POOL PARTY
Sunday, October 20, 2013
AY " VIDEO YA BILA KUKUNJA GOT DIRECTOR ALIWEKA VITU AMBAVYO HATUKUVITARAJIA KABISA"
Ikiwa ni wiki moja imepita
tangu video iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ya Hamis Mwinjuma aka Mwana FA na Ambwene Yessaya aka AY ya single yao ‘Bila kukunja goti’ itoke, FA amezungumzia mambo mbalimbali kuhusu video hiyo.
Kupitia kipindi cha Showtime cha Radio Free Africa ya Mwanza, FA amezungumza juu ya matarajio aliyokuwa nayo katika video hiyo na kile walichokipata baada ya kuiona video kwa mara ya kwanza.
“Always unakuwa na mawazo mengine unakuwa unafikiria kitu ambacho ungetarajia kitokee kwenye video yako kwenye wimbo wako mara nyingi, lakini that is the personal perception tu aah not necessary kile unachofikiria kitokee kitatokea, mimi binafsi nilikuwa nafikiria kitu kingine kabisa, lakini jamaa kaja na vitu vingine kabisa kama zile colors nini ah kanichanganyia habari mi naona vitu vingine ambavyo sikuvitarajia na vitu ambavyo nilikuwa navitarajia vingine havikutokea, but am all good”. Alisema FA
Upande wa gharama FA hakuwa tayari kutaja kiasi kilichotumika lakini amesema wametumia pesa nyingi ikiwa ni pamoja na kumlipia J. Martins gharama ya kumsafirisha kutoka Nigeria hadi Afika Kusini na gharama zote za kukaa siku tatu nchini humo.
“hilo ni swala ambalo tumekuwa tunajaribu kuliruka sababu gharama mara nyingi zimekuwa zinaleta matatizo lakini jua hela nyingi imetumika, imagine kama kumtoa J.Martins kutoka Nigeria kumsafirisha business class kumuweka hotel ya Michelangelo …..kwa siku tatu alizokaa yeye South Afica na vitu kama hivyo”. Aliongeza FA
FA licha ya kutopata kile alichokitarajia katika video hiyo lakini ameusifia ubora wake ambao amesema ndio kati ya sababu zilizochangia video hiyo kupitishwa na vituo vikubwa vya kimataifa kama Trace, MTV Base, na Channel O.
“moja ya vitu vimeniridhisha sana kwenye hiyo video ni quality yake achana na kila kitu kingine angalia quality yake, ndio maana imeweza zile Televisheni kubwa za muziki za Afrika zote tulizokuwa tunazilenga hiyo video imepita, kwahiyo it is a hundred percent success”.
Kama umeshaiona video ya ‘Bila kukunja goti imefanyika mazingira ya ndani (studio) FA amezungumzia sababu za kuamua kubadilisha wazo lao la mwanzo la kufanyia mtaani.
“walitupa mifano halisi wakatuambia angalia video za nje kwa mfano ukiangalia video za YMCMB na ukiangalia video za Jay Z, zote zinafanyika ndani, it’s a trend sasa hivi yani inabidi watu wafanye hivi, kuna video mbili tatu ambazo zinafanyika nje lakini trend ni kwamba video zinafanyika ndani za dunia, ndo mkondo umekuwa hivyo. Kwahiyo jamaa aka-make sense si tulikuwa tunafikiri kwamba tungeweza kufanya mtaani …..”.
Baada ya audio ya Bila kukunja goti kutoka, FA na AY walitoa mchongo kwa mashabiki wao kujirekodi style ya kucheza bila kukunja goti na ku upload clips za video hizo katika mtandao wa youtube, na kuahidi kwamba washindi wangepata nafasi ya kushiriki katika video hiyo, FA ameelezea sababu iliyokwamisha zoezi hilo.
“namna pekee ambayo tunayofikiri labda ni kuwazawadia wale ambao tunafikiri wamefanya vizuri kwenye hili , kwa sababu idea ya kutumia dancers ilishakufa wakati tunaenda South Africa kwasababu gharama na nini hatuwezi kuwasafirisha wale jamaa wanaofanya video waje kufanya hapa, that’s one lakini pia lile swala la kwamba video tunataka kuifanya ndani likawa limeondoa ile idea ya kwamba sisi tunataka dancers, watu wawe wanacheza mtaani bila kukunja goti na nini….kwahiyo tunafikiria namna ya kufanya na hizi videos, bado videos zipo na tunajua zinatudai”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment