POOL PARTY

POOL PARTY

Friday, February 21, 2014

LA LIGA: BARCELONA, REAL MADRID NA ATLETICO DE MADRID KWENYE VITA KULILIA NAFASI YA KILELENI WIKIENDI HII!! NANI KUIBUKA KINARA?

Wote wakiwa na Pointi 60 kila mmoja, na kutenganishwa kwa ubora wa Magoli kitu ambacho mwishoni mwa Msimu hakihesabiki.
Kwa Kanuni za La Liga, mwishoni mwa Msimu, ikiwa Timu zitafungana kwa Pointi kinacho watenganisha ni Matokeo yao Mechi zao za Uso kwa Uso.

Wikiendi hii, Jumamosi Real Madrid watakuwa Nyumbani Santiago Bernabeu kuikaribisha Elche ambayo iko Nafasi ya 13.
Real watatinga Mechi hii bila ya Cristiano Ronaldo ambae ndie anamalizia Kifungo chake cha Mechi 3.

Siku hiyo hiyo Jumamosi, FC Barcelona wako Ugenini kucheza na Real Sociedad Mjini San Sebastian Uwanjani Anoeta ambako Barca hawajashinda katika Mechi 5 Uwanjani hapo.
Mara ya mwisho Timu hizi kucheza ni mapema Mwezi huu kwenye Nusu Fainali ya Copa del Rey ambako walitoka 1-1 Uwanjani Anoeta na Barcelona kusonga Fainali kwa vile walishinda 2-0 Nou Camp katika Mechi ya kwanza.
Nao Atletico Madrid watacheza Jumapili Ugenini na Osasuna ambayo iko Nafasi ya 14.

RATIBA:
Leo Ijumaa Februari 21

23:00 Real Valladolid v Levante
Jumamosi Februari 22
18:00 Real Madrid CF v Elche CF
20:00 Celta de Vigo v Getafe CF
22:00 Real Sociedad v FC Barcelona
23:59 UD Almeria v Malaga CF
Jumapili Februari 23
14:00 Rayo Vallecano v Sevilla FC
19:00 Real Betis v Athletic de Bilbao
21:00 Valencia v Granada CF
23:00 Osasuna v Atletico de Madrid
23:59 RCD Espanyol v Villarreal CF


kwa hisani ya www.bukobasports.com

No comments:

Post a Comment