Pia aliongeza kuwa katika jamii kulikuwepo na ukimya mkubwa juu ya haya madawa ya kulevya,majadiliano juu ya ulevi wa madawa hayo yalikuwa hayazungumziki kwa uwazi hata kidogo japo madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ni makubwa sana na yanatisha katika jamii yetu hapa Tanzania.
Ameongeza kuwa nia na madhumuni ya kuanzisha Ray C Foundation hasa ni kuhamasisha na kuelimisha vijana na jamii nzima athari za utumiaji madawa ya kulevya na kuwafikia walengwa ndani ya jamii na katika maeneo ya nchi nzima!!!!!!Eeh Mungu Tuepushe na Janga hili Nguvu kazi ya Taifa isipotee.........We need your Support...Alimalizia Ray C.
No comments:
Post a Comment