BENDI ya muziki wa dansi ya Msondo, wasanii nyota wa Bongo Fleva, H. Baba, Nay wa Mitego na Stamina wanatarajia kulipamba Bonanza la Jogging la Global Breaking News 15778 litakalofanyika katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar, Februari 9 mwaka huu.
Mratibu wa Bonanza hilo, Rajabu Mteta (KP) ameiambia Mikito Nusunusu kuwa kabla ya wasanii hao kupanda jukwaani kuanzia asubuhi hadi jioni, kutakuwa na jogging (mbio za taratibu) zitakazosimamiwa na wenyeji, Kejo Jogging Sports Club, kuanzia uwanja wa taifa majira ya saa 12 na nusu hadi ukumbini Dar Live.…
Mratibu wa Bonanza hilo, Rajabu Mteta (KP) ameiambia Mikito Nusunusu kuwa kabla ya wasanii hao kupanda jukwaani kuanzia asubuhi hadi jioni, kutakuwa na jogging (mbio za taratibu) zitakazosimamiwa na wenyeji, Kejo Jogging Sports Club, kuanzia uwanja wa taifa majira ya saa 12 na nusu hadi ukumbini Dar Live.
Alisema zaidi ya klabu 200 kutoka wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam zimethibitisha kushiriki matembezi hayo huku klabu kadhaa za soka, netiboli, darts na pool table zikishindana katika bonanza hilo kwa kiingilio cha shilingi 2000 kwa wasio wanamichezo.
Mteta alizitaja klabu za soka zitakazopepetana kwenye tamasha hilo kuwa ni veteran kutoka Taifa, Hamasa, Buguruni, Mwembechai, Azam, Oilcom, Machava, Ufukoni, Dovia, Scud, Mafaza, Sakaramento, Kejo, Police Baracks, Magereza, Temeke, Uamsho, Mjengo na Global.
Pia alizitaja timu zitakazochuana katika mchezo wa netiboli kuwa ni Hamasa, Barracks, Buguruni, Kejo, Mwembechai, New Habari 2006 Ltd, The Golden, Ndiyo sisi Netiboli, Classic, Global na Magenge 20.
Pia kutakuwa na michezo mingine kama kuvuta kamba, bao la kete, drafti, karate, kukimbia na gunia, ngumi na michezo maalum ya watoto ambayo itaambatana na zawadi.
Meneja wa Kampuni ya Global Publishers ambao ndiyo wanaotoa huduma ya Global Breaking News, Abdallah Mrisho, amesema kupitia bonanza hilo, wataitambulisha huduma hiyo mpya inayowezesha wasomaji wanaotumia mtandao wa Vodacom kupata habari mbalimbali za papo kwa hapo katika simu za mkononi.
“Tutaizindua rasmi huduma ya Global Breaking News ukumbini. Kwa wanaotaka kujiunga na huduma hii, wataandika neno Global katika uwanja wa meseji kisha kutuma kwenda namba 15778, burudani Bongo Fleva na bendi ya Msondo kama kawa,” alisema Mrisho.
No comments:
Post a Comment