POOL PARTY

POOL PARTY

Wednesday, July 31, 2013

MADEE AKAGULIWA LISAA LIMOJA UWANJA WA NDEGE SOUTH AFRICA KWA HOFU KUWA ANA MADAWA YA KULEVYA


Kwenye Exclusive interview na millardayo.com Madee amehadithia kila kitu kilichomtokea wakati anaingia tu Afrika Kusini siku kadhaa zilizopita ambapo hii imetokea kutokana na ukubwa wa habari, uzito wa tukio la wale Watanzania wawili wasichana waliokamatwa kwenye kiwanja cha ndege Johannesburg wakiwa na dawa za kulevya wakitokea Tanzania.
Madee anakwambia alipotua kwenye kiwanja cha ndege, kawaida huwa kuna utaratibu wa kuchekiwa hati ya kusafiria na ukaguzi mwingine ambao hufanywa na mitambo maalum kwa kila abiria anaeingia Afrika kusini, ni ukaguzi ambao unafanywa Airport kabla ya abiria kuruhusiwa kuingia kwenye nchi yenyewe.
Kilichomfanya Madee kusachiwa na kuhojiwa karibu dakika 60 ni pale tu aliposema anatokea Tanzania, kuna wazungu wawili wenye sare tofauti za kipolisi wakaanza kumsachi mpaka kufikia kumwambia avue t shirt yake, alivua t shirt na kubakiwa na nguo nyepesi ya ndani wakati huo abiria wenzake aliokwenda nao walikua wameruhusiwa.
Kati ya abiria wote waliokuja pamoja kwenye ndege, Madee na Mzimbabwe mmoja ndio walikaguliwa sana ila huyo mwingine alikaguliwa kidogo tu kama dakika 10 na wala hakuambiwa avue nguo.
Sehemu yenyewe Madee aliyoambiwa avue nguo sio kwenye chumba maalum, ni palepale kwenye foleni wanaposimama watu ila kwa pembeni kidogo, ni sehemu ambayo imezibwa na kioo kinacholingana na usawa wa tumbo kushuka chini…. Madee anakwambia jamaa walinong’onezana sana wakati wanamkagua.
Hata hivyo baada ya Askari hao kumuweka sana msanii huyu wa bongofleva kutoka kundi la TipTop Connection walimuomba radhi baada ya kumaliza ukaguzi wao ambao pia ulihusika kulivuruga sana begi lake.
Unataka kupata stori kamili? sikiliza AMPLIFAYA ya Clouds FM leo saa moja usiku, pia kwa Breaking News, habari yoyote ambayo ni habari, vituko, vichekesho, videos na music na mengine… jiunge kuwa mwanachama wa millardayo.com kupitia facebook https://www.facebook.com/millardayo au twitter https://twitter.com/millardayo pia instagram.com/millardayo ili uwe wa kwanza kutupiwa link kila tukio linapoandikwa.

MONALISA AGOMA KUOLEWA TENA BAADA YA NDOA TANO KUVUNJIKA


Msanii mkongwe  kwenye  soko  la  filamu  Tanzania,Yvonne Cherry "Monalisa"  amesema  hatarajii  kuolewa  tena  baada  ya  kuvunjika  kwa  ndoa  zake  kadhaa  ikiwemo  ile  ya  producer  Tyson....

Akisimulia  mikasa  ya  maisha  yake  mbele  ya   mwandishi  wetu,Monalisa  aliema  kuna  siku  walipokuwa  kwenye  kikao  cha  sendoff  ya  mama  yake, alitania  na  kusema  ataolewa  disemba  lakini  hakuwa  serious....

"Sina  mpango  wa  kuolewa  kabisa,kwanza  sina  mchumba, ntaolewaje?

"Siku  ile  nilikuwa  natania  tu kwa  sababu  sipo  tayari  kuolewa  na  kuachika  tena"..Alisema  Monalisa

ROSE NDAUKA ANASWA AKIPAPASWA NDANI YA GARI KABLA YA KUPELEKWA HOTELINI

 
Rose Ndauka  au  Aisha  anaweza  kuwa  ameitia  najisi  funga  yake  baada  ya  kunaswa akiingia  hotel  moja   iliyoko  kinondoni  jijini  Dar  kwa  kile  kilichoelezwa  ni  kwenda  kuivunja  amri  ya  sita  na  mwanamziki wa  bongo  fleva  Nassoro  Ayoub  "Nasry"   au  Tajiri Boy
 
Rose ambaye alisilimu mwaka jana  na  kupewa  jina  la  Aisha  baada  ya  kuchumbiwa  na mwanamziki  mwasisi  wa  kundi  wa  TNG Squad, Malik Bandawe, alifumwa na  kamera  za wakazi wa jirani na  hoteli  hiyo  mwishoni  mwa  wiki  iliyopita.....

Shuhuda  wa  tukio  hilo  amedai  kwamba  majira  ya  mchana  kweupe  gari  aina  ya  Toyota Mark  X lenye  rangi  nyeusi  liliwasili  kwenye  viunga  vya  hoteli  hiyo  na  kusimama  kwa  takribani  dakika  10  kisha  likaondoka  na  kwenda  kupaki  sehemu  nyingine  ambapo  ni  umbali  mfupi  toka  hotelini  hapo...
  Kitendo  hicho  kiliibua  mashaka  miongoni  mwa  watu  hasa  kutokana  na  vioo  vya  gari  hilo  kuwa  tinted  hivyo  kutowaonesha  waliokuwemo  ndani...

"Walipoondoka  na  kupaki  palipojificha  tuliamua  kuwasogelea  ili  tujue  ni  akina  nani

"Baada  ya  muda, kioo  cha  dereva  kilishushwa kidogo, tukamuona  dogo  anayefanana  na Diamond  akiwa  anampapasa  demu  aliyekuwa  pembeni  yake...

