comment