Leo msanii Bob Junior kupitia mtandao mmoja wa kijamii aliamua kuwachana wasanii waliojiunga na CCM, alisema kua hakukua na ulazima wa wao kujiingiza katika siasa na pia alisisitiza kua hakukua na ulazima wa wao kujitangaza kua wameiunga na chama hicho. Moja ya kauli aliyoisema ni " muelewe kwamba iyo ni janja ya nyani kwani sio kuingia kila sehem mpaka watu wajue bongomoves so mjipange kwan mtaanguka kisanaa "
Itakumbukwa kua mwaka 2010 mwanadada Nakaya na msanii Marlow walijiingiza katika siasa jambo ambalo lililowafanya kushuka kimziki hadi leo hawasikiki. Msanii Marlow kupitia gazeti moja alisema kua anajutia kitendo chake cha kujiingiza katika siasa kwani kilimshusha sana kisanaa.
No comments:
Post a Comment