"Tulipoona  hivyo, tulidhana  mnyamwezi  ameamua  kumaliza  mambo  yake  ndani  ya  gari, hivyo  tukaziweka  simu  zetu  standby  kwa  ajili  ya  kushuhudia" alisema shuhuda  huyo

Baada  ya  muda, mlango  wa  kulia  ulifunguliwa  kisha  wakamuona  dogo  aliyetambuliwa  kwa  jina  la  Nasry

"Kumbe  hakuwa  Diamond,alikuwa  ni  dogo  Nasry.Tulipotupa  jicho  ndani, tulihamaki  kumuona  Rose  Ndauka  akibadili  nguo  na  kujitanda  baibui.

"Nadhani  alifanya  hivyo  ili  watu  wasimjue  pindi  atakaposhuka  kwenye  gari  maana  aliposhuka  tu, waliongozana  na  dogo  Nasry  kwa  mwendo  wa  kasi  hadi  ndani...

"Toka  walipoingia  ndani  hadi  walipotoka  iliwachukua  kama  masaa  matatu  hivi.Wakati  wa  kutoka, Nasry  alilifuata  gari  hadi  mlangoni  na  kisha  Rose  akaingia  na  kutokomea"...Kilimalizia  kusimulia  chanzo  hicho

-Habari  kwa  hisani ya KIU

Tuesday, July 30, 2013

KESI YA LADY JAYDEE YAPIGWA KALENDA



MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, leo ililetwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na wakili anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na kumtuma mwakilishi wake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama Kuu kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo.
Kwa mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia blogu yake.

FEZA AONGOZA KUCHUKIWA NA WENZAKE NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER


Habari mbaya kwa Tanzania, Feza Kessy ni miongoni mwa washiriki watatu waliopigiwa kura zaidi kutoka wiki hii...FEZA amepata kura nyingi zaidi hii inaonyesha kuwa ndio mshiriki anayechukiwa zaidi ndani ya jumba hilo...
Feza ameungana na mpenzi wake Oneal na Elikem kwenye kikaango hicho cha eviction. Wa kwanza kumtaja Feza kwa kudai kuwa ni mbeya na jinsi anavyopenda kuwakusanya washiriki wenzake na kuwashawishi mi Msouth, Angelo.

Beverly wa Nigeria pia amemtaja Feza kwa madai kuwa ana upinzani mkali kwenye shindano hilo.

Elikem amewataja Oneal na Feza huku Cleo wa Zambia akimtaja Feza kwa madai kuwa ni tishio kubwa kwake na kusema wazi kuwa hataki kumuona Feza anaondoka na dola laki tatu.

Haya sasa muda wa kuanza kumpigia kura Feza Kessy asitoke ndio huu.

SINTAH " NASUBIRI KUPIGWA NA SHILOLE KAMA ALIVYO AHIDI-SAFARI ZA UKUBWANI MAJANGA"


"Heee aliposema Sintah akarukiwa kwenye media zote nini na nini mbuta nanga.
Nothing personal to be honest ila watanzania tusipende kudanganyana jamaniii, juzi tu tulikuwa na kampeni za kwenda World Cup 2014 Brazil na kamati zikaundwa za kutosha tu, leo hakuna hata anayejua ndoto zimefia wapi now heeee.


Mtu anayekupenda lazima akwambie ukweli, truth sets a person free sasa sielewi kwa nini sie watanzania hatupendi critics rather tunapenda urahisi wa maisha vitu vitokee tu pap ndo maana mabinti wanaamua kubeba madawa e.t.c TUSIPENDE KURAHISISHA MAISHA

Joke of the year ni pale mtu hana hata album, nyimbo mbili/tatu tu za mdumange anakuja kutuambia eti Jenifer Lopez kafurahi anataka kufanya naye nyimbo kiruuuuuu. Charity begins at home, hujawagusa hata kina Lady Jaydee sogeasogea mpaka kwa kina Wahu na Juliana Kanyomozi kwanza ndo at least uje utudanganye Lolest. Kuna tofauti gani sasa kati ya huyu na wale waliotuambia tutaenda Brazil 2014?????


Tukijipanga timu yetu ya taifa itashiriki World Cup. Why not?
Msanii ukijipanga hakuna kinachoshindikana, nini JLO unaweza fanya featuring hata na Jay Z lakini sio kutuletea mambo ya mfalme njozi kwa kuwa umepata sponsor kakusafirisha basi mburula mwanzo mwisho. 

kuwa exposed ukubwani linaelekea kuwa janga la taifa sasa....Dont hate critics, you can learn a lot from them!

I had to say that because nasumbuliwa sana na media kila mara simu na interviews, I got nothing to hate on nothing... Im always honest nasubiri kupigwa now kama alivyoahidi Lolest. 

Thx kwa wale mliokuwa mna mtazamo kama mie coz sio wanafiki, Mungu anapenda sana wasema ukweli.


sitaki tena media yeyote sasa iniulize hili swala that's it, huu ndio ukweli wangu na sipendi kupigiwa simu kwasababu sitaki kumpa mtu hypes za kumtajataja, got better things to do than discuss issues that aint no valuable.

Monday, July 29, 2013

MAKALA:NANDO AMEIANGUSHA TANZANIA


Kama ilivyokuwa kwa Watanzania wengi, usiku wa jana ulikuwa mgumu sana kwangu. Mara nyingi nimekuwa nikiwashangaa mashabiki wa soka wanavyojikuta kwenye huzuni kubwa baada ya timu yao kufungwa.
Wengine hukosa hata hamu ya kula kwa siku kadhaa. Kwakuwa mimi si shabiki wa mpira, sijawahi kupata hisia hii. Lakini hatua ya jana usiku ya Biggie, kumchinjia baharini mwakilishi wa Tanzania wa Big Brother Africa, Ammy Nando aliyekuwa akitegemewa na wengi kuwa mmoja washiriki wanaoweza kuwa washindi wa mwaka huu, ilinifanya nihisi hisia kama wapatazo mashabiki wa soka, huzuni. Ni sababu iliyonifanya jana nilale mapema.

