Ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja toka staa
wa Bongo Luca Mkenda aka Mr Nice apoteze nafasi ya kufanya kazi na label
ya GrandPa ya Kenya kwa shutuma za uvivu, kushindwa kutoa ushirikiano
na ukiukaji wa mkataba hatimaye mlango mwingine umefunguka kwa nyota
huyo wa ‘Kikulacho’.
Mr Nice ambaye bado yuko Kenya
anatarajia kujiunga na label nyingine nchini humo ‘Candy Records’ ambayo
ina miezi michache toka ianzishwe.
Kwa mujibu wa CEO wa
label hiyo John Kariuki aliyekuwa akizungumza katika ufunguzi rasmi wa
label hiyo jijini Nairobi, alisema wako katika hatua za mwisho
kukamilisha mpango wa Mr Nice kusain mkataba nao kama ilivyoripotiwa na
Niaje.
Label hiyo tayari imesha wasain wasanii kadhaa wa
Afrika Mashariki akiwemo hit maker wa ‘Ulofa’ Top C wa Tanzania, pamoja
na wengine kutoka Kenya.
No comments:
Post a Comment