POOL PARTY

POOL PARTY

Friday, October 11, 2013

MASTAA WETU NA ULIMBUKENI WAO!

Mr Blue.
POPOTE duniani, wasanii na wanamichezo maarufu ni kioo cha jamii. Hutegemewa kwamba kwa ustaa wao, hujikuta wakiwa na mamilioni ya mashabiki, hasa wale wanaofuatilia fani zao.

Hata hivyo, inatokea mara nyingi kwamba siyo watu wote maarufu ni wenye kufahamika kwa sura au majina. Wakati mwingine huwa ni vigumu kwa mfano, mtu asiyependa Bongo Fleva kumfahamu kwa sura msanii chipukizi kama Ommy Dimpoz, licha ya ukweli kwamba kwa sasa jina lake lipo juu.

Hii hutokea na kuna wakati baadhi ya wasanii, hasa wasiojitambua hujikuta wakitoa kauli kama vile; hunijui mimi?!

Majina yao yanasafiri sana, umbali mrefu ambao wakati mwingine ni vigumu kujua kama hata wenyewe wataweza kufika huko. Ni kwa sababu…
Mr Blue.
POPOTE duniani, wasanii na wanamichezo maarufu ni kioo cha jamii. Hutegemewa kwamba kwa ustaa wao, hujikuta wakiwa na mamilioni ya mashabiki, hasa wale wanaofuatilia fani zao.
Hata hivyo, inatokea mara nyingi kwamba siyo watu wote maarufu ni wenye kufahamika kwa sura au majina. Wakati mwingine huwa ni vigumu kwa mfano, mtu asiyependa Bongo Fleva kumfahamu kwa sura msanii chipukizi kama Ommy Dimpoz, licha ya ukweli kwamba kwa sasa jina lake lipo juu.
Hii hutokea na kuna wakati baadhi ya wasanii, hasa wasiojitambua hujikuta wakitoa kauli kama vile; hunijui mimi?!
Majina yao yanasafiri sana, umbali mrefu ambao wakati mwingine ni vigumu kujua kama hata wenyewe wataweza kufika huko. Ni kwa sababu hiyo, popote wanapokuwepo, macho ya watu huvutika nayo, hata kama wengine watajifanya kutowashobokea!
Wapo watu ambao hushoboka sana wanapowaona masupastaa, wawe wa filamu, muziki, soka, kikapu, riadha, mitindo au fani nyingine yoyote. Wakiwaona watu hao wanakosa amani, watataka kupiga nao picha, kusalimiana nao au kwa wenzetu kule majuu, kutoa vitabu vyao ili visainiwe nao!
Lakini pia wapo wengine, na hawa ni wengi zaidi, huwapotezea masupastaa wakiwaona, ingawa wanatambua uwepo wao. Wanawaona lakini kila mtu kimpango wake.
Kuna uzuri mmoja wa kuwa supastaa. Ni rahisi kutambulika na kwa maana hiyo, wakati mwingine ni rahisi kupata huduma kwa upendeleo. Msanii nyota akiwa mgonjwa, anaweza kupatiwa huduma mapema kuliko mtu mwingine, siyo kwa sababu ana fedha, bali wakati mwingine ni kutokana na umaarufu wake tu!
Nitatoa mfano mmoja. Mimi siyo mtu maarufu ila kazi yangu ni maarufu, inajulikana. Siku moja nilikwenda katika ofisi moja ya serikali kwa ajili ya kupatiwa huduma. Ni kwa Mtendaji wa Serikali.
Nilikuta watu wengi kila mtu na mahitaji yake. Umati ule ulinitisha, nikatambua kuwa kama nitafuata foleni, jambo ambalo kwa kweli ndilo hasa nilipaswa kulifanya, nitachelewa, nikaona hebu nijaribu kutumia kazi yangu kama naweza kupata upendeleo.
Nikamfuata mhudumu aliyekuwa akiingia na kutoka kila mara ofisini kwa Mtendaji. Baada ya kumsalimu, kwa upole  nikamwambia; Mimi ni mwandishi wa habari, nina shida ya haraka sana na bosi, naomba umwambie anipe nafasi mara moja.
Alinitazama usoni na kutikisa kichwa, baadaye akaingia ndani, dakika chache hivi akatoka na kunipa ishara ya kuingia!
Heri Sameer, ni msanii wa Bongo Fleva anayejulikana sana kama Mr Blue. Ni kijana mdogo, lakini uwezo wake kimuziki umemfanya aonekane kama vile ni mkubwa kwa umri kuliko Hussein Machozi.
Wiki mbili zilizopita alifanya kituko cha kitoto sana pale Hospitali ya Taifa Muhimbili, kitengo cha mifupa (MOI). Alikwenda na rafiki yake mmoja ambaye alikuwa mgonjwa akihitaji huduma ya kitengo kile. Akiwa amevalia kihuni (kofia ameigeuzia upande) Mr Blue akawa analazimisha mtu wake apatiwe huduma haraka!
Kitendo kile, siyo tu kiliwakera wafanyakazi wa hospitali, bali hata wagonjwa wengine. Kwani yeye ni nani? Matokeo yake, mgonjwa wake akapata wakati mgumu kuhudumiwa, akizungushwa huku na kule.
Binafsi ninaamini hali ile ilitokana na tabia ambayo Mr Blue aliionyesha. Kama kwa mfano, angekuwa mpole, mwenye heshima na aliyetanguliza uungwana, wahudumu na madaktari wangeweza kumsikiliza na kumsaidia vizuri.
Na hili siyo tatizo la Mr Blue peke yake, bali wasanii wengi, wanamichezo na hata watendaji wenye nyadhifa serikalini wanalo. Wanadhani umaarufu au ukubwa wa vyeo vyao wanaweza kufanya lolote mahali popote.
Umaarufu au cheo chako kinaongezeka thamani pale unapojishusha katika eneo lisilohitaji vitu hivyo. Huwezi kuleta mambo ya club hospitalini, polisi, mahakamani, msibani au kwenye shughuli yoyote ya kijamii.

No comments:

Post a Comment