POOL PARTY

POOL PARTY

Thursday, July 11, 2013

DIAMOND AFICHUA KISA CHA KULALA NA UWOYA!

SIRI nje! Lile skendo la Rais wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kudaiwa kulala na mwigizaji Irene Uwoya ambaye ni mke wa ndoa wa mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ limevuja.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
KISA KAMILI

Huku akijua kabisa kuwa ataibua zogo kwa kuwa Uwoya ni mke wa ndoa wa mtu, kwa mara ya kwanza, Diamond ameamua kuanika kisa kilichomfanya kujiweka kwa muda kwa Uwoya.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika cha gazeti hili,…
SIRI nje! Lile skendo la Rais wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kudaiwa kulala na mwigizaji Irene Uwoya ambaye ni mke wa ndoa wa mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ limevuja.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
KISA KAMILI
Huku akijua kabisa kuwa ataibua zogo kwa kuwa Uwoya ni mke wa ndoa wa mtu, kwa mara ya kwanza, Diamond ameamua kuanika kisa kilichomfanya kujiweka kwa muda kwa Uwoya.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika cha gazeti hili, kilichomfanya Diamond kufikia hatua ya kumtongoza na kutoka naye kimapenzi, ni kitendo cha Uwoya kutoa  maneno ya kumponda huku akionesha waziwazi hali ya kumchukia kila walipokutana.
Irene Uwoya.
UWOYA ALIKUWA HAMPENDI DIAMOND
“Unajua Irene (Uwoya) alikuwa hampendi Diamond hata siku moja na mara nyingi alikuwa kila akimuona lazima amponde. Habari hizo zilikuwa zikimfikia mwanamuziki huyo kupitia mashoga wa mwigizaji huyo ambazo ndiyo zilichochea.
“Kufuatia hali hiyo, Diamond naye kila alipofikishiwa taarifa na mashosti wa Uwoya, alikuwa akijisikia vibaya mno ndiyo maana ‘Sukari ya Warembo’ alilazimika kumvizia Uwoya kwa hali na mali ili kumfanya ampende.
Uwoya na Diamond waliponaswa.
CHIKOKA ATAJWA
“Nakumbuka kwa mara ya kwanza Diamond alimtuma (Juma) Chikoka ‘Chopa’ kwa Uwoya ili amfikishie ujumbe wa yeye kumtaka.
“Chikoka hakufikisha taarifa hizo, kitendo ambacho kilimuuma sana lakini siku moja Diamond alikutana na Uwoya akiwa na Chikoka, maeneo ya Sinza-Mori (Dar), akamuomba tena Chikoka namba, akampa, hapo ndipo uhusiano ulipoanzia.
 “Siku mbili baadaye Diamond alizungumza vizuri na Uwoya.

GLOBAL NOMA
“Diamond aliomba ahadi ya kukutana na mwigizaji huyo, bila kuchelewa, Uwoya aliiva na kukubali ambapo walikutana kwenye ile hoteli mliyoandika (Global) kule Mbezi Beach (Dar) wakamalizana.
“Unajua Diamond alifanya hivyo kwa sababu ya kupondwa na washikaji zake kuwa anatamba kutembea na mastaa lakini hamuwezi Uwoya.
“Kwa hiyo utagundua chanzo cha yote ni mdomo wa Uwoya kutangaza kutompenda Diamond kwani alikuwa akimsema vibaya sana kwa watu wake wa karibu,” kilidai chanzo chetu.

BOFYA HAPA KUMSIKIA DIAMOND
Baada ya kujazwa habari hizo, mwanahabari wetu alilazimika kumtafuta Diamond ili kuhakikisha kama alichoelezwa kina ukweli ndani yake ambapo bila kinyongo, mkali huyo wa wimbo wa Kesho alifunguka:
“Dah! Japo yalishapita ila ni kweli Uwoya nilikuwaga nikipata taarifa kutoka kwa marafiki zangu kuwa alikuwa ananichukia sana.
“Nilikuwa nikijiuliza sababu za yeye kunichukia lakini nikawa sizipati hata kidogo na hata nilipochunguza niligundua kweli alikuwa hanipendi kabisa.
“Sipendi sana kuzungumzia ishu hiyo ila naweza kukubali kweli kuwa marafiki zake na wangu ndiyo walionichochea sana kukutana na Uwoya na sasa hatuna tatizo na tunaishi kwa amani na upendo ingawa mengi yamepita na yaliyosemwa sina sababu ya kuyashikilia, kikubwa tumuombe Mungu.”

KAMA KAWA UWOYA HAPOKEI SIMU
Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilimwendea hewani Uwoya lakini kama kawaida, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.

TUJIKUMBUSHE
Miezi kadhaa iliyopita, gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda liliripoti habari ya Uwoya na Diamond kunaswa usiku katika moja ya vyumba vya hoteli maarufu kwenye Ufukwe wa Bahari ya Hindi huko Mbezi Beach, Dar ambapo habari hiyo iliibua maneno lakini sasa mwanamuziki huyo amemaliza utata kwani nguzo na sifa kuu ya Global Publishers ni kuandika ukweli siku zote

No comments:

Post a Comment