Nando aliondolewa (disqualified) kwenye shindano hilo kwa kuonesha utovu wa nidhamu, kumshambalia na kumtukana mshiriki mwenzie Elikem, na kumtishia maisha.

Ni kweli Nando alistahili adhabu ile na kwa kiasi kikubwa, ametuangusha sana. Japokuwa bado tuna matumaini kwa Feza Kessy, lakini kuondoka kwa Nando kumeiondoa hamu ya si tu Watanzania kufuatilia shindano hilo, bali kwa mashabiki wengi wa nchi nyingi za Afrika waliokuwa wanampenda Nando.

Mbaya zaidi ameondoka kwa sifa mbaya, uhuni, ujana wa kijinga, utoto, usela ma*i, ulimbukeni na hasira za mkizi. Nando alikuwa amebakiza wiki chache tu kufika kwenye mstari wa mwisho wa shindano hilo na huenda maisha yake yangebadilika milele kwakuwa alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda.

Alichokifanya Nando ni sawa na mwanafunzi aliyebakiza wiki mbili afanye mtihani wa taifa halafu anamtukana mkuu wa shule/chuo, usela ma*i haswaaa.

Nando alisahau kuwa ule ni mchezo na hauhusiani kabisa na maisha ya nje. Huenda hakupata muda wa kuzipitia vizuri sheria za shindano hilo, labda asingejiingiza kwenye fujo na uhuni wa aina ile.

Siku zake nzuri na za kuvutia kwenye jumba hilo, zimeharibiwa na dakika chache zilizotiwa dosari na mdomo wake na maamuzi ya kitoto ya kujifanya John Cena ama Floyd ‘Money’ Mayweather.

Uamuzi wa kumpa kibuti Nando, ulichukuliwa na Big Brother kufuatia ugomvi uliozuka Ijumaa hii kati yake na Elikem.
Bahati mbaya ni kuwa Nando ndiye aliyeuanzisha ugomvi huo na hivyo kumfanya avunje baadhi ya sheria za Big Brother.

“Any Housemate who becomes physically violent will be removed from the House immediately. Violence can refer to self-inflicted violence, or violence towards another. Violence includes provocation, goading, bullying and victimisation,” alisema Biggie.

Lakini katika msimu huu, Big Brother alianzisha sheria iliyopewa jina ‘Three Strike Rule’ ambayo itatumika kwa mshiriki atakayefanya kitendo kikubwa cha kuvunja sheria za shindano hilo.

Kutokana na ugomvi huo, Nando alipata Strike yake ya pili huku Elikem akipata moja.

Baada ya hapo, Nando aliitwa kwenye Diary Room na kupewa Strike ya tatu kwa kutishia maisha ya Elikem kwa kusema: “I feel like stabbing him. A nigga like that deserves to die”, (Najiskia kumchoka kisu. Mtu kama huyo anastahili kufa)
Mbaya zaidi ni kuwa, Nando alikutwa akiwa amelala na mkasi chini ya kitanda na hiyo si mara ya kwanza kukutwa akiwa na silaha kwenye jumba hilo. Ni wazi uwepo wa Nando kwenye BBA ulikuwa tishio kwa maisha yaw engine, ni kweli alistahili kutolewa ili kuepusha shari.
Mwezi uliopita alipata Strike ya kwanza na onyo kali kutoka kwa Big Brother baada ya kwenda na kisu kwenye party ya Channel O. Kisu cha nini sehemu kama hiyo? Nando bhanaa.

Umiliki wa silaha ama kusudi la kufanya ukatili kwenye jumba hilo ni kinyume na sheria za Big Brother.
Baada ya Diary session Nando jana, Nando aliambiwa afungashe virago mara moja huku pia Big Brother akitoa onyo kwa washiriki wengine kuishi kwenye jumba hilo kama watu wazima.

Biggie alikuwa na maana kubwa kuwaambia washiriki waliosalia ‘kubehave kama watu wazima’ kwakuwa tabia aliyoionesha Nando ni ya utoto uliopitiliza. Ana miaka mingapi vile?

Itawachukua muda mrefu Watanzania waliokuwa nyuma yake kumsamehe kwa ujinga alioufanya.

Bado haijulikani kama Nando anakuja Tanzania moja kwa moja ama ataenda Marekani alikokuwa akiishi. Kama atachagua kuja kwanza Tanzania, basi ategemee mapokezi hafifu kwakuwa amezivunja roho za watu wengi waliokuwa wakimpenda.

Nando atakuwa na wakati mgumu sana akija kuendelea na maisha ya kawaida kwakuwa amezingua kwa namna nyingi.Usisahau kuwa ana wakati mgumu pia kwa watu wa Ghana kwakuwa atatakiwa kusawazisha scandal yake na aliyekuwa mshiriki wa nchi hiyo, Selly ambaye anamtuhumu kuwa alimwambukiza STD. Kiufupi Nando ni adui mkubwa wa Ghana kwa sasa.

Selly anadai kuwa hakufanya mapenzi na Nando na mama yake amepanga kumshitaki Nando kwa kuchafua jina la bintiye, na ameshawasiliana na watayarishaji wa shindano hilo. Anasema ameshapimwa na wala hana ugonjwa wowote wa ngono na kwamba hajui Nando aliupata wapi ugonjwa huo.

Tusubiri kuona maisha mapya ya Nando akirudi mtaani. Pamoja na kutoka kwa aibu, bado atakuwa na future nzuri kwenye fashion industry barani Afrika na hata kwenye filamu, hasa zile za action!! Lol.

Hizi ni baadhi ya reactions za watu mbalimbali baada ya Nando kuondolewa kwenye shindano hilo.

