POOL PARTY

POOL PARTY

Tuesday, October 29, 2013

RAY C ANARUDI KWA VISHINDO AMPA KIPIGO CHA MWAKA NORA


Na Musa Mateja

KATIKA hali ya kushangaza, siku chache baada ya kuripotiwa kupona na kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ anadaiwa kugeuka mwanamasumbwi na kumpa kipigo mwigizaji Nuru Nassoro ‘Nora’, Ijumaa Wikienda limenyetishiwa.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri wiki iliyopita ndani ya studio moja ya kurekodia muziki iliyopo Kinondoni, Dar ambapo wawili hao walikutana walipokwenda kurekodi ngoma zao.
Ilidaiwa kuwa akiwa studio hapo, Nora alikutana na Ray C ambaye pia alizama mahali hapo bila mawasiliano na prodyuza anayemtengenezea ngoma mpya.


Chanzo hicho kilipasha kuwa baada ya Ray C kuingia studio hapo alimkuta prodyuza huyo akiandaa ngoma ya Nora ambapo alihoji kilichompeleka mwigizaji huyo mahali hapo.

Ilidaiwa kuwa prodyuza huyo ambaye jina halikupatikana alimwambia Ray C kuwa Nora alifika kurekodi wimbo wake.

Ilisemekana kuwa Ray C hakuridhishwa na majibu hayo, akaomba asikilizishwe ngoma hiyo ya Nora lakini baada ya kusikiliza ilidaiwa kwamba Ray C aliiponda mbele ya Nora, jambo ambalo mwigizaji huyo hakufurahishwa nalo.
Ilidaiwa kuwa Nora alipandwa hasira na kujikuta akimjibu mbovu Ray C.

Habari ziliendelea kutiririka kuwa siku hiyo walimalizana kwa kusonyana na siku iliyofuta walikutana tena studio hapo ambapo Ray C alidaiwa kutinga akiwa ‘masanga’.
Ilisemekana kuwa alipomuona Nora alianza kumpa vijembe, jambo lililosababisha Nora kushikwa hasira ndipo wakavaana na kuzichapa.

Hata hivyo, ilidaiwa kuwa Ray C ndiye aliyeibuka bingwa wa ndondi hizo kwa kumtwanga Nora hadi kumvimbisha jicho kabla ya maprodyuza na watu wengine kufanya kazi ya ziada kuwaamulia.
Ilisemekana kuwa baadaye Ray C alitolewa nje ndipo akahamishia hasira kwenye gari la Nora aina ya Toyota Vitz kisha akalivunja kioo na kutambaa zake.

Baada ya kupenyezewa ‘niuz’ hizo gazeti hili lilimtafuta Nora ambaye alikiri kutokea kwa sekeseke hilo huku akibainisha namna alivyoumizwa jicho lake na kuvunjiwa kioo cha pembeni cha gari lake.
Aliongeza kuwa siku hiyo alipoteza pochi wakati wa ugovi huo.

“Ray C alinikuta studio nikifanya wimbo, kilichonishangaza baada ya kuniona tu alibadilika ghafla.
“Nilijua angenishauri kwa kuwa ndiyo ninaanza gemu kumbe mwenzangu alifikiria vingine,” alisema Nora na kuongeza:
“Mbali na kuniumiza jicho lakini alinifanyia mambo ya ajabu sana, kama kusingekuwa na watu wa kutuamulia basi chochote kingetokea.

“Sikwenda kuripoti polisi. Niliamua kusamehe kwa sababu kuna watu walinisihi niachane naye kwa sababu bado kuna mambo yanamwendesha. 

Kwa upande wake Ray C alitafutwa kwa kila njia kupitia simu ya mkononi na kumvizia studio lakini hakupatikana hivyo juhudi za kumpata zinaendelea.

BABA DIAMOND ACHEKELEA MWANAYE KUMRUDIA WEMA


Na Gadness Mallya

Baba mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa amejikuta akiangua kicheko ‘hevi’ baada ya kusikia taarifa za mwanaye kurudiana na aliyekuwa zilipendwa wake, Wema Isaac Sepetu.

