Diamond Platinumz atakuwa ni msanii pekee wa Tanzania atakayeungana na wasanii walio kwenye orodha A, katika kuhudhuria utoaji wa tuzo za Africa Music Magazine(Afrimma)
zitakazofanyika Jumamosi July 26,Eisemann Center,Texas nchini Marekani.
Tuzo hizo zilizoandaliwa na African
Muzik Magazine na Big A Entertainment zimelenga hasa katika
kuwatunuku wasanii mbalimbali wakubwa wa Afrika waliopo duniani kote na itagusa
nyanja mbalimbali za burudani.
Bright Okpocha aka Basket Mouth ambaye
mchekeshaji maarufu wa Nigeria na mrembo
wa Nollywood Juliet Ibrahim (Ghana) watakuwa washereheshaji wa tuzo hizo.
No comments:
Post a Comment