POOL PARTY
Monday, February 3, 2014
UWEZI AMANI YAANI BAADA YA KUDHALILISHANA INSTAGRAM STALISHA NA PREZOO WARUDIANA
Baada ya matusi ya kila aina aliyoyapata kutoka kwa mpenzi wake, Starlisha Tillya aka ‘Mdoli wa Kichaga’ (Chagga Barbie), Prezzo aliandika: President” is like a drug (highly addictive) he’s the best up until the drugs runs out, withdrawal symptoms can be seen from miles.”
Kauli hiyo ilikuwa na ukweli kwa asilimia 100, kwakuwa ni kweli Starlisha ameshindwa kumsahau rapper huyo anayejiita Mfalme Mswati na hivyo kuamua kurejea tena kwenye himaya yake.
Mtanzania huyo anayeishi nchini Marekani, jana alipost picha ya Prezzo kwenye Instagram na kudai kuwa ameamua kumsamehe Prezzo na kwamba hakuna mahusiano rahisi duniani.
“Let De Movie Continue #MapenziniUpofu #HakunaNgechuBilaChaggabarbie #MunguAnajuaKwanini #SihitajiyeyoteZaidiYake #NawaombaMtuombee #HakunaMahusianoRahisiDuniani NimeaminiUkimpendamtuhataitokeeniniHuwezikuukimbiaMoyo. Nawatakia Jumapili Yenye Amani, Furaha, Upendo, Kusamehe na Mumtangulize Mungu Jamani Ndio Kila Kitu. Kwa Neema Yake Kanipaujasiri wakuwaeleza haya Leo,” aliandika kwenye picha hiyo.
Bado Prezzo hajasema lolote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment