Nisha alisema kuwa hata yeye alipitia msoto kama huo kabla ya kuto hivyo anajisikia huruma na industry hii ili izidi kukua ni lazima mastaa wa sasa wawaandae wasanii chipukizi ambao ndiyo watakaotingisha siku za mbele na kuzipeleka filamu za Tanzania katika level za kimataifa. Hii ina maana kuwa baada ya filamu hii mpya ya Nisha kuingia sokoni hivi karibuni atafanya usaili mwingine wa wasanii wachanga amabo atafanya filamun mpya nao. "nawapenda sana wasanii chipukizi nikiwaona huwa nasikia uchungu mpaka machozi hunitoka kwa wanavyohangaika kila siku kutafuta sanaa naahidi kuwasaidia" alisema Nisha
Hongera sana Nisha kwa hilo. Kazi kwenu wenye vipaji kuanza kumsaka Nisha alipo.
-Bongomovies.com
No comments:
Post a Comment