POOL PARTY

POOL PARTY

Wednesday, August 21, 2013

MLIE TUU ! WASTARA HATAOLEWA BONGO TENA


Na Imelda Mtema
KAKA wa staa wa Filamu za Kibongo, Wastara Juma aitwaye Juma Juma ameliambia Risasi Mchanganyiko kwamba dada yake hatafunga  tena ndoa nyingine hapa nchini.

“Iwapo dada yangu akitaka kuolewa atafanya hivyo Uarabuni siyo hapa kabisa,” alisema kaka huyo na kudai kuwa ameshuhudia mateso mengi ya dada yake kwa wanaume wa Kitanzania.

Kaka huyo amesisitiza kwamba wanaume wasipate tabu ya kumuuliza dada yake kuhusu suala la ndoa kwani watajisumbua bure.
Juma alizungumza kwa niaba ya dada yake ambaye awali alipigiwa simu ili kuulizwa kama alikuwa na mpango wa kufunga ndoa nyingine hapa nchini.

Hata hivyo, Wastara alimwachia kaka yake huyo kujibu badala yake, ingawaje kaka huyo hakufafanua kama dada yake ameshapata mtu wa kufunga naye ndoa huko Uarabuni.

Wastara alifunga ndoa tatu na wanaume tofauti na mume wake wa mwisho alikuwa msanii wa filamu, Juma Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia mapema mwaka huu.

MASHABIKI WAMSHUKIA DIAMOND BAADA YA KUPOST ONLINE PICHA YA DOLE LA KATI


“Is this the right finger that you are talkin about @roma2030 …?” ameandika kwenye picha ya Instagram aliyopiga na rapper Roma Mkatoliki

Hata hivyo picha hiyo imevuta hisia za mashabiki wenye hasira waliomwangushia mvua ya madongo kwenye Instagram ambapo ana followers zaidi ya 36,100 hadi sasa. Hizi ni baadhi ya comments:

Mafuruzenkonoki: Umekua sasa hivi kijana, hizo ishara haziendani na ulivyo! Change!

Lugnno: Umeimba wimbo ma mc mara matus mara bang umekuwa mc naona inshara ya tus kwenye kdole cmon usizd sana hta km upo mbal utakosea km wkt ule ulvua surual takecare man sijaipenda

luvcartel: Astaghafurullah… juzi ulikua muislam leo ushakua kafir? Subhannallah

ladisdallaz: The middle finger? To u nt to us

mmolezson: Diamond n Roma nyie wote wajinga tu, mtu yeyote mwenye akili timamu and rational awez point finger lik dat then anapoist kwenye social networks ili jamaa waone.

Alice_aswile: Aah hapana diamond,hivyo vitu hapa cio mahali pake loh,hivyo mfanyie demu wako gheto.

Makitoti: Ain’t ryt diamond ….just ain’t ryt, we love ur music Ila that pic!!!!naaaah,haifai

Mmolezson: Kwa hyo hcho kidole mnatuoneshea sis ee, hv unawakumbka wasanii hpa Tz ambao walikuwa maaruf kulko nyie? Je saiz wko wp ee na wala hawakuwa na tabia za limbuken kma ww free lancer. I hate u mother***

Trofmo: Very disappointin… Ww km Kioo cha jamii unataka tuelewe vip hii picha?! Plz dis z Tz not states! Our culture is decency & dignity!!! Behave..

