MSANII wa filamu za Kibongo, Tamrina
Poshi ‘Amanda’ amesema anawachukia sana wasanii wa kike wa Bongo Movie
kutokana na tabia zao za kuchukuliana mabwana.
Amanda alisema wasanii wengi wa
filamu wana tabia za kuibiana mabwana kitendo ambacho kinamkera na
kusababisha kuwachukia kwani wanavyofanya siyo heshima na inawaharibia
sifa kwa jamii pamoja na kuichafua tasnia yao kwa jumla.
“Nawachukia na ndiyo maana sitaki
kuwa na rafiki Bongo Movie kwa sababu wamekuwa na tabia mbaya sana
mifano halisi ipo lakini siwezi kuitaja,” alisema.
Mbali na hivyo, Amanda alisema kuna
wasanii wawili wa kike walikuwa marafiki sana hata kwenye mitandao
walikuwa wakiitana mawifi lakini hivi sasa hawaivi, kisa kunyang’anyana
bwana
No comments:
Post a Comment