Akizungumza na mwanahabari wetu juzikati, Baba Diamond alisema alifurahishwa mno na hatua ya mwanaye kurudiana na Wema kwani ndiye mwanamke anayejielewa na ana nyota kali tofauti na warembo wengine aliowahi kuwa nao.

“Wema ni mwanamke mwenye nyota kali sana na anapendwa na wengi. Siyo kama hao akina sijui Penny (Penniel Mungilwa).


“Hana majivuno hata mimi nilisema mwanzoni walipoachana kuwa Diamond alipoteza bahati lakini sasa naamini atafika mbali zaidi kwani kama siyo kuachana kwao, Diamond angekuwa mbali,” alisema.


Hata hivyo, alimtaka Diamond kutulia na Wema kwani ndiye mwanamke sahihi kwake na aepuke kutangatanga kwani atashindwa kufanya mambo ya maana yatakayomuwezesha kuwa juu zaidi ya hapo alipo kwa sasa.


Hivi karibuni Diamond alithibitisha kurudiana na Wema wakiwa China lakini alipotua Bongo akaendelea na uhusiano wake na Penny hivyo kuwaacha mashabiki wake njiapanda

SINTAH AMCHANA AUNTY LULU LIVE KWA KUGAWA URODA BURE KWA MIDUME.


Katika mahojiano yake na gazeti moja hapa jijini nimesikia aunt lulu akisema wanaume wamemla sana uroda bure kwa miaka mingi sana bila faida, ila kwa sasa harudii kosa hilo ni mwendo wa faranga kwa kwenda mbele, sincerely kwa hizo pics hapo juu nani anaweza akawa na mwanamke kama huyu and shower her dollazzzz?? men also haaaaa as they say one man's meat is another man's poison.

 kwahio tusiliongelee sana ila wakati mwingine maneno tunayaongea ktk media yanafanya wasanii waonekane kituko katika jamii kabisa na akili zako na unajitambua wewe ni msanii  unaweza ukaongea pumbaless kama hii na watu wakasoma na kukuelewa ??

WANAUME WAMENILA URODA BURE MIAKA MINGI SANA BILA FAIDA SASA HIVI SIRUDII KOSA NG'OO: ANT LULU!

hiki ni nini wajameni? nikisema mtasema Sintah anaongea?? niko hapa kwaajili ya kurekebisha watu na jamii inachukulia wasanii kama kioo chao, sasa kwa matendo haya ya lulu na alivyoongea wengine tunaonekana vipi,

ni wakati umefika sasa tujue kuna wasanii na wanaotafuta umaarufu ili ya kwao yawaendee eg kupata mabwana na wanawake 

yaani nimekereka sana na hii kauli ya Aunt Lulu so sasa hivi anauza rasmi na ameamua kujitangaza kama tunavyojua biashara ni matangazo ?? God  forbid.


i do the seeking n u do the judging...

NEY WA MITEGO AKAIDI AMRI YA BASATA YA KUTOKUVAA MLEGEZO..AWAONYESHA USO WA MBUZI FIESTA


Msanii wa Hip pop Ney wa mitego 'TRUE BOY' Amewaonyesha uso wa mbuzi Basata ambao awali walimwonya kutokana na tabia yake ya kuvaa mlegezo "KATA K" akiwa jukwaani kwa madai ya kuidhalilisha sanaa hiyo..

Katika hali ya kushangaza kabisa Msanii huyo ameonekana kupuuzia agizo hilo la basata na kendelea kuvaa mlegezo wakati akilishambulia Jukwaa huku akishangiliwa na mashabiki lukuki wa Bongo Fleva .


Tukio hilo lilitokea jana wakati wa Show ya FIESTA DAY 2 iliyofanyika kwenye viwanja vya Leaderz Club alipokuwa akiwapagawisha wapenzi wake na kibao chake cha "MUZIKI GANI" Akiwa sambamba na Msanii mwenzake Diamond Platinumz.