Jocelyne Maro

If he had stayed composed he definitely would have won…what a wrong way to leave the house…shame…

$un$hine☀

Nando was a weak chap! U don’t brag about stabbing people n think thats strength. Be gone gangsta wannabe Tanzanian #BBATheChase

Godfrey Rugambwa

Nando umetuvua nguo watanzania mbele ya waafrika wote bro! Sasa nchi zote za Afrika zimeelewa kuwa hivyo ndivyo watanzania tulivyo! SAD. Namuangalia Bimp anakusanya kila kilichokuwa cha Kaka yetu (Nando) huku akiwa anahema vibaya sana! The dude is so damn cool All the best bro

KW ‏@keezywear

Nilikuwa naamini Nando angechukua 300 USD za #BBATheChase, but I was wrong… Ungeacha uhuni wako kwa siku chache zilizobaki Nando!!!

Hakeem Mandaza

Nandoooooo…… :( :( :( not happy

Christine Sintah

Kwanza Biggie kamuhurumia Nando kuanzia ijumaa mpake leo, hasira hasara , bambii Bimp

SebaTheWarrior: u cant threaten somebody’s life and expect people to treat u the same the next day..that’s how the cooky crumbles

♥ FEZA ♥ NANDO ‏@HPhillipo

Biggie jamanii why plsss why biggie whyyy ooooh! NandooooOoooo ☹#BBATheChase

jacqueline ulotu

Shame Tanzania.. Nando disqualified from the game.. #BBATheChase

Source:Bongo 5

DIAMOND PLATNUMZ AENDA SHULE SOUTH AFRICA KUONGEZA VIDATO

The Bongo Flava Prince, Diamond Platnumz yupo nchini Afrika Kusini alikoenda kuongeza vidato kidogo. Apparently, hitmaker huyo wa Kesho amejiunga na chuo ambacho hakijajulikana jina lake bado na hajasema ameenda kusoma nini.

Kupitia Facebook, staa huyo amewauliza mashabiki wake wabashiri ameenda kusoma nini chuoni hapo na haya ni baadhi ya majibu.

Faiso Yahya: Ka si english course basi unenguaji

Galus de Focus: HOTEL MENEGEMENT

Benjamin Osarya Jr.: Unasoma matangazo….kwenye notes board.

Nelson Choka: Samahan form 4 umemaliza ww et..!! Labda una risit dogo mh

Rose Selestini: Unatafuta wadada wa chuoni.

Christian Biseko: wa kusoma uwe wewe??? Elimu siyo mchezo wewe!!!

Gara B Kubwa: English Course ili Ushiriki BBA mwakani…una Mbwembwe dogo wewee..

Emmanuel Makaga: Unasomea jnc ya kubun skendo mpya kwny mass media

Gabrie Lbrighton: Wanaosoma hawajitangazi wew may be ungetuambia akitoka huyu mwanamke uliye nae nani anafata.
Nàdhifá Dórnald Unasomea mapenz maana unayapenda sana.

Friday, July 26, 2013

IRENE UWOYA AREJEA NCHINI NA SALAMU KUTOKA KWA MSWATI-AMEAIDIWA MAMBO MAKUBWA

Mwigizaji Irene Uwoya amerejea nchini toka nchini Swaziland alipokuwa kwa takribani wiki tatu.
Irene Uwoya aliyerejea nchini leo hii amerejea na salamu toka nchini Swaziland alizoziandika kupitia ukrasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii alisema…
“Mswat anawasalinmu sana! Nahiv karibun atatinga hapa nakanipa kibali chakufanyya move na ful suport...I wl prove u wrong...try me”
Akimaanisha, amerejea nchini na Mswati amnawasalimia sana na amesema atakuja nchini hivi karibuni na amenipa kibali cha kufanya Filamu na atanisaidia kwa kila kitu. Nijaribu nitakuthibitishia kuwa umekosea (Kwa Kiswahili fasaha).
Bado tunamtafuta Irene amabye namba yake ya simu haipatikani kujua kama kauli hii ni ya kweli au anawatania tuu mashabiki wake.

ASHLEY TOTO ANAWATAKIA WAISLAM WOTE MFUNGO MWEMA


Ashey Toto.Anawatakia Waislam Wote Mfungo Mwema ....

MUONEKANO MZURI WA WASHIRIKI WA BIG BROTHER KUTOKA TANZANIA WAWASAIDIKIA KUPETA BIGBROTHER



ChaseFeza3LRG 
The good looking duo of Feza and Nando has done well to fly the Tanzanian flag high in this season of Big Brother The Chase.
This is the ninth week of the game and both Feza and Nando don’t look like they will be leaving anytime soon.
Nando is the resident bad-boy with a colourful personality, while Feza is as fiery as the bright colours she wears on her hair.
We put together some up close and personal pictures of this fun loving pair for your viewing pleasure. How long would you like to see these two stay in The Chase?
ChaseFeza1LRG
ChaseFeza2LRG

ChaseFeza4LRG
ChaseFeza5LRG
ChaseFeza6LRG
ChaseNando1LRG
ChaseNando2LRG
ChaseNando3LRG
ChaseNando4LRGChaseNando5LRG

Thursday, July 25, 2013

UJUMBE MZITO KUTOKA KWA IRENE UWOYA KWENDA KWA JOHARI


Katika pita pita zetu leo hii tuliweza kupata ujumbe mmoja mzito na wa kutia moyo toka kwa mwanadada Irene Uwoya aliomwandikia mkongwe wa bongo movies nchini kwa upande wa kinadada Blandina Chagula maarufu kama Johari wiki chache zilizopita.
Ujumbe huu wa Irene ni ujumbe wa kutia moyo na unaweza kuwa kama “Motivation message” kwa wadada wengi hapa mjini ili badala ya kukaa na kuwaza kupata mali au mafanikio kwa njia za mkato au zisizo halali basi wafanye kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi.
Tukinukuu ujumbe huo Irene kwa Johari aliandika….
“Wewe nimwanamke wapekee...mchapakaz sana...atawaongeee vp kaza moyo...one thng u hav to know if God say yes no body I mean no body can say no...so don gv r f*ck
Hii inawahusu wadada wote jamani. Nyie ni wanawake wapekee, wachapakazi, kazeni moyo. If God say yes, nobody can say no (Mungu akisema ndio hakuna awezaye kusema hapana)

