Lakini leo (February 25) Ali Kiba amezua maswali mengine kwa mashabiki wake baada ya kuweka kwenye Instagram picha inayomuonesha akiwa na AY na Mwana Fa na kuandika ‘@Aytanzania&007#mj record #wait for it bonge ya wimbo.’
Hata hivyo hakuweka wazi kama ni wimbo wake au ameshirikishwa na maswaiba hao.
Tovuti ya Times Fm imefanya mahojiano na Ali Kiba ambaye ameyajibu maswali hayo yote, maswali ambayo hapo awali yalikuwa na majibu ya kuhisia tu bila kuwa na uhakika.
Ali Kiba ameiambia tovuti hii kuwa aliweka picha hiyo kwenye Instagram lakini hakuweka maelezo ya kutosha kwa makusudi.
“Sababu ya kuweka vile ni katika kutaka tu kuwa-surprise watu kwa sababu sikupenda kuwambia ni ngoma ya nani ila nimewajulisha kuwa nimefanya nao na tumefanya kwa MJ, hiyo yote ni kutaka kuwa-surprise.” Amesema Ali Kiba.
Mwimbaji huyo amedai kuwa hadi sasa wimbo huo haujajulikana ni wa nani kati yake yeye, Mwana Fa na AY, “tumefanya wote…haijajulikana ngoma ni ya nani.”
Ali Kiba ameongeza kuwa mashabiki wampe miezi miwili ijayo na kisha watapata maelezo ya kutosha kutoka kwake na kwamba baada ya muda huo kila kitu kitakuwa sawa.
Mwimbaji huyo wa ‘My Everything’ ameeleza pia sababu za yeye kuwa kimya, pamoja na mpango wake kwa mwaka 2014 ambapo amedai kuwa ataachia albam yake mpya.
“Sababu ya kuwa kimya ni kumpush Abdu Kiba aweze kuwa sawa sawa na vilevile mimi ni mzazi kwa hiyo niko busy na jinsi ya kuwa baba. Yaani vitu vingi vyote nilikuwa nikifanya, wakati muda wote niliokuwa nikifanya hivyo vitu nilikuwa najiandaa na albam yangu nyingine ambayo ni ujio mpya…nakuja na everything.
“Albam ipo kwa sababu itakuwa chini ya usimamizi wa kampuni ambayo inanihost, na ndio maana nikakwambia nipe miezi miwili na watu watajua kila kitu kinachoendelea…itafanyika na usimamizi mzuri tu na process zote zitakuwa ziko okay. Ila siwezi kukwambia ntafanya na distributor gani lakini, wasimamizi wangu watafanya hilo, wasimamizi ambao wamenichukua ndio maana ukaona kimya kingi, ni ku-fight maandalizi na kumaliza ngoma.”
No comments:
Post a Comment