Siku kadhaa tangu alipo-post picha akiwa amevaa taulo, huku mitandao
ikiripoti kuwa alikuwa supermarket akiwa nchini Marekani, Shilole
amekanusha kutembea na taulo supermarket na kusema kuwa alikuwa
akiogelea katika swiming pool iliyoko nyuma ya hoteli aliyofikia.
"Ile ilikuwa nipo swiming pool sawa, hoteli niliyokuwa ninakaa ilikuwa
na swiming pool pembeni, unajua miji ya wenzetu bana, imekaa yaaani
yaaani ukitizama hivi mtu anaweza akasema, ina maduka meengi, halafu
hoteli yetu sisi kubwa chini kuna swimming pool kwa nyuma, kwa hiyo mi
nilikuwepo kule nyuma pale swiming pool naoga, nimetoka kuoga ni Masanja
ndio akanipiga picha.
kwahiyo hiyo picha mi nimeitupia tu instagram, kwamba hakuna mtu ambae
anaweza kama, kama huku Tanzania mtu labda kusema unaweza ukasimamama
kutoka hapa, umetoka swmming pool si iko hapa, mtu labda akaanza
kukushangaa.
Nimejaribu kuona nimeona wenzetu huko wa Africa, hawana taimu na mtu
hata uvae kichupi hana taimu na wewe, yaani kila mtu anafanya mambo
yake, kwasababu hata sasa hivi kule ni kipindi cha summer, kwahiyo watu
wanavaa hivi, kwahiyo mi nilivyokua nimevaa vile sio kwamba nilikuwa
nimevaa naenda supermarket, nilikuwa naenda swimming pool." zaidi
msikilize hapo chini
No comments:
Post a Comment