JEURI YA FEDHA WEMA SEPETU AVUTA MKOKO UNAOENDANA NA RANGI AIPENDAYO ZAIDI KATIKA MAISHA YAKE


Haya ndio Maneno ya Martin Kadinda aliyoandika facebook na kuweka picha ya Wema akiwa na gari hilo

"samahani kwa ubora wa picha kuwa hafifu....... Ila huyu dada anapenda pink kupitiliza..... haya she gat new pink Car.... mkutane barabarani..." aliandika Martin

BAADA YA KUPIGWA CHINI BIG BROTHER, HUDDAH AAMUA KUMALIZA HASIRA ZAKE KWA KUJIPIGA UCHI


Wengi waliamini  kwamba    Big Brother  imempa  fundisho  mrembo  huyu  na  kutegemea  mabadiliko   makubwa  ikiwa  ni  pamoja  na  kuuuheshimu  mwili  wake  baada  ya  Video  zake  za  uchi  kuvuja  akioga  bafuni...
Hali  imekuwa  ni  tofauti  kwa  mrembo  huyu  asiyeijua  thamani  ya  mwili  wake.Tabia  ni  ngozi.Skendo,picha  za  uchi  huenda  ziko  katika  mishipa  ya  damu  yake....
Hizi  ni  picha  zake  za  nusu  uchi  alizotupia  mtandaoni.
 

PENZI LA FEZA KESSY NA ONEAL LAZIDI KUPAMBA MOTO KWENYE JUMBA LA BBA.....FEZA KESSY AKIRI KUFA KIMAHABA


“We’re getting more serious,” Feza alimwambia Big Brother. “Kukutana na Oneal kwenye nyumba hii kumeonesha upande wangu ambao sikudhani watu wangeuona, alisema Feza. Upande wa ulaini na udhaifu wangu. Marafiki zangu nyumbani wanasema nimekuwa rahisi sana na napotea. Mtu mmoja anahitaji kwa kiasi fulani kuwa mjinga kwenye uhusiano. Ni ngumu sana pia, sababu wakati mwingine nataka kuwa mkali na siwezi sababu uhusiano huu si tu unanihusu mimi. Unanihusu mimi Oneal na Africa.” Feza alimwambia Biggie kuwa yeye na mpenzi wake huyo raia wa Botswana wana hamu kubwa siku wanaondoka mjengoni humo kwenda kuundeleza zaidi uhusiano wao.

JOKATE, MUSSA KIPANYA WAZUA JAMBO

MWANAMITINDO na mtangazaji maarufu Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Mtangazaji Mussa wa runinga wamezua jambo kufuatia picha zinazodhihirisha urafiki wao uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi kunaswa.

Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ katika pozi na Mtangazaji Mussa.
Awali paparazi wetu aliinasa picha ya wawili hao ambayo kwa mujibu wao, walipiga miaka kumi iliyopita na walipokutana tena mwaka huu wakapiga mpya.
Baadhi ya wadau walioziona kwa mara ya kwanza, waliibua minong’ono kuwa urafiki wao ni wa siku nyingi hivyo kuna uwezekano wakafikia hatua ya ndoa.
 
Musa na Jokate katika picha ambayo inadaiwa kupigwa miaka kumi iliyopita.
“Urafiki wao ni wa kitambo, wanaweza kuja kuoana kabisa sababu aina ya maisha yao ni ya usiri sana,” alisema mdau mmoja ingawa wenyewe wamesema hawana cha kuzungumza juu ya hilo

Wednesday, July 24, 2013

Mwezi mtukufu wa Ramadhan: Tunda Man aachia Qaswida


Tikiwa ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhan, msanii kutoka Tiptop Connection ametengeza wimbo aina ya Qaswida (wa dini ya kiislam). Ingawa sijausikia bado, lakini Tunda amethibitisha kuwa nao na kutoa fursa kwa yoyote anae uhitaji kumtumia email yake au kwa kutumia whatsapp kwa mwenye namba zake za simu.

IRENE UWOYA NA LUCY KOMBA WASHIKANA UGONI


NYOTA wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krrish’ ametoa kali ya mwaka baada ya kudai kwamba amemshika ugoni msanii mwenzake, Lucy Komba mara baada ya kuziona picha za msanii huyo akiwa na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ wakiigiza filamu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutokea nchini Swaziland, Uwoya amepinga vikali utetezi unaosemwa kwamba Lucy na Kataut walikuwa wakishuti filamu na anaamini kuwa msanii huyo ameamua kumzunguka na kutaka kuibomoa ndoa yake.

“Lazima kuna kitu kinaendelea kwani katika dunia hii sijawahi kuona filamu inayochezwa na watu wawili tu mwanzo mpaka mwisho, ninachotaka kusema  ni kwamba Lucy ana mpango wa kuiharibu ndoa yangu,” alisema Uwoya kwa hasira.


Uwoya amehoji usiri wa filamu hiyo na kila alipokuwa akimpigia simu mumewe alikuwa akimjibu kwamba yuko Rwanda kumbe alikuwa Bongo akiigiza filamu na Lucy.
 

“Kwanza Lucy ashukuru niko mbali, laiti ningekuwa karibu angenieleza vizuri kwa sababu hata yeye angeweza kunipigia simu na kunifahamisha ushiriki wa mume wangu kwenye filamu hiyo kwa kuwa namba zangu anazo, ilikuwaje hakufanya hivyo?” alihoji.

Kuonesha kwamba amechukizwa na kitendo hicho, Uwoya alisema kwamba akitua Bongo atamtafuta Lucy ili aweze kumshughulikia vizuri na ikiwezekana amuoneshe hiyo filamu waliyoigiza watu wawili tu.

