Kampuni
ya GS1 (TZ) National Limited iliyoko Msasani karibu na hospitali ya
CCBRT, leo hii imemkabidhi Rapper Professor Jay Barcode itakayokuwa
ikitumika katika kazi zake za muziki na kumuwezesha
kuuza
kazi zake online na hata kuingia katika chart kubwa duniani kama
Billboard na zinginezo na kumfanya aweze kutanua soko la kazi zake
duniani kote.
GSI
imeanzishwa kwa kusudio kubwa la kuweza kutoa huduma za Barcodes na
teknologia nyingine zinazotewa na taasisi GS1 ulimwenguni, za kuendeleza
biashara kimataifa na kitaifa.
Imedhibitika
kwamba chombo hiki, kabla ya kusajiliwa nchini, wafanyabiashara wengi
wa Tanzania walikuwa wakizifuata huduma za barcodes kutoka nchi za Kenya na Afrika ya Kusini. Chombo hiki kinasimamiwa na Mkutano Mkuu wa mwaka na Bodi ya Wakurugenzi.
No comments:
Post a Comment