Akizungumza
leo asubuhi kupitia kipindi cha Power Breakfast cha clouds
fm,Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba
alisema kuwa kipindi hicho kitaonyesha mchakato mzima wa mwanzo wa
kutafuta washindi wa idea bora ambapo barua zilikuwa 2000 zikachujwa
hadi zikapatikana barua 100 mwisho wakapatika washindi 30 ambapo
washindi hao ndiyo watakaoanza kuonekana kwenye kipindi hicho.Ambapo
aliongeza kuwa kipindi hicho kitakuwa na majaji na kitaenda kwa muda wa
miezi miwili kuanzia leo,ambapo watazamaji watapata fursa ya kuingia
ubia na mshiriki ambaye atakuwa amevutiwa na idea yake na kuchukua wazo
lake.
No comments:
Post a Comment