“Nitatua Bongo siku si nyingi na cha kwanza ni kumtafuta Lucy, anieleze vizuri kuhusu filamu hiyo waliyocheza na mume wangu,” alisema Uwoya.

Filamu hiyo ambayo imekuwa maumivu makubwa kwa Uwoya, imechezwa na Lucy na Ndikumana tu mwanzo hadi mwisho na imepewa jina la Kwa Nini Nisikuoe.

MA PRODUCER WALIOCHANGIA BONGO FLAVA KUINUKA-MASTER JAY V/S P.FUNK MAJANI NANI MKALI ?


Ni ma-producer wakali toka enzi hizo waliochangia kuinua muziki wa Bongo. Je, yupi unamkubali zaidi?

Master Jay V/S P.Funk Majani

SHILOLE MATATANI WIZI SIMU ZA DIAMOND


Stori:Shakoor Jongo na Musa Mateja
STAA wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameingia matatani akidaiwa kuingia mitini na simu tatu za mkononi alizoaminiwa nchini Afrika ya Kusini alikokwenda kufanya shoo.
Msanii huyo alikumbwa na kasheshe hilo Julai 19, 2013 nyumbani kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sinza Mori, Dar.
Siku hiyo Diamond alikuwa akifuturisha na aliwaalika watu mbalimbali wakiwemo mastaa lakini nusura futuru iingie doa kufuatia zogo hilo.

ISHU ILIKUWAJE?
Ndugu wa Diamond aitwaye Majaliwa Majuto ‘Q Boy’ alidai ndiye mwenye simu hizo. Alisema miezi kadhaa iliyopita, Shilole alikwenda nchini humo kufanya shoo ya muziki. Wakati wa kuondoka alimpa simu tatu, Ipad, Samsung Galaxy na Blackberry ili akifika Bongo ampe Diamond lakini msanii huyo hakufanya hivyo.

“Alikuja Sauzi kufanya shoo, wakati wa kuondoka nilimpa simu tatu amletee Diamond lakini nashangaa hakufanya hivyo na mimi tangu nirudi Bongo simpati, kila nikimpigia simu hapokei, leo ndiyo tumekutana hapa kwa Diamond,” alilalama Q Boy.
DIAMOND ALIAMBIWA SIMU ANAZO SHILOLE
Alisema awali akiwa nchini humo baada ya kumkabidhi mali hizo, alimpigia simu Diamond na kumtaarifu kuwa ‘mzigo’ anao Shilole, akashangaa staa huyo kujibu kwamba hajazipata wala hajamwona Shilole.

SHILOLE AJITETEA
Katikati ya mzozo huo, Shilole alijitetea kwa kusema: Mi namdai rafiki yake fedha yangu ya shoo iliyobaki, kama shilingi laki nane hivi ndiyo maana nikaamua kuzizuia simu za huyu (Q Boy) hadi nimaliziwe pesa yangu.
Hata hivyo, katika sakata hilo ilielezwa kuwa Shilole na Q Boy hawakuwa na makubaliano yoyote kuhusu shoo hiyo na simu hizo hivyo madai ya mwigizaji huyo ni ‘usanii’ tu.

MAMA DIAMOND AINGILIA KATI KUOKOA
Zogo hilo lilipopamba moto na kuashiria kuvurugika kwa amani, mama mzazi wa Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ aliamua kuingilia kati na kuagiza suala la kudaiana simu lifanyike kesho yake (Jumamosi) kwa vile siku hiyo haikuwa muafaka.
“Jamani! Jamani! We nani, Shilole na we Majaliwa, naomba kwa leo muepusheni shetani kwani hapa si mahali pake, ila kesho tutaitana na kumaliza suala hili, mimi mwenyewe nitalisimamia,” alisema bi mkubwa huyo na kumaliza henyahenya iliyoibuka.

JUMAMOSI YAFIKA, KIKAO VIPI?
Jumamosi, mapaparazi wetu walifuatilia ishu hiyo nyumbani kwa akina Diamond na kuulizia ili kujua kama kikao cha usuluhishi kilifanyika kama mama Nasibu alivyoagiza.
“Mh! Sijaona kikao chochote, kwanza Shilole mwenyewe akipigiwa simu hapokei,” alisema ndugu mmoja wa Diamond huku akiomba hifadhi ya jina lake.

MSIKIE DIAMOND
Juzi, Diamond alipopigiwa simu na kuulizwa kama anaijua ishu ya simu, alikubali.
Staa huyo alisema anashindwa kuingilia kati sakata hilo kwa sababu wahusika wote ni watu wake wa karibu kikazi.
“Yeah! Ishu ni kweli ipo, lakini mimi nilijiweka kando mapema, nikamwambia dogo (Q Boy) afuatilie mwenyewe baada ya kuona Shilole haeleweki.
“Unajua Shilole ni mwanamuziki mwenzangu, dogo yupo ndani ya Kampuni ya Wasafi Entertainment (ya Diamond), sasa kukomaa na ishu za simu tu nahisi itanishushia hadhi, napiga shoo za hela nyingi halafu leo nakomaa kwa hela ndogo, inakuwa siyo,” alisema Diamond.

SHILOLE TENA
Baada ya kuzungumza na Diamond, Shilole alipigiwa simu na kuomba kufafanua kwa undani ishu hiyo ambapo katika hali isiyotarajiwa, alimlalamikia paparazi wetu akidai anapendelea katika sakata hilo.
“Nyiye mnamtetea tu yule dogo, mimi sina tatizo, kama rafiki yake (aliyemuitia shoo Afrika Kusini) akinilipa hela yangu nawapa simu zao,” alisema Shilole.
Msanii huyo alikwenda mbele zaidi kwa kumwambia paparazi kuwa atatia timu kwenye Ofisi za Global Publishers ili kuzungumzia suala hilo na viongozi.
Baadaye Shilole alifika ofisini kwetu na kufafanua juu ya sakata hilo ambapo alirudia kukiri kuzuia simu hizo akidai kwamba anamdai Q Boy hivyo mpaka atakapomlipa ndiyo atampa simu zake.

