POOL PARTY

POOL PARTY

Saturday, October 26, 2013

DIAMOND ATOA SIRI 5 ZA KUMRUDIA WEMA


Stori: Shakoor Jongo na Musa Mateja


MKALI wa songi linalotamba runingani na redioni ndani na nje ya Bongo la Number One, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ amefunguka na kuanika siri tano za kurudiana na Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.

Wiki mbili zilizopita, wakiwa Hong Kong, China, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii viliripoti kurudiana kwa Diamond na Wema waliomwagana takriban mwaka mmoja uliopita ambapo staa huyo wa Bongo Fleva aliibuka na kukanusha vikali akidai kuwa picha zinazomwonesha yuko na Wema ni za Filamu ya Temptations.

Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa dakika ishirini katika mahojiano maalum jijini Dar mara tu baada ya kutua kutoka China Jumatano iliyopita, Diamond alikiri kufaidi penzi la Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006.

Diamond alisema kuwa, Wema ndiye aliyetangulia kwenda China ambapo yeye aliungana naye siku kadhaa baadaye akitokea kwenye shoo nchini Malaysia.

SIRI YA KWANZA
Akianika siri za kujikuta mikononi mwa mwigizaji huyo mwenye mashabiki wengi zaidi katika tasnia ya filamu za Kibongo, Diamond alisema kwanza ni ukarimu aliopewa na mrembo huyo.

Alisema kuwa alipotua Hong Kong alishangaa kukutana na mapokezi ya Wema kwenye uwanja wa ndege jambo ambalo hakulitegemea.

“Alinionesha ukarimu wa hali ya juu mno. Wakati tulipokuwa hapa Bongo tulikuwa hatusalimiani.
“Kuna vitu vingi vya ajabu vilitokea huko nyuma kati yangu na Wema. Sikufikiria wala kuwaza kama anaweza akawa mkarimu kwangu kiasi kile.

Akaongeza: “Kwa mazingira yalivyokuwa, kwa namna yoyote lazima mwanaume aliyekamilika arudishe moyo nyuma na kuacha mambo mengine yaendelee.


“Kiukweli nisema tu kuwa hata tungekutana Morogoro au Dodoma kwa ukarimu ule mwisho wa siku tungerudisha uhusiano wetu.”

SIRI YA PILI
Diamond alisema baada ya mapokezi ya nguvu, Wema alimpeleka kwenye hoteli ya nyota tano (five stars) ambapo huko alipatiwa huduma ‘klasiki’ na kujiona kama yupo kwa mama Nasibu vile.

SIRI YA TATU
Alifunguka kuwa kitendo cha Wema kuwa mwenyeji wake China ambako alikuwa mgeni hadi akapazoea nacho ni siri nyingine iliyochangia wao ‘kukumbushiana’.

SIRI YA NNE
Alisema kuwa mwanadada huyo alimuonesha mapenzi mazito (yaani kutekwa kimapenzi) hivyo haikuwa rahisi kumchomolea kwani waliishi kama ndiyo penzi jipya linachipuka, akajikuta akiogelea naye. 

SIRI YA TANO
Diamond alisema kuwa bado ana ndoto ya kupata mtoto kupitia kwa Wema ambaye anajua kuwa alishamwambia lengo lake juu ya kupata naye uzao hivyo katika nyakati za kukutana kwao anaamini ndoto itatimia.

HAKUNA CHA FILAMU
Alipoulizwa juu ya madai kuwa walikuwa wakirekodi filamu, Diamond alifunguka kuwa hakuna cha filamu wala sinema na kama kuna mtu anasubiri filamu atakaa sana.

“Naomba nikiri kuwa kweli zile picha hazikuwa za filamu wala nini bali ndivyo hali halisi ilivyokuwa kati yangu na Wema kule China.
“Pia naomba niseme kuwa uhusiano wetu wa kimapenzi uliishia China na sasa hivi tumebaki kama kaka na dada na ni ruksa kila mtu kumtumia mwenzie katika kazi mbalimbali kama ataona kuna ulazima wa kufanyika hivyo,” alisema Diamond.
Hii ni mara ya kwanza kwa Diamond au Sukari ya Warembo kukiri kuwa kweli alirudisha penzi lake kwa Wema walipokuwa nchini humo wakijiachia.

PENNY HANA CHAKE?
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Diamond, ukifuatisha simulizi hiyo ya mapenzi kati ya msanii huyo na Wema, ni dhahiri kuwa mpenzi wa sasa wa jamaa huyo, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ hana chake kufuatia usaliti huo.


Hata hivyo, jitihada za kumtafuta Penny ziligonga mwamba kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa lakini juzi wanahabari wetu walipofika nyumbani kwa Diamond, Sinza-Mori, Dar waliambiwa mrembo huyo alilala hapo na kuondoka asubuhi.

No comments:

Post a Comment