POOL PARTY

POOL PARTY

Wednesday, July 17, 2013

MAZISHI YA BABA WA JOYCE KIRIA-KABURI LAZUA MPASUKO, MAKABURI MAWILI YACHIMBWA, NI KAMA SINEMA.


      My Late Dad Michael Francis Iwambo Kiria, R.I.P

Huyu ndo baba yangu aliyefariki dunia 10/7/2013 huko mkoani Tanga ambako alikuwa anaishi na familia yake. Katika kizazi cha Babu yangu mzaa Baba,  anaanza Baba yangu mzazi kisha anafata huyu ambae ni Baba yangu mdogo (kwangu binafsi  hana tofauti na baba mzazi kwa namna tulivyoishi nae enzi za uhai wake)

HISTORIA
Kwa miaka mingi sana kumekuwa na MGOGORO WA ARDHI kwenye familia yetu, na kila malumbano yakitokea yanayohatarisha AMANI ya Familia, Baba Michael Kiria pichani alisimama kidete kuhakikisha Amani inakuwepo. 


TAARIFA ZA MSIBA
Siku ya Jumatano nilipokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za msiba wa Baba  aliyefia katika hospitali ya Mkoa Bombo, Kwa taarifa nilizopewa na mdogo wangu anaeitwa KIRI (Mwanae wa kwanza wa kiume) ni kuwa Baba alipata matatizo ya kupumua na katika harakati za kumkimbiza Hospitali alifia mapokezi mara baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Bombo.


PIGO LINGINE
 Taarifa za msiba nimezipata siku ya Jumatano, jana yake siku ya Jumanne nilikuwa nimetoka safarini mkoani Tabora ambapo nilikwenda kuhudhuria mahakamani Katika kesi inayomkabili mume wangu kipenzi, Baba wa watoto wangu wazuri Lincon na Linston, Henry Kilewo ambaye yupo katika gereza la Uyui akikabiliwa na tuhuma za kuhusika kumwagia mtu tindikali. Ni kitendo cha masaa tu kupita kisha napokea taarifa nyingine nzito katika maisha yangu! Ila baada ya muda nikajifariji na kusema kazi ya Mungu haina makosa, kubwa ni kumuomba anipe nguvu katika kipindi hiki kigumu katika maisha yangu na familia yangu kwa ujumla.

WAJIBU WANGU
Baada ya kuwasiliana na ndugu,  nikiwa ndo dada mkubwa huku nikijuwa wazi kwamba MHIMILI mkuu kwenye BOMA letu umeanguka na hakuna mtu mwingine wa kushulikia matatizo ya BOMA letu, ilinibidi kuyabeba majukumu yote kwenda nyumbani Kibosho Moshi kufanya maandalizi zaidi ya kumpumzisha salama Baba yetu kwenye nyumba yake ya Milele (Kaburi). So nikaanza kuaandaa taratibu za safari na kuwapa taarifa ndugu, jamaa na marafiki. Katika watu ambao nilikuwa nawapa taarifa nikapata mtu ambaye nae siku iliyofata ambayo nilipanga kusafiri alikuwa na safari ya kuelekea Arusha, hivyo aliamua kunipa lifti na gari yake hadi kunifikisha Moshi. Shukrani za dhati kwa Mh Grecy Kiwelu ubarikiwe sana Wifi yangu.


          Mh Grace Kiwelu (Wifi)

Dah hapa nikapata mawazo tena kuwaacha wanangu Lincon na Linston, mana wakati naendelea kupanga hii mipango wengi walinishauri nisiende na watoto, hali ya hewa Moshi ni baridi sana sana, Nikaona kwa kweli nawadhulumu wanangu muda mwingi siko nao, ila nasema tena hizi ni changamoto naamini yatakwisha na tutaendelea kuja kuwa happy family again"Poleni Wanangu Lincon na Liston.
Watoto wangu Lincon kulia na Linston

Siku iliyofuata Alhamisi tukaanza safari kuelekea mkoani Moshi, baada ya safari ndefu kidogo maeneo ya Mombo kupata chai kidogo.
   Tukiwa safarini          
Tukipata chai/Supu kidogo.

