Stori: Mwandishi Wetu
MAMA mzazi wa mkali wa ngoma ya Number One, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, Sanura Kasim ‘Sandra’ ameingilia kati penzi lililofufuka upya
kati ya mwanaye na staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu.
Habari za chini ya kapeti zilitonya kuwa baada ya kuambiwa na
kuoneshwa picha za Diamond akiwa kimahaba na Wema alikuja juu akidai
kuwa hamtaki Wema kwa kuwa anamkubali zaidi Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar
wikiendi iliyopita, bi’mkubwa huyo alisema kuwa kwa sasa hafahamu
chochote kuhusu Diamond kurudiana na Wema zaidi ya kusikia kwa watu na
kuona picha katika mitandao ya kijamii.
“Kuhusu Nasibu (Diamond) kurudiana na Wema, nasikia tu na kuoneshwa
picha namsubiri Nasibu arudi kisha nikae naye ndipo nitatoa tamko,”
alisema mzazi huyo.
Mapaparazi wa Ijumaa Wikienda kadiri walivyozidi kumchimba mama mkwe
huyo wa Wema ni jinsi gani anavyojisikia kuhusu tabia ya kubadilisha
wanawake kama nguo, ikizingatiwa yeye ni mzazi haoni kama mwanaye
anamfedhehesha alisema kuwa hayo ni maisha yake.
“Hayo ni maisha yake na mwenyewe kwa kuwa ameshazoea kuonekana katika
magazeti kila wakati mi niongee nini wakati ndiyo maisha aliyojiwekea,”
alimalizia kusema.
Imeandikwa na Shakoor Jongo na Musa Mateja.
No comments:
Post a Comment