Ile
filamu ya Kigodoro ambayo ilihairishwa uzinduzi wake siku ya Valentine
mwezi huu,sasa kufanyika Jumamosi hii pande za Dar Live,Mbagala.Muandaaji
wa uzinduzi huo,Zamaradi Mketema amesema kwa kushirikiana na Global
Publishers walihairisha uzinduzi huo ili kuufanya uwe na burudani za
kutosha na kuwapa mashabiki kitu cha uhakika.Alisema
kuwa katika uzinduzi huo wa Usiku wa Kigodoro watakuwepo wasanii
mbalimbali kama Msagasumu a.k.a Mkali wa Kigodoro, Rihama Ally,Shamsha
Ford,Wema Sepetu,Kajala Masanja na wengineo.
Naye Staa wa filamu za
Kibongo,Wema Sepetu amesema kuwa hajawahi kuhudhuria Kigodoro na ana
hamu sana ya kukiona na na kuwaambia mashabiki wajitokeze kwa wingi
Jumamosi hii
No comments:
Post a Comment