POOL PARTY

POOL PARTY

Monday, February 24, 2014

TIMBULO NA PENZI LA SKAINA

Stori: Mayasa Mariwata
CHIPUKIZI wa Bongo Fleva, Ally Timbulo amefunguka kuwa alimwagana na mwigizaji Skyner Ally ‘Skaina’ kwani aligundua kuwa ana uhusiano na Mbongo Fleva mwenzake, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Skyner Ally ‘Skaina’.
‘Akikonfesi’ mbele ya kinasa sauti cha Ijumaa Wikienda, Timbulo alisema ishu hiyo ilitokea miaka kadhaa iliyopita ambapo ‘alimsarendia’ mlimbwende huyo ili awe mpenzi wake na aliposhtuka kuwa ana uhusiano na Nay wa Mitego, fasta alibadili uelekeo.
Ally Timbulo.
“Daah! Nilipogundua ana uhusiano na Nay, fasta nilimpotezea,” alisema Timbulo, alipotafutwa Skaina, alisema: “Usiniulize hizo habari, ulivyosikia ndiyo hivyohivyo.”

No comments:

Post a Comment