Hamis Corleone Mwinjuma
Katiba sio jambo dogo..na hii inayotakiwa kutengenezwa sasa pengine
itakaa kwa vizazi kadhaa..watu walioaminiwa kwenda kulisaidia Taifa
kuandika historia na kuamua mustakabali wake wanapoacha ya msingi
wanayotakiwa kuyafanya na kuanza kujadili ulafi wao ni upuuzi..naamini
wote mle 'wanajidai' wanafanya kazi ile kulisaidia Taifa lao,hapo
hapo,kama ndivyo walitakiwa kuifanya BILA MALIPO..kwa sababu ya hali za
kimaisha tunavyozijua ni sawa kuwezeshwa ili waweze kujikimu,sasa haya
ya 'hadhi yetu' yanatoka wapi tena?kama kweli una 'hadhi hiyo' utakuwa
na kipato cha 'kuchangia' kumudu aina ya maisha unayodai ni yako ili
utusaidie sisi wa 'hadhi ya chini' tupate katiba,NO??acheni tamaa,hili
TUTALIKOMALIA hamtakaa muamini..
No comments:
Post a Comment