Baada ya kumaliza kula tukaendelea na safari, na tunamshukuru Mungu tulifika salama Moshi, Tukaagana na Mheshimiwa, yeye alikuwa bado na safari ya kuelekea Arusha. Sikwenda nyumbani moja kwa moja, tukaanzia madukani na sokoni ili kununua mahitaji mbalimbali ambayo yangeanza kutumika nyumbani kwa jioni ile na katika kipindi chote cha msiba. baada ya kupata tulivyovihitaji sokoni ndo tukaelekea nyumbani.
Tulifika home nikakutana na mama baada ya salamu, alinieleza mamwili matatu na kujua taratibu zinazoendelea.
With My Mum, Akini update mawili matatu baada tu ya kufika nyumbani.

Tukaongea mawili matatu kuhusisna na taratibu za msiba, na tukaandaa mipango kadhaa na siku ya Alhamisi ikawa imekwisha.
 Siku hiyoooo inayoyoma..

Ijumaa mapema tukaanza maandalizi ya pale nyumbani ya kila kitu kinachohitajika, na kuendelea kupeana taratibu kadhaa ya mipango ya mazishi.Namshukuru Mungu nilisimamia taratibu zote mpaka kuhakikisha ziko sawa.
Nikihakikisha kila kitu kipo tayari.
Mida ya mchana bado kuna baadhi ya maandalizi yalikuwa hayajakamilika ukizingatia siku inayofuata Jumamosi ndo siku ya mazishi ilibidi nizidi kwenda resi na shughuli za pale ili zikamilike.
Hapa Vijana wakianza kufunga maturubai.
Kazi ikiendelea.
Kazi ya kufunga turubai ikiwa imekamilika.
Ndugu wakiendelea kuwasili nyumbani kwenye msiba.
nikidiscuss mawili matatu na baba mdogo anayemfuatia marehemu.
After a long day, it's a MBEGE time...
Kiza kikiwa kimeshaingia.
Mpaka usiku huu sehemu kubwa ya maandalizi ilikuwa imekamilika.
Siku ya Jumamosi tukijiandaa kupokea mwili wa marehemu.
Msafara uliobeba mwili wa marehemu wakitokea Tanga wakiwa wamewasili nyumbani.
Wageni kutoka Tanga wagoma kushuka katika gari akiwemo mke wa marehemu pamoja na watoto wake.
Mwili wa Marehemu Baba ukitolewa kwenye gari baada ya muda wa nusu saa, hatukujua ni kwanini walichelewa kushusha Mwili.
Mwili ukiletwa nyumbani..
Vilio vilizidi kutawala mara baada ya mwili wa marehemu kushushwa nyumbani.
Mama Alizimia.
Hapa mama akipewa huduma ya kwanza baada ya kuzimia.
Mwili wa marehemu baba ukiwa ndani, kusubiria taratibu za mazishi.

Ndugu wa marehemu baba kutoka Tanga akiwepo mke wake baada ya kugoma kushuka kwenye gari, tulipewa sababu za kukwama huko kwenye gari kwamba kaburi lililokuwa tayari hawalitaki bali wanataka wamzike wanapotaka wao, kwa madai kwamba Baba aliacha Wosia wa wapi azikwe na wakaongeza kwamba, baba aliagiza mtoto wake wa mwisho wa kiume awe mtu wa kwanza kupiga jembe kwenye kaburi lake.  
Utaratibu wa familia hii ambao upo toka kwa waanzilishi wa mji huu babu na bibi eneo la makaburi limetengwa. alianza kufa bibi akazikwa hapo, akafuatia babu akazikwa hapo, akafuatia baba yangu mzazi akazikwa hapo. kwa hiyo baada ya baba mdogo kufariki kaburi lilichimbwa hapohapo pembeni ya hayo makaburi yaliyotangulia.
Kwa mbali ni kaburi la kumzika baba lililokuwa limeandaliwa pembeni ya makaburi mengine, ambalo familia ya marehemu kutoka Tanga walilikataa.

