Muimbaji wa THT Barnaba Elias amesema mama yake mzazi amefariki mapema mno na akiwa na umri mdogo.
Msanii huyo ambaye yeye na Amini wanaunda kundi liitwalo Gemini alikuwa akiongea na Bongo5 leo na kudai kwamba wimbo wao mpya ‘Why Mimi’ una uhusiano na msiba huo wa mama yake aliyefariki mwezi uliopita.
“Mimi mama yangu obvious nilikuwa nampenda sana. Mama yangu ndio mtu ambaye alisababisha Barnaba na ndio nimesimama hapa mnaniona Barnaba,”alisema na kuongeza
“Mzee yupo lakini power nyingi niliipata kwa mama, wote walikuwa wananisaidia vizuri lakini mama nilimzoea kwasababu mama alikuwa kipenzi changu zaidi ya kipenzi, mshkaji wangu zaidi ya mshkaji rafiki yangu wa dhati.
"Nilikuwa na uwezo wa kumwambia vitu vyangu vya ndani, nikamshirikisha akanisaidia, akanipa mawazo, tukataniana, tukacheka. Kwahiyo ni vigumu, ni neno ambalo huwa linarudi lakini siwezi kumkufuru mwenyezi Mungu.
"Ni neno ambalo huwa najiuliza why mimi? Sababu mama yangu amefariki akiwa kijana sana na ni ghafla sababu mama yangu mimi hakuumwa, kafa tu pressure, kwikwi, akapoteza maisha.”
No comments:
Post a Comment