Msanii kutoka Kigoma na memba wa kampuni
ya Leka Dutigite Linex Sunday Mjeda ameendelea kutoa kilio chake juu ya
uzushi ulioenezwa siku kadhaa zilizopita baada ya kupost picha
mbalimbali akiwa na video vixen maarufu wa hapa bongo Agnes Gerald aka
Masogange.
Baada ya picha hizo kusambaa Linex alikana habari
zilizoandikwa na baadhi ya blogs kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na
mrembo huyo.
“ni kweli watu wa blog mnapush sana kazi zetu but
nimesikitishwa na habari hii iliyoandikwa na blog kadhaa mtasababisha
tutashindwa ata kukaa na Dada zetu au marafiki zetu Uliza b4 Hujaandika
ujinga am single na sina haraka ya kua na mpenzi.” Aliandika Linex
kwenye akaunti yake ya facebook.
Kupitia Facebook jana mwimbaji huyo wa ‘Kimugina’ ameendelea kulalamika juu ya matokeo ya habari hizo za uzushi:
“Daaah
Uzushi ulioenezwa na baadhi ya blog miyeyusho umesababisha
Umenitofautisha na familia yangu ndugu jamaa na marafiki wish kama Mungu
awafunue ndugu jamaa marafiki washabiki wangu waujue ukweli bado
naendelea kupokea cm nyingi za maswali japo nilishaongea b4 kwamba sina
mahusiano na Masogange daaaaah.”
No comments:
Post a Comment