POOL PARTY

POOL PARTY

Wednesday, July 3, 2013

Nu joint: Nikumbatie / Joe Makini feat Fundi Samweli


Joe Makini ametambulisha wimbo wake mpya leo hii "Nikumbatie" akiwa amemshirikisha producer wa wimbo huo "Fundi Samweli."
"Huu wimbo ni wa mapenzi kwasababu wakati nau-record mwanzoni mwa mwaka jana kabla Fundi hajaondoka nilikuwa katika feelings hizo, na ilikuwa nitoe mda kidogo lakini wakati nataka kuuachia Nikki akawa anatoa wimbo wake, baada ya kutoa ikawa niachie lakini kutokana na msiba wa Ngwea na Langa ikabidi nitulie kwanza na sasa naona ni wakati muafaka wa kuachia"
Joe makini pia alizungumzia habari iliyopo sasa ya Mtayarishaji mkali wa Videos za kibongo "Adam Juma" kutangaza kuacha kutengeneza videos na kuangalia michongo mingine.
"Kweli hii habari sio nzuri kwasasbabu sidhani kama kuna atakae ziba pengo lake kwa sasa, ila najipanga kushoot video ya wimbo huu wiki ijayo, na bado sijajua nani atakae fanya video ya wimbo huu". amesema Joe.

No comments:

Post a Comment