POOL PARTY

POOL PARTY

Thursday, October 24, 2013

DOGO JANJA ATIMULIWA MTANASHATI ENTERTAINMENT-WALIMLETA KWA NDEGE SASA WAMRUDISHA KWA BASI


Msanii chipukizi wa muziki wa Hip Hop, Abdulaziz Chende maarufu kwa jina la Dogo Janja, ametimuliwa katika kundi la Mtanashati Entertainment.
Akizungumza na Mtandao huu, kiongozi wa Mtanashati Entertainment Ustaadh Juma Namusoma alisema kuwa sababu za kumtimua Dogo Janja ni utovu wa nidhamu, unywaji pombe, kutokwenda shule pamoja na uvutaji bangi.

Aliongeza kuwa tayari amempatia nauli ya basi shilingi 90,000/=  kurudi nyumbani kwao jijini Arusha alipotokea. Dogo Janja alitua kwa mbwembwe jijini Dar es Salaam kwa ndege Juni 22 mwaka jana akitokea Arusha na kujiunga na kundi hilo.


Awali alikuwa katika kundi la Tip Top Connection linaloongozwa na Madee lakini ilitokea kutoelewana kati yao na kurudishwa kwao Arusha. Alipopigiwa simu na Mtandao huu, Dongo Janja alidai kuwa bado ni memba hai wa Mtanashati Entertainment.

No comments:

Post a Comment