Alfajiri ya leo, mtangazaji wa
ITV anayejulikana kwa jina la Ufoo Saro amejeruhiwa vibaya kwa
kupigwa risasi na mchumba wake ambaye baada ya tukio hilo naye
alijipiga risasi na kujiua.
Akizungumza na mpekuzi wetu, kamanda
Wambura ambaye ni kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa
kinondoni amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo.
Kamanda wambura amedai kuwa mwanaume
aliyetenda mauaji hayo ni mchumba wake na alikuwa anafanya kazi
katika umoja wa mataifa ( UN ) huko sudani ila bado haijafahamika
kitengo alichokuwa akifanyia kazi.
Kwa mujibu wa Kamanda Wambura,
inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa
kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro(mama
mkwe) ili awasuluhishe
Baada ya usuluhishi kuanza na
kuonekana kuwa tatizo liko kwa mwanaume, mwanaume huyo alimshutumu
mama mkwe wake kwamba amekuwa na mazoea ya kumtetea mwanae na
ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake na Ufoo Saro risasi ya
kichwa na kumuua papo hapo....
Alipomuua mama huyo, mwanaume huyo
alimpiga Ufoo Saro risasi mbili , moja ya tumboni na nyingine ya mguuni
na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe
risasi ya kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.
No comments:
Post a Comment