Ni
ukweli usiopingika kuwa ajali zimekuwa ni mwiba mchungu kwa familia, jamii na
taifa kwa ujumla unaoacha kilio, walemavu, yatima, wajane na wagane kila
kukicha.
Katika
kuunga mkono jitihada za kupunguza ajali barabarani wakali katika muziki wa
bongo fleva Mr Blue, Amini, Barnaba Boy na Dyna Nyange wameshiriki kurekodi
wimbo wao utakaotumika kwenye kampeni ya dereva makini inayolenga kuhamasisha
uzingatiaji wa usalama barabarani na kwenye vyombo vya usafiri. Wimbo huo
umerekodiwa na mtayarishaji wa muziki C9.
Kampeni
hiyo ya dereva makini imeandaliwa na Transevents Marketing kwa lengo la kutoa
hamasa kwa madereva kuwa makini wanapoendesha magari ili kuwawezesha abiria
kufika salama waendako.
Audio
ya wimbo wa dereva makini imesharekodiwa na kinachosubiriwa ni video yake,
tazama video ya maelezo ukitumia link hii hapa chini.
No comments:
Post a Comment