POLISI
wametambua mwili wa mwanafunzi wa Howard University aliyeuawa kwenye
jaribio la uhalifu Alhamisi usiku. Omar Sykes, 22, na mwanafunzi
mwenzake walikuwa wanatembea maeneo ya 700 block of Fairmont Street
NW kabla ya saa 5.30 usiku walipofuatwa na watu wawili.
Polisi
wanaamini kulikuwa na jaribio la uhalifu ila yalitokea mabishano kabla
mmoja ya wale watu kutoa bastola na kumuua Sykes. Alifikia mauti kwenye
hospitali ya maeneo ya jirani.
“Tunadhani
ilikuwa jambo la ghafla na hatuna uhakika kama wanafunzi hao waliibiwa
mali yoyote” alisema Kapteni Bob Alder wa kituo cha polisi DC
alipohojiwa na News4. Mwanafunzi mwingine alipigwa na kitako cha
bastola na kujeruhiwa kichwani ingawa hana majeraha makubwa.
“Wanafunzi
wengi wamepatwa na hofu ya kutoka na kutembea usiku kwani hali hii
inaogopesha sana,” alisema mwanafunzi mmoja alipohojiwa na Megan McGrath
kutoka News4.
Maelezo
kamili kuhusu watuhumiwa bado hayajapatikana. Kulikuwa na matukio mengi
ya kujumuisha watu wakati wa tukio hivyo polisi wanatumaini kuwa
haitawia vigumu kwa wahalifu hao kujulikana. Sykes alipenda uandishi na
mara ya mwisho aliandika makala kwenye mtandao unaoitwa Our Black Pages
mnamo tarehe 11 Juni. Wasifa wake unaonesha kwamba alikuwa anasomea
Marketing na Public Relations. Mkesha wa sala kwa ajili ya marehemu
utafanyika shuleni kwao Jumamosi kuanzia saa 1 usiku.
Howard University imetoa maelezo yafuatayo kuhusiana na kifo cha Alhamisi:
“Tuna
huzuni kubwa kufuatia kifo cha mmoja wa wanafunzi wetu kilichotokea nje
ya shule. Mwanafunzi mwingine alijeruhiwa kwenye tukio hilo na
anaendelea na matibabu…. Polisi wa Howard University wanashirikiana
polisi wa mji ili kupeleleza tukio hili hatari. Tunawapa pole familia,
shule na wale wote walioguswa na tukio hili kwa namna moja au nyingine.
Huduma ya ushauri nasaha itapatikana masaa 24 kwa wanafunzi wote
watakaohitaji msaada katika kipindi hiki kigumu.
No comments:
Post a Comment