Wema alitupia picha yake kwenye mtandao wa kijamii akionekana amekata nywele zote huku akiwa ameondoa kope za bandia na kutoa kucha alizobandika kuashiria kuuheshimu mwezi huu huku akibaki na kila kitu cha asili yake.
“Mwezi Mtukufu ni wa kuheshimiwa na kuweka kila kitu pembeni, nafurahi kuwa hivi kwa maana hata kama nikifunga swala zangu zitapokelewa vizuri,” alisema Wema.
No comments:
Post a Comment