Q BOY NAYE TENA
Kwa upande wake, Q Boy alipozungumza na paparazi wetu siku hiyo alisema amekusudia kwenda kufungua kesi kituoni ili apewe msaada zaidi wa kisheria kwa vile simu hizo zinamuuma hasa ukizingatia kuwa yeye siye aliyempeleka Shilole Afrika Kusini kufanya shoo.
“Mimi leo (Jumatatu) nimebanwa sana, kuna sehemu nakwenda na Diamond, nadhani nitamaliza jioni. Lakini kesho (Jumanne) nitaamkia polisi kufungua kesi nione watanisaidiaje?” alisema Q Boy.

POLISI AGUSIA ISHU
Risasi Mchanganyiko lilizungumza na askari mmoja kutoka Kituo cha Polisi cha Oysterbay na kummegea mtiririko wote, kisha kumuuliza kama kuna kesi ambapo alijibu:
“Japokuwa mimi si msemaji wa jeshi (la polisi), lakini ishu kama hiyo shitaka lake lipo, ni wizi wa kuaminiwa. Unajua wengi wanadhani kuibiwa lazima mtu uwe hujui, lakini mtu akifanya kama hivyo alivyofanya huyo msanii nani sijui (Shilole), kama ni kweli, kosa linakuwa wizi wa kuaminiwa endapo atafikishwa polisi.”

DIAMOND, Q BOY WALIFANYA MCHEZO?
Hata hivyo, baadhi ya watu walioshuhudia sakata hilo walikuwa na maswali kibao yaliyokosa majibu.
Swali la kwanza: Shilole alikwenda kufuturu kwa mwaliko wa Diamond na alijua staa huyo na Q Boy ni wamoja na simu alizopewa ilikuwa amletee msanii huyo, kwa nini alikwenda huku akijua ana msala?
Swali la pili: Kama Shilole alikwenda akijua Q Boy hayupo Bongo, je! Si kwamba ulikuwa mpango wa wawili hao kumwita ili wampe kibano ateme simu zao?
Swali la tatu: Je, ni kweli Shilole alizuia simu ili amaliziwe deni lake kwa mtu aliyemuitia shoo Afrika Kusini au shetani alimwingia baada ya kutua Bongo na kuamua kuzitumia hasa ikizingatiwa kuwa siku hizi mambo ya Instagram ndiyo habari ya mjini?

Tuesday, July 23, 2013

Kelly Rowland aokolewa baada ya kupotea baharini kwa masaa 12



Wasamwahi huwa tunasema "maneno huumba", nikiangalia hii story inayomuhusu Kelly Rowland kuokolewa baharini, nakubaliana kabisa pale nikiifikia video ya wimbo wa Destinys Child "Survivor" ambayo kuna kipande kinamuonyesha Kelly akiwa katikati ya bahari huku akiwa hajui pa kuelekea.
 In reality hii imetokea  kwa Kelly siku ya Ijumaa ambapo aliokolewa baada ya kukaa baharini na kutokujua wapi pa kuelekea kwa masaa 12.
Rowland na wengine nusu dazeni walikuwa kwenye chombo cha baharini kwaajili ya kwenda kujionea  nyangumi  (Ijumaa asubuhi) wakiangalia kujiingiza katika nyangumi, lakini ghafla walikutana na wimbi lenye urefu wa futi 5 na kusababisha ukungu, hatimae kuwapotezea muelekeo.
Nahodha wa meli akawa dhaifu na hajiwezi kutokana na hali hiyo, hata hivyo Master wa bandari alifanikiwa kupiga mahesabu yake na kufanikiwa kurudisha meli hiyo .
Nahodha Nuhu Santos alifawaokoa kila mmoja na kuwarudisha mida ya saa 5 ya Ijumaa usiku huku kila mmoja akiwa anatetemeka kivyaake.
Santos anasema siku ya pili yake, alipokea shukran binafsi kutoka kwa Rowland mwenyewe alipokutana nae  akiwa na mkewe out kwa ajili ya dinner, na Kelly aliwalipia chakula walichokula. Mpaka dakika hii Kelly hajaongea lolote juu ya hilo.
Kelly akiwa na aliemuokoa

Picha: Quick Rocka (The Switcher) akiwa ndani ya studio zake mpya "Switcher Records"



Tuddy Thomas nae alipita kucheki vitu vipya ndani ya studio mpya ya Quick Rocka

Mark Zuckerberg alishawahi kuhisi 50 Cent amefanya kazi kwake (facebook)


50 Cents hajawahi kumaliza high school, lakini alishawahi kuaminiwa kuwa "mkuu wa maendeleo ya biashara  na mauzo" kupitia facebook 2005.

Wakati nafasi ya  mwanzilishi mwenza wa Facebook, Saverin Eduardo (mkuu wa maendeleo ya biashara  na mauzo) kuchukuliwa na Kevin Colleran, Zuckerberg alimchanganya kijana huyo na mega superstar 50 Cent kutokana na picha ya profile yake inayomuonyesha akiwa na 5o Cent.


Hivi ndivyo jinsi ilivyokuwa siku ya kwanza walipokutana Zuckerberg na Colleran uso kwa uso..

Zuckerberg alipanga kukutana na Colleran mbele ya Virgin  Megastore iliyopo New York Union Square, Colleran alifika akiwa amechelewa na hivyo kuelekea moja kwa  moja alipo Zuckerberg huku akipokea simu kutoka kwa huyo huyo Zukerberg akimuuliza "Uko wapi", Colleran akamjibu nimpo mbele yako. Zuck alimuangalia kwa mshangao sana, alidhani muuza matangazo ya facebook ni yule jamaa aliekuwa akionekana  mweusi na tafu sana kwenye profile picture (50 Cents)

Rais wa Facebook na mwanzilishi wa Napster, Sean Parker alimwambia Colleran kuwa mkutano na Zuckerberg ulikuwa wired sana sababu "sisi tulidhani ungekuwa African-American."