Chocolatedesweetness: This is too much……..!!! Umeanza kulewa mafanikio eeenhe, ngozi nyeusi taaabu sana, U better apologise and delete this photo before its too late!U shauri tu

FEZA KESSY NDANI YA MAPENZI MOTO MOTO NA ONEAL..APOKEWA KWA SHANGWE BOTSWANA


4Hakuficha mapenzi ya kweli aliyonayo kwa mpenzi wake mpya waliekutana kwenye jumba la BBA 2013, Mbotswana Oneal… kuna wengine walichukulia kama mzaha pale Feza alipohojiwa na kusema wazi kwamba anampenda kiukweli Oneal na chochote kinaweza kutokea kati yao.
Taarifa ikufikie kwamba tayari Feza ameshaondoka Tanzania na kwenda Botswana kwa mpenzi wake ambapo amepata mapokezi makubwa ambapo kunatarajiwa kufanyika party ya chakula cha jioni cha mastaa hao ambao watajumuika na watu wengine pia watakaolipa kiingilio.
1
2
6
358

DIAMOND PLATNUMZ ATAJWA SAKATA LA UNGA, AHUSISWA NA MTANDAO WA MASOGANGE


KWA mara ya kwanza tangu lilipoibuka sakata la watu maarufu kujihusisha ama na utumiaji au usafirishaji wa dawa za kulevya, jina la mwanamuziki anayeaminika kuwa na ukwasi mkubwa kwa sasa hapa nchini, Naseeb Abdulmaliki, maarufu zaidi kwa jina la Diamond, limeanza kutajwa kuwa ni miongoni mwa vigogo wa ‘unga.’

Tayari mjadala mkubwa wa chini chini umeibuka kwa watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wake, na taarifa ambazo zimelifikia MTANZANIA Jumatano kutoka vyanzo mbalimbali zimedai kuwa, mwenendo wa maisha ya Diamond sasa unachunguzwa na baadhi ya maofisa wa vyombo vya dola vya ulinzi na usalama.

Kutajwa kwa jina la Diamond katika sakata hili, kunatiwa nguvu zaidi na mwenendo binafsi wa maisha wa msanii huyo maarufu wa muziki wa kizazi kipya, unaokwenda sambamba na ukwasi mkubwa alioupata katika kipindi kifupi.

Kama hiyo haitoshi, safari za nje ya nchi za mwanamuziki huyo unaohusisha ziara zake nchini Afrika Kusini na Uingereza, pia ni mambo ambayo yamechochea wingu la mashaka lililofikia hatua ya jina lake kuingizwa katika mtandao huo ambao katika siku za karibuni, umewagusa pia baadhi ya watu wenye majina makubwa katika jamii.

Kuhusu ziara hizo, kilicholeta mshtuko na dukuduku dhidi yake ni kuwapo kwa taarifa kwamba, katika moja ya ziara hizo za nje ya nchi, Diamond alifikia hatua ya kusafiri akitumia chumba kinachotumiwa na wageni mashuhuri (VIP), badala ya njia ya wasafiri wa kawaida.

Mbali na hilo, taarifa nyingine zinaeleza kwamba, mizigo ya msanii huyo ambaye mara kadhaa amekuwa akisafiri na kundi la wacheza shoo wake, imekuwa ikipita pasipo kupitishwa katika hatua za ukaguzi kwa namna ile ile ilivyokuwa kwa mabinti wawili wa Kitanzania walionaswa nchini Afrika Kusini baada ya kuruka mfumo wa ukaguzi wa JNIA.

Aidha, ukaribu wa kimahusiano kati ya Diamond na baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini na ambao majina yao pia yameanza kuhusishwa na biashara hiyo ya mihadarati, ni jambo jingine ambalo limechochea harakati za kufuatiliwa kwa karibu kwa nyendo za Diamond.

Taarifa zaidi kutoka JNIA zinaeleza kwamba, miongoni mwa watu wanaoweza wakawa wamemponza Diamond ni wale ambao walionekana kuwa karibu na Agness Gerald ‘Masogange’ (25) na Melisa Edward (24), siku walipokuwa wakisafiri kwenda Afrika Kusini kabla hawajanaswa katika uwanja wa Ndege wa Oliver Thambo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, wakiwa na shehena ya dawa za kulevya.