Sasa wapenzi wa Bongo fleva wanasubiri Rungu la Basata liweze kufanya kazi yake huku wengi wakionekana kumtetea kwa kudai kuwa kila mtu ana aina ya maisha yake 'Life Style'

BEN POL AIMISS M-LAB STUDIO ATAJA FAIDA NA HASARA ZA KUONDOKA LABEL HIYO


Ben Pol amezielezea faida na hasara za kuondoka kwenye label iliyomtambulisha, MLab huku akisema kwa sasa hana uhuru wa kurekodi nyimbo nyingi kwa wiki kama alivyokuwa kwenye label hiyo.


“Sasa hivi sina freedom ya kurekodi nyimbo 3 kwa wiki kwasababu itabidi upige simu, ufanye booking hata two weeks before, uende utengeneze beat, unaweza ukarekodi wimbo mmoja miezi miwili au mwezi mmoja. Lakini kipindi nipo MLab unarekodi nyimbo nne, hizi Maneno, Nikikupata, Maumivu, ndani ya wiki moja nimerekodi nyimbo tatu kwasababu una all access ya studio, unaweza ukarekodi hata nyimbo mbili siku moja, yaani hiyo access ndio nimeimiss sasa hivi,” alisema Ben Pol.


Akizungumzia faida za kuondoka MLab, Ben Pol amesema kwa sasa ana meneja wake binafsi ambaye ni kaka yake na hivyo mazingira ya kufanya kazi ni rahisi tofauti na kuwa chini ya uongozi wa label.


“Kunakuwa na mlolongo mkubwa hata kama ikitokea kazi kuona maslahi yake ni adimu sana tofauti na ukiwa unafanya mwenyewe.”


AIBU:HUU NDIO UCHAFU UNAOFANYWA KWENYE PARTY ZA BIKINI CAR WASH


 




Asikwambie mtu hivi ndio party za kuosha magari huku wanawake wakiwa na bikini zinavyofanyika huko Uganda...kwa kizungu wanaziita Bikin Car Wash ...Hapa mambo yanayofanyika huwa ni aibu watoto kaaa mbali sanaaaa....kama unavyojionea kwenye picha ...Mdakuz unaonaje hapo? Bongo Je zipo hizo ?ama ndio zile Baikoko?
Udaku Specially Blog

Saturday, October 26, 2013

DOGO JANJA NA OSTAZ JUMA NAMUSOMA WANATUCHEZEA MCHEZO WA DANGANYA TOTO...


Story ya Dogo Janja kutimuliwa kwenye kampuni ‘inayolegalega’ ya Watanashati Entertainment jana ilivitawala vyombo vingi vya habari nchini. Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Ostaz Juma ambaye hivi karibuni naye alijaribu bahati kwenye muziki kwa kurekodi wimbo uliopotea kwa wiki chache tu, alisikika akihojiwa kwenye vituo vingi vya radio akielezea hatua hiyo.


Kuanzia kwenye U Heard ya XXL, Clouds FM, hadi kwenye Showtime ya RFA, Ostaz alisikika akiongea kwa sauti ya msisitizo, kuhusu uamuzi wake wa kumuondoa rapper huyo wa Arusha kundini kwa kile alichodai kuwa amekuwa mtovu wa nidhamu. Wasiwasi wangu juu ya hatua hiyo ilianza mapema tu jana baada ya maelezo ya Ostaz Juma, Dogo Janja na baba yake rapper huyo kukinzana.

Ostaz alisisitiza kuwa amemfukuza msanii huyo kwasababu kadhaa, kubwa likiwa ni suala la nidhamu. Dogo Janja alidai kuwa, hajafukuzwa, bali kajiondoa mwenyewe. Baba yake Dogo Janja alisema hakuwa na taarifa za kufukuzwa kwa mwanae kutoka kwenye kampuni hiyo licha ya Ostaz kuiambia Bongo5 kuwa alishampigia simu kumwelezea uamuzi wake. Baba huyo huyo pia jana aliiambia RFA kuwa waliyaongea jana na wakayamaliza.

Hata kabla ya siku moja haijaisha, leo Ostaz Juma anasema yamekwisha, na amemrejesha kundini.

