Mrembo aliyeuawa enzi za uhai wake.
UHUSIANO wa kimapenzi, ulioanzishwa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, umesababisha kifo cha mrembo nchini Nigeria.
Habari za mtandaoni zinadai kuwa mrembo huyo (jina halikutajwa) pamoja na boyfriend wake (jina pia halijatajwa), walikuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu.
Imedaiwa kuwa wakati wawili hao wakiwa kwenye utekelezaji wa hatua za mwanzo za kufunga ndoa, mrembo huyo alimtaarifu boyfriend wake kuwa amepata mpenzi mwingine kwa njia ya Facebook.
Chanzo cha habari kiliiambia tovuti moja ya nchi hiyo kwamba mrembo huyo alianzisha urafiki wa Facebook na kijana mmoja raia wa Marekani (jina halijatajwa) kabla ya kibao kubadilika na kuwa wapenzi.
Chanzo kiliendelea kupasha habari kwamba mrembo huyo na mpenzi wake wa Facebook, walidumisha uhusiano wao kwa njia ya mawasiliano ya simu kwa muda mrefu kabla ya kukata shauri la kuonana ana kwa ana.
“Yule kijana raia wa Marekani alitembelea Nigeria, akafikia hoteli moja kubwa. Yule mrembo akaenda kukutana naye na kutumia muda mrefu chumbani.
“Ni kama baada ya kukutana ndiyo mapenzi yaliongezeka zaidi, kwani alipoondoka hotelini, yule mrembo alirudi kwa boyfriend wake aliyepanga kufunga naye ndoa na kumueleza kwamba mapenzi yamekwisha.
“Baada ya kuambiwa hivyo, kijana aliyekuwa na mategemeo ya kufunga ndoa na mrembo huyo, alimpeleleza mpenzi wake na kubaini mahali ambako kijana kutoka Marekani alifikia.
“Siku iliyofuata alivamia kwenye ile hoteli, akamkuta mpenzi wake na yule kijana wa Facebook, hapo ugomvi mkubwa ulizuka.
Ugomvi haukuishia hapo kwa sababu kijana wa Nigeria aliahidi ni lazima aue mtu.
“Siku moja baada ya ugomvi hotelini, kijana wa Nigeria alimteka mpenzi wake na kumuua kwa kumkatakata na silaha inayodhaniwa kuwa ni panga,” alisema mtoa habari huyo.
Kwa mujibu wa mtandao huo mpaka pale habari hiyo inachapishwa, mtuhumiwa wa mauaji alikuwa hajakamatwa.
No comments:
Post a Comment