POOL PARTY

POOL PARTY

Monday, February 24, 2014

Haya ndio maoni ya MwanaFA kuhusu bunge la katiba

 
Hamis Corleone Mwinjuma
Katiba sio jambo dogo..na hii inayotakiwa kutengenezwa sasa pengine itakaa kwa vizazi kadhaa..watu walioaminiwa kwenda kulisaidia Taifa kuandika historia na kuamua mustakabali wake wanapoacha ya msingi wanayotakiwa kuyafanya na kuanza kujadili ulafi wao ni upuuzi..naamini wote mle 'wanajidai' wanafanya kazi ile kulisaidia Taifa lao,hapo hapo,kama ndivyo walitakiwa kuifanya BILA MALIPO..kwa sababu ya hali za kimaisha tunavyozijua ni sawa kuwezeshwa ili waweze kujikimu,sasa haya ya 'hadhi yetu' yanatoka wapi tena?kama kweli una 'hadhi hiyo' utakuwa na kipato cha 'kuchangia' kumudu aina ya maisha unayodai ni yako ili utusaidie sisi wa 'hadhi ya chini' tupate katiba,NO??acheni tamaa,hili TUTALIKOMALIA hamtakaa muamini..

No comments:

Post a Comment