POOL PARTY

POOL PARTY

Friday, October 25, 2013

KWA MARA YA KWANZA MZEE MAJUTO AUTAJA MSHAHARA WAKE ANAOPATA KWA KUIGIZA KWA MWEZI


Ni nadra sana kwa Mastaa wengi wa Tanzania kukubali kusema kiwango anachopata kwa mwezi kutokana na kazi yake ya umaarufu ila kwa Mzee Majuto ni kinyume, amekubali kusema kila kitu kwenye kipato cha movie zake za vichekesho ambazo mpaka sasa ndio zinashika namba 1 kwa mauzo Tanzania?
Kwa sababu ni kiapo cha millardayo.com kuhakikisha chochote ambacho ni stori unakipata, imempata Mzee huyu Mbembe kutoka Kigoma akiwa ni mzaliwa wa Tanga umri ukiwa miaka 65 na kukubali kuzungumza kwenye hii Exclusive interview.
Akiwa ni baba wa watoto tisa, anakwambia ‘kwenye movie za kuigiza sasa hivi kama mtu akitaka kunishirikisha ni lazima unilipe milioni nane kutoka milioni 2 au tatu nilizokua nazikusanya mwanzoni, hii bei nimeibadili kuanzia mwezi September 2013, mimi kadri ninavyocheza movie nyingie za kushirikishwa ndio nazidi kujipunguzia kipato changu kwa mwezi kutoka kampuni ya STEPS iliyoniajiri’
‘Mpaka sasa nimecheza movie zaidi ya 600 toka nimeanza kuigiza za kushirikishwa na zangu mwenyewe, nilianza kulipwa zaidi ya milioni moja kwenye movie toka mwaka 2007/2008 baada ya kuwa na kampuni ya Ally Riyami ambae alikua ananilipa shilingi laki sita kwa kila movie ya Comedy kwa hiyo kwa mwezi napata mpaka kwenye milioni 6 au saba kutokana na idadi ya movie nitakazoigiza’ – Mzee Majuto
‘kwa sasa hapa Steps nalipwa kuanzia milioni 17 mpaka 20 kwa mwezi, ni malipo mazuri sana ambayo napata kila mwezi na nimepangiwa kucheza movie 9 kwa mwaka lakini kule Ally Riyami kwa mwezi ndio nilikua nacheza hizo movie 10, yani unacheza movie mpaka unasikia kizunguzungu…. kwa sababu nilitakiwa kucheza movie 1 kila baada ya siku tatu ila kwa sasa kwenye mkataba wa Steps nacheza movie moja ya kampuni na moja ya nje ya kampuni, maisha mazuri’ – Mzee Majuto

No comments:

Post a Comment