STAA wa filamu Bongo, Salma Jabu
‘Nisha’ amesema kuwa katika maisha yake hakuwahi kufikiria kujihusisha
na masuala ya muziki, isipokuwa aliingia katika fani hiyo kwa kufuata
mkumbo.
Akipiga stori na paparazi wetu, Nisha
alisema imekuwa ni aibu kubwa kujikita kwenye fani hiyo na kukaa kimya
kwa kipindi kirefu kwa kuwa hana mapenzi ya dhati na fani hiyo kama
ilivyo kwenye filamu.
“Niliona waigizaji wanaingia kuimba
na mimi nikaingia, nilivamia fani tu ndiyo maana najuta, nimeamua nikae
chonjo kwanza na mambo hayo nijikite zangu kwenye filamu,” alisema
Nisha.
No comments:
Post a Comment