Chuo Kikuu cha Howard alichokuwa akisoma mtanzania aliyeuawa mjini Washington Dc, marehemu Omary Adam Sykes kinataraji kuuaga mwili wake leo jioni, viongozi mbalimbali akiwemo meya wa jiji la Washington DC Bwana Gray nao wanatarajiwa kuhudhuria.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia Swahili TV shughuli za
kumuaga marehemu zitafanyika katika ukumbi wa Andrew Rankin Memorial
Chapel ulio katika kona ya 6th Street na Howard place na
kufuatiwa sherehe za kukumbuka ya maisha yake zitakazofanyika katika
ukum bi wa Blackburn ambao pia uko katika chuo hicho.
Shughuli za kuuaga mwili huo zimepangwa kuanza saa 12 jioni (6pm), ambazo habari…
Na Swahili TV, Washington DCChuo Kikuu cha Howard alichokuwa akisoma mtanzania aliyeuawa mjini Washington Dc, marehemu Omary Adam Sykes kinataraji kuuaga mwili wake leo jioni, viongozi mbalimbali akiwemo meya wa jiji la Washington DC Bwana Gray nao wanatarajiwa kuhudhuria.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia Swahili TV shughuli za
kumuaga marehemu zitafanyika katika ukumbi wa Andrew Rankin Memorial
Chapel ulio katika kona ya 6th Street na Howard place na
kufuatiwa sherehe za kukumbuka ya maisha yake zitakazofanyika katika
ukum bi wa Blackburn ambao pia uko katika chuo hicho.
Shughuli za kuuaga mwili huo zimepangwa kuanza saa 12 jioni
(6pm), ambazo habari hizo zinasema Mstahiki meya Vicent condol Gray
atakuwa muongeaji mkuu akishirikia na rais wa chuo hicho Profesa Sidney
A. Ribeau. Sherehe hizi pia zitashirikisha familia ya marehemu Omar
ambaye baba yake mzazi mze Adam Sykes na baba yake mkubwa waliingia
jana wakitokea nchini Tanzania.
Si jambo la kawaida kwa Meya wa jiji kubwa la Washington
kuhudhuria sherehe za kuuga mwili, wachambuzi wa mambo ya siasa za
Washington Dc wanasema hali hiyo huenda inatokana na umaarufu wa chuo
hicho na mstuko mkubwa wa mauaji ya mwanafunzi huyo ambayo yamelistua
jiji la Washington DC, ambalo licha ya kuwa na matukio ya mauaji ya
hapa na pale lakini eneo la chuo hicho limekuwa salama kwa miaka mingi.
Taarifa ya chuo kwa Swahili TV inasema,Uongozi wa chuo uliamuwa
kuanzisha mfuko maalum utakaosaidia wananchi mbalimbali wasio na uwezo
kulipia ada zao, mfuko utatambulika kama Omar Scholarship Fund na tayali
watu kadhaa wameshaanza kuchangia.Taarifa za namna ya sifa na
uwasilisha wa maombi zitatangazwa baadaye.
Swahili TV itakuwepo katika shughuli za kuuaga mwili ili kukuletea habari za kina na uhakika.
No comments:
Post a Comment