Mwenendo wa watu hao unatiliwa shaka kuwa huenda ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya wenye maskani yao nchini Afrika Kusini, kwa sababu mbali na ukaribu na wasichana hao, pia walihusika kwa karibu kuusafirisha mwili wa mwanamuziki Albert Mangwair, aliyefia huko huko Afrika Kusini ambaye taarifa za kufa kwake ziligumbikwa na matumizi ya dawa za kulevya.

Alipoulizwa jana na MTANZANIA Jumatano kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu taarifa hizo na iwapo amekwishahojiwa na vyombo vya dola baada ya jina lake kuanza kutajwa kuwa miongoni mwa orodha ya wasanii wa muziki wanaosafirisha dawa za kulevya, Diamond alikiri kuwa na pesa za kutosha kuishi maisha anayoyataka, lakini akakana kujihusisha na biashara hiyo.

Akifafanua tuhuma moja baada ya nyingine kwa mpangilio aliokuwa akiulizwa na gazeti hili, Diamond alisema katika maisha yake, hajawahi kujihusisha na utumiaji au usafirishaji dawa za kulevya, lakini madai hayo yamekuwa yakitolewa dhidi yake na watu ambao hawajui siri ya mafanikio yake.

“Kazi ngumu siku zote inalipa, sasa napata matunda ambayo yanatokana na kile nilichokifanya, iweje watu wanitilie mashaka, Watanzania ni mashahidi wangu wananiona navyochumia juani, nitaendelea kulia kivulini tu kwani nakula kwa jasho langu.

“Siyo kweli kwamba mizigo yangu haikukaguliwa na kama haikukaguliwa na ingekuwa na kasoro, basi Uingereza wangenitia hatiani, nilipita na nilikaguliwa.” Alisema Diamond.

Alipoulizwa kuhusu taarifa za kuwa mwanamtandao wa kundi la Masogange, pia alikanusha kwa kueleza kuwa hata siku aliyosafiri kwenda Afrika Kusini alikwenda peke yake uwanja wa ndege na kuongeza kuwa alikwenda huko kwa shughuli za kimuziki, ambapo safari nzima iligharimu zaidi ya Dola 30,000 za Kimarekani.

“Afrika Kusini nimekwenda kufanya kazi zangu na safari hiyo imenigharimu zaidi ya Dola 30,000, nilikwenda kurekodi nyimbo yangu mpya inayoitwa namba moja ambayo itaanza kusikika hivi karibuni.

“Unajua Watanzania sasa hivi wanajua mtu hawezi kufanikiwa au kupata maendeleo bila kuuza ‘unga’, hili si sawa juhudi za mtu ndizo zinamfikisha alipo, na mimi juhudi zangu ndio zinanifikisha hapa, watu waache kunijadili vibaya.” Alisema Diamond.

Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja ikiwa ni takribani miezi miwili sasa tangu Watanzania wawili, Agness Gerald ‘Masogange’ (25) na Melisa Edward (24), waliokuwa na uhusiano wa karibu na baadhi ya wanamuziki maarufu hapa nchini, kukamatwa nchini Afrika Kusini wakiwa na dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya Sh bilioni 6.8.

Mbali na kuwa na uhusiano wa karibu na wanamuziki, Edward anadaiwa kuwa alikuwa mfanyakazi katika mgahawa mmoja maarufu jijini Dar es Salaam, unaomilikiwa na mmoja wa vijana matajiri hapa nchini ambaye hata hivyo gazeti hili halijafanikiwa kumpata ili kufanya naye mahojiano.

Wakati huo huo, tayari hatua za kinidhamu zimekwishaanza kuchukuliwa dhidi ya wafanyakazi wa JNIA waliohusika kupitisha kilo 150 za dawa za kulevya, ambao Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ametaja majina yao hivi karibuni na kuonyesha kwa waandishi wa habari ushahidi wa kuhusika kwao.

CHANZO: GAZETI LA MTANZANIA AGOSTI 21, 2013