POOL PARTY

POOL PARTY

Thursday, February 20, 2014

MWAKIFWAMBA AWAINGIZA CHAKA BONGO MUVI


Wakizungumza katika kikao cha dharura kilichoitishwa ghafla Jumatatu iliyopita kwenye viwanja vya Leaders, Kinondoni, jijini Dar, wasanii tofauti wa burudani waliungana na…
 
WASANII wa sinema wanaounda Kundi la Bongo Muvi, wamemshutumu Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba kwamba amewaingiza chaka katika uteuzi wa mjumbe anayewawakilisha katika Bunge la Katiba lililoanza juzi mjini Dodoma.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba.
Wakizungumza katika kikao cha dharura kilichoitishwa ghafla Jumatatu iliyopita kwenye viwanja vya Leaders, Kinondoni, jijini Dar, wasanii tofauti wa burudani waliungana na kuweka mikakati ya kuhakikisha wanapata wawakilishi wengine watakaoweza kuwatetea kikamilifu.
“Sisi hatuelewi kwa nini Mwakifwamba ametuchezea mchezo, alitakiwa kutuita na kutuambia kuwa kuna kitu kama hicho, lakini alipeleka majina yake kumi na mwisho wa siku amechaguliwa Paul Mtenda mtu ambaye tuna uhakika hana uwezo wa kuongea na kutusaidia kwa lolote huko bungeni,” alisema mmoja wa wasanii hao akiungwa mkono na wenzake.
Wasanii hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ walisema watamuweka chini Mwakifwamba mara tu akirejea kutoka Dodoma ili wamkemee.
“Hii imethibitisha kwenye tasnia tuna matatizo, alitakiwa kutushirikisha wote lakini yeye amekaa na watu wake akaamua kuteua na mwisho wa siku ndiyo wakampitisha Mtenda, sisi tumemkubali lakini hatujafurahishwa na tabia ya Rais kwani ameweka wazi tofauti zetu, tutahakikisha wanaingia watu wengine wenye nguvu,” alisema Steve Nyerere.
Lakini akijibu shutuma hizo, Mwakifwamba alisema taasisi zote zilituma maombi baada ya matangazo kutoka na kupelekwa kwa katibu wa bunge. Aliwataja baadhi ya waliotuma kuwa ni yeye mwenyewe, Yvonne Cherly ‘Monalisa’, Suzan Lewis ‘Natasha’, Mike Sangu, Deo Songa, Paul Mtenda na Emmanuel Myamba  ‘Pasta Muyamba’.
“Mimi naweza kuwaona kama hawana hoja huko hawakuwa wakipelekwa watu maarufu, waliangalia CV na mpaka sasa sijajua ni vigezo gani vinavyotumika lakini ninachofahamu kuna wizara inayohusika ambayo iko chini ya Mhe. William Lukuvi na mchujo ulipita kwa watu wa intelijensia kisha majina yote yakapelekwa kwa Rais yeye ndiye alipitisha majina yake, hivyo kama wamepanga kuniweka chini mimi niko tayari na nitawashinda kwa hoja kwa sababu kwanza wao si wanachama wa TAFF,” alisema Mwakifwamba.

No comments:

Post a Comment