MWANAMITINDO na mtangazaji maarufu Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na
Mtangazaji Mussa wa runinga wamezua jambo kufuatia picha
zinazodhihirisha urafiki wao uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi kunaswa.
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ katika pozi na Mtangazaji Mussa.
Awali paparazi wetu aliinasa picha ya wawili hao ambayo kwa mujibu
wao, walipiga miaka kumi iliyopita na walipokutana tena mwaka huu
wakapiga mpya.Baadhi ya wadau walioziona kwa mara ya kwanza, waliibua minong’ono kuwa urafiki wao ni wa siku nyingi hivyo kuna uwezekano wakafikia hatua ya ndoa.
Musa na Jokate katika picha ambayo inadaiwa kupigwa miaka kumi iliyopita.
“Urafiki wao ni wa kitambo, wanaweza kuja kuoana kabisa sababu aina
ya maisha yao ni ya usiri sana,” alisema mdau mmoja ingawa wenyewe
wamesema hawana cha kuzungumza juu ya hilo
No comments:
Post a Comment