Wakati wa mkutano wao, 50 Cent alikuwa tayari kashauzwa rekodi zaidi ya milioni 8 na album yake ya kwanza Get Rich Or Die Trying, na moja ya single zilizofanikiwa sana kwenye radio kwa muda wote  "In Da Club" na alikuwa kashasainiwa Dr Dre na Eminem.

NAY WA MITEGO ASHANGAA KUONA WASHINDI WA BSS WAKIFULIA LICHA YA KULIPWA PESA ZA KUTOSHA

 Hit maker wa Muziki Gani, Nay Wa Mitego ametuma salamu kwa mwandaaji ya shindano la Bongo Star Search, Rita Paulsen kuhusu zawadi wanayopewa washindi wa shindano hilo ambayo huwa haiwafikishi popote.
 
“Hizi Salamu ziende kwa Madam Rita na bongo star search. Mshindi analipwa nini mbona kama magumashi?! Namuona Walter Chilambo kapigika km zamani, haji ramadhani kachoka yupo kitaani. 


"Nauliza milioni hamsini zao anazila nani, acheni ubabaishaji wekeni mambo hadharani. #966#, salam zao# my new track,” aliandika Nay Wa Mitego kupitia Instagram.

ROSE NDAUKA AKANUSHA HABARI ZILIZO SAMBAA KUWA NI MJA MZITO

Mwanadada Rose ndauka amekanusha habari zilizoandikwa jana kwenye mitandao mbalimbali nchini kuwa huenda yu mjamzito kutokana na tukio la kuugua ghafla na kupandwa na kichefuchefu alipokuwa location akitengeneza Filamu yake mpya (kama nayoonekana pichani)
Akizungumza na mtandao wa Swahili World Planet, Rose ndauka amesema kuwa habari hizo si za kweli na wala yeye hajaongea jambo kama hilo
 "sio kweli na kilichoandikwa sijakiongea" hata sijui wamepata wapi hizo taarifa. Alinukuliwa akisema Rose ndauka

Cheki Feza alivyopagawa alipoiona video yake, “Amani ya Moyo” kwa mara ya kwanza ktk BBA House

Post navigation

BBA UPDATES:NANDO NA DILLISH WAONDOA TOFAUTI ZAO BAADA YA NANDO KUTANGAZA KUWA DILLISH ALIMSHIKA SEHEMU NYETI


Uh-oh is Dillish and Nando's friendship on the rocks? The two former Diamonds spent a good portion of the night airing out their differences.
From the looks of things, today's comical court session had some not so funny consequences. The Namibian was not impressed by Nando sharing in front of everyone that she had jokingly touched his penis.
She felt that he was being inappropriate talking about things that are real during a joking court session. "You come in the shower and touch my boob and I laugh because it is just a joke. I didn't go around sharing that with everyone," said Dillish.
The Namibian told her buddy that the reason that their friendship has changed is because she doesn't know if she can just joke around with him anymore without knowing if he will take things personally. She said: "That's why I only want to chill with Melvin, because I know that he will just laugh about things".
Meanwhile Nando said that he was not happy with Dillish assuming that he takes things personally without asking him. "I hate when you make me feel like sh*t," said the Tanzanian.
In the end, the two both agreed that they still like being friends and they went back to their playful ways; laughing and joking with one another.

TID"SIO KWELI KWAMBA NYIMBO ZA ALI KIBA ZINAPENDWA MUSCAT OMAN, MIMI NDIO NAPENDWA ZAIDI HUKO"



 Khalid Mohamed, Top In Dar (T.I.D) ambae pia ni mmiliki wa Top Band amepinga vikali taarifa zinazoonesha kuwa Nyimbo za msanii mwenzake Ali Kiba zinasikilizwa zaidi Muscat huenda kuliko msanii mwingine wa Bongo Fleva.

Taarifa hizi zilizotolewa na mtandao wa Bongo5 ambao ulipata maelezo ya kina baada ya kuchat na mtanzania aishie nchini Muscat aliyetambulika kwa jina la Rayya Al Habsi aliyewapa tathmini kuhusu nyimbo za kibongo zinazosikilizwa zaidi huko mjini Muscat,Oman.

Rayya alisema nyimbo za Ali Kiba zinasikilizwa sana lakini pia wasanii wengine wanaopendwa ni Diamond Platinumz, Ommy Dimpoz na Dully Sykes.

Rayya aitaja pia upande wa mduara kuwa ni AT, Off side Trick na Kilimanjaro Band, na kwamba band inayofunika zaidi ni Twanga Pepeta.

Taarifa hizi zinakuja wakati ambapo T.I.D amepata deal la kwenda mjini Muscat kupiga show akiwa na band yake ‘Top Band’, na hivyo ameona kama taarifa hizi zimepotoshwa na yeye ndiye alistahili kutajwa katika nafasi aliyopewa ‘Ali Kiba.’ Na kwamba yeye ameshapiga show mara mbili na anaenda kwa mara ya tatu akiwa na band yake.

Kupitia ukurasa wake wa facebook T.I.D a.k.a Mnyama amedondosha  maelezo confidently.

“This came after I have been mentioned perfoming well its too late for this reminder its my time,and they listen to me alot its my third time perfomin there and this time with my band.”

Kisha akaambatanisha na kichwa cha habari chenye picha ya Ali Kiba kama kilivyoandikwa na Bongo5, yenye kichwa cha habari “Nyimbo za Ali Kiba zinasikilizwa zaidi Muscat ‘huenda’ kuliko msanii mwingine wa Bongo Flava.”
Well, yale yanaweza kuwa ni maoni ya Rayya, maoni sio utafiti rasmi japo unatoa picha ya jumla. Lakini inaonekana kama Top In Dar hataki kuwa Down any where hivi hivi.