POOL PARTY
Thursday, July 11, 2013
"SIPO TAYARI TENA KUMVULIA NGUO MR. BOND.".....AUNT LULU
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amesema yeye na aliyekuwa mpenzi wake, Bond Bin Salim imebaki historia na kamwe hawawezi kurudiana naye japo anayajua mapenzi.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Aunty Lulu alisema ameshaamua kujituliza kwa mpenzi wake wa sasa hivyo hata iweje hawezi kurudiana na Bond.
“Jamani kwa sasa mnaona nimebadili kabisa staili ya maisha yangu hivyo Bond atabaki kuwa rafiki kama walivyo marafiki zangu wengine.
“Niliwahi kuachana naye kipindi flani baadaye tukarudiana kutokana na ukweli kwamba ni mwanaume anayejua kupenda na anayajua mapenzi ,lakini hii ya sasa ndiyo imetoka, kamwe siwezi kurudiana naye,” alisema Aunty Lulu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment