POOL PARTY

POOL PARTY

Friday, October 11, 2013

MSANII WA BONGO MOVIES CLOUDS AMTUSI MAINDA


Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’, mkali wa sinema za Kibongo amesema kitendo cha mwigizaji Mussa Issa ‘Cloud 112’ kumwambia Ruth Suka ‘Mainda’ kuwa hana mvuto wa kucheza ‘scene’ ya mama wa nyumbani ni sawa na kumtusi kwani siyo sawasawa.
Akipiga stori na paparazi wetu, Dk. Cheni alifafanua kuwa kwa wadhifa alionao Mainda kwenye gemu ni makosa kumwambia hawezi kuigiza nafasi ya umama wakati anaweza sana.

“Cloud ni kama amemtusi Mainda, binafsi siwezi kumuunga mkono, mimi naweza kucheza naye scene ya wanandoa kwa kuwa ni msanii mwenye uwezo mkubwa,” alisema Dk. Cheni.

No comments:

Post a Comment