Stori: Erick Evarist na Joseph Shaluwa
SIKU chache baada ya kuzagaa kwa taarifa za kuachana na mkewe mama
Tunda, mfalme wa Rhymes, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ ameibuka na
kusimulia mambo ya kusikitisha waliyopita katika safari ya maisha yao.
Mfalme wa Rhymes, Seleman Msindi ‘Afande Sele’.
Akizungumza na wanahabari wetu ndani ya Ukumbi wa Meeda, Sinza-Mori,
Dar, juzi Afande alisema hadi kufikia hatua ya yeye kutangaza kuwa
ameachana na mama Tunda ambaye amedumu naye kama mume na mke kwa zaidi
ya miaka 10, alikuwa akivumilia mambo mengi na mwisho kuamua kuachia
ngazi.
Afande Sele akiwa na familia yake.
“Nilikuwa nikielezwa mengi kuhusu mke wangu, nilishapigiwa simu na
kuambiwa mke wangu anagombaniwa na wanaume usiku klabu lakini huwa mimi
siyo mtu wa kuishi kwa hisia, nilivumilia nikiamini atajirekebisha,
haikuwa hivyo.
“Japo sikuwa na uthibitisho wa moja kwa moja, lakini nyumbani alikuwa
siyo mtu wa kutulia, amekuwa akinizunguka hadi kwa washkaji zangu wa
karibu. Kuna jamaa alichoshwa na habari hizo akanifuata na kuniambia
hata kama lakini uvumilivu wangu ulizidi,” alisema Afande kwa hisia.
Akiendelea kushusha masikitiko yake mbele ya kinasa sauti cha
Risasi Jumamosi,
Afande alienda mbele zaidi kwa kusema mbali na mkewe huyo kumsaliti kwa
wanaume tofauti wakiwema marafiki zake, ilifika wakati mama Tunda akawa
anachukua fedha ndani na kwenda kutumia na wanaume.
Alisema
alitumia mwanya wa mkali huyo wa mashairi anapokuwa amesafiri katika
shoo mbalimbali na kuachiwa fedha za matumizi pamoja na ujenzi wa nyumba
yao mpya, kutanulia.
“We acha tu, yaani fedha za matumizi, ujenzi nilikuwa namuachia
lakini cha kusikitisha ni kwamba alizitumia kutanulia, jambo ambalo
nililizidi kunitia umaskini na machungu ukizingatia jamii inaniheshimu
kama msanii, mbaya zaidi wananchi wamenitaka nigombee ubunge Morogoro
Mjini,” alisema Afande.
Akizidi kushusha ‘vesi’, Afande alitiririka
kuwa kuna wakati aliwahi kupewa taarifa na rafiki yake mwingine aishie
Kurasini jijini Dar ambaye alilamika juu ya mkewe kufika kwa jamaa huyo
na kuazima fedha bila kuzilipa.
Kwenye aya nyingine, mkali huyo alisema anakumbuka jinsi alivyoishi
na familia yake, mkewe, wanaye Tunda na Ahsante Sanaa lakini hana jinsi
kwani ameona bora kuachana kwani umri wake una mruhusu kuoa mke mwingine
siku ikitokea.
“Nakumbuka maisha kidogo ya furaha na familia, mama Tunda atabaki
kuwa mama wa watoto wangu lakini kamwe hawezi kurudi kwangu kwani
itakuwa ni aibu juu ya aibu,” alisema.
Afande aliachana na mama
Tunda mwishoni mwa mwaka jana alipotimba jijini Dar katika shughuli zake
za kikazi na kumuachia mkewe fedha za ujenzi lakini aliporejea nyumbani
Morogoro, alikuta mzazi mwenzake huyo ameondoka nyumbani na kuacha
funguo, kila alipompigia simu hakupokea.
Alipoulizwa kuhusiana na shutuma zilizoporomoshwa na Afande, mama Tunda alitiririka:
“Alinipa Sh. milioni 3 za shoo tu, tukanunua vifaa vya ujenzi lakini
siyo kwamba nilitanua na wanaume, tena kama ni kumfumania, mimi ndiye
nilimkuta na mwanamke alitoka naye Fiesta Dodoma, sikutaka tu kumsema,
hizo taarifa anazusha tu.
“Kwanza kuna mambo mengi tu amenifanyia, alikuwa mlevi kwani hadi
wazazi wangu walikuwa wakinishangaa sana, sasa na mimi nikaona bora
niachane naye,” alisema mama Tunda.