Hapa ilibidi kuitisha kikao cha UKOO kilichopelekea shughuli zote kusimama kwa lengo la kuwaelewesha na kuwaomba wakubali marehemu azikwe eneo la makaburi lililoandaliwa. 
Nilipata nafasi ya kuchangia 
Kiukweli hii hali ilinichanganya, ilinisikitisha, iliniumiza, ilinistua, ilinihuzunisha, ilinishangaza!!!!!!!!!! Kwa sababu kwanza ni ndugu zangu na zaidi ya hapo nilikuwa nawasiliana nao hatua kwa hatua jinsi taratibu zilivyokuwa zinakwenda. Wakati nikiendelea na maandalizi kule Moshi nilihakikisha nilihakikisha nafuatilia kujua kule Tanga kunaendaje, nini kimekwama, wanahitaji sapoti gani n.k
Nikafanya maandalizi yote kama ambavyo waliniamini kunipa majukumu ya kusimamia shughuli zote za mazishi nyumbani Kibosho
Niliwaomba sana na kuwasihi tuendelee na utaratibu wa kumpumzisha baba kwenye hiyo nyumba yake ya milele na kama kuna kitu chochote tutakizungumza baada ya mazishi...
Baada ya jitihada zangu za kuwasihi sana ziligonga mwamba na wakashikilia uamuzi wao wa kutaka kaburi lingine.
Muafaka wa suala hili ulikuwa ni kuwaacha wafanye wanachotaka (wachimbe kaburi lingine)  
Katika taratibu za kufukia kaburi la mwanzo, Wazee wa UKOO walidai kwamba Mila na desturi za kwetu ni lazima Kondoo azikwe kwenye hilo kaburi. 
Mtoto wa kwanza wa Marehemu akichinja Kondoo kwa ajili ya taratibu za kufukia kaburi la kwanza..
Mila zikiendelea katika kufukia kaburi 
Maandalizi ya kuchimba kaburi la pili, na mtoto anaeonekana amevaa jaketi ndo mtoto wa mwisho wa marehemu ambae wanadai baba yake alisema awe mtu wa kwanza kupiga jembe kaburi lake
Mwili ukisubiri kaburi la pili liwe tayari ili taratibu za mazishi zianze
Baada ya kaburi kuwa tayari, Mwili ukitolewa nje kwa ajili ya Ibada ya Misa.
Wakiandaa mwili kwa ajili ya kuaga
Heshima za mwisho
Mhimili wetu umedondoka na sasa BOMA limepasuka vipande vipande
Maskini Nguzo iliyoshikilia familia imedondoka. Ee Mungu wa Mbinguni mpasuko huu utatupeleka wapi??? Ni nani atakayetusimamia tena??? Ni nani atakayetuongoza??? Ni nani atakayeleta Amani kwenye mji huu????
Ibada ya kumuombea Marehemu ikiendelea
Baada ya Ibada Mwili ukapelekwa kaburini
Mwili ukisubiri kuwekwa kaburini
Mwili ukiingizwa kaburini
Mwili ukiwa tayari kaburini
Utaratibu wa mashada ukiendelea
Ee Mwenyezi Mungu nakuomba umlaze mahali pema peponi baba yangu kipenzi Mzee Michael Francis Iwambo Kiria. Amen
Swali kubwa ninalojiuliza kwa nini hawa watu wasikatae vitu vyoooooooote vilivyoandaliwa??????????? CHAKULA, MAPAMBO, MBEGE, VITI, MAGODORO NA MABLANKETI, MC NA MUZIKI...... KABURI TU!!

WAMEKUJA HAWAJABEBA CHOCHOTE ZAIDI YA MWILI WA MAREHEMU NA NGUO ZAO. SASA KWA NINI WAKATAE KABURI PEKEE??????!!!!!!!!!!!


ANYWAYS... NAMSHUKURU MUNGU KWA YOOOOOTE. SHUGHULI ILIMALIZIKA NA MAISHA YANASONGA

SHUKRANI
Nachukua fursa hii kuwashukuru watu wote walionisapoti kwa namna moja au nyingine, kwa hali na mali, Mwenyezi Mungu awabariki na awaongeze mara dufu

No comments:

Post a Comment