“Nimeamua kumrudisha, kwa sababu yale mambo yaliyopelekea mpaka mimi kutoa maamuzi yale niliyotoa jana, yaani kawa kama mtu mzima mwenye akili timamu, na mtu yeyote anayelifikiria na akaona kwamba hili ni kosa akasema kwamba ntajirudi, ni kumpa nafasi ya kumsikiliza,” Ostaz ameiambia tovuti ya Times FM.

“Kwa hiyo jana tulikaa kama kikao cha familia nyumbani kwangu, tukazungumza na ni kweli ameona kwamba ni bora aache baadhi ya mambo ambayo hayakuwa mazuri kwenye jamii, na mimi nachokitaka Dogo Janja awe mtu bora, awe mzuri katika jamii. Na yeye ameniahidi kwamba, atawahakikishia watanzania kwamba atakuwa Dogo Janja ambae watanzania wanamtaka wao.”

Naye Dogo Janja ameiambia tovuti hiyo, “Mi niko mtanashati, kwa sababu ni mambo ya kifamilia na tumeshakuwa familia moja, na mimi naona kuhamahama sio swala zuri, na kama nilikuwa na malengo ya kufanya kazi nzuri, ni bora niendelee kupalilia tu hapahapa. Yamekwisha isha kwa ufupi. Kwa namna moja ama nyingine ni ile chuki, marafiki ambao wamenizunguka, ni watu ambao ni soo, sio watu wazuri. Sasa hivi rafiki yangu hela tu.”

Maelezo hayo Ostaz Juma na kauli pamoja na msimamo aliokuwa nao jana na hiki anachokisema Dogo Janja ni ngumu kushawishika kuwa hiki kinachoendelea ni halisi ama ni njia nyingine ya kuendeleza ugonjwa wa kutafuta ‘kiki’ uliopata umaarufu kwenye kiwanda cha muziki cha hapa nyumbani.

Na pengine labda kumshauri tu Ostaz, ni kuwa asipendelee sana kuconclude mambo na kuongea kwa uhakika kwa vyombo vya habari pale ambapo migongano midogo inapotokea ambayo ingeweza kumalizika bila hata nyumba ya jirani kufahamu. Kulikuwa hakuna haja ya jana kutoa kauli ya kumfukuza na tena kwa msisitizo kama huo na kisha leo kuamka na uamuzi mwingine.

Hii inaifanya kampuni ya Mtanashati ionekane ipo kienyeji mno na maamuzi mengine yanafanywa kitoto. Kama ingekuwa ni kampuni iliyodhamiria kufanya kazi kikampuni, basi isingekuwa rahisi kutimua watu kienyeji hivyo na hadi leo kuifanya ibakize wasanii wawili tu, ambao nao hawamake noise yoyote. Pengine ndio maana, Ostaz ameamua kuingia front pia na kufanya muziki. Muziki ambao kwa wengi unaonekana kama utani tu na kejeli kubwa kwa fani hiyo.


Hata hivyo hiyo ni ishara kuwa fungate la Dogo Janja na Mtanashati lina mushkeli mkubwa na nachelea kusema, siku si nyingi watarudi tena hewani wakiongea kile kile kama kilichofanyika jana na kisha baada ya siku chache kurudi tena na kusema wameyamaliza.

NEY WA MITEGO AWEKWA SERO KWA KOSA LA KUTUMIA SARE ZA POLISI


Rapper Ney Wa Mitego ameniambia kuwa hii picha hapo juu tukio hilo limetokea Jana wakati wana shoot video ya wimbo wake Unaofanya vizuri kwa sasa kwenye radio stations ' Salam Zao'.

Ney Wa Mitego Amesema ' Nikweli nilituwa sero jana baada ya raia wasio julikana kuleta fujo eneo la kazi yangu  kwasababu kulikuwa na waigizaji waliokuwa na sare za polisi. Watu hao sijuani nao na walijitambulisha kama askari na kutaka kujua kwanini natumia sare za polisi kwenye video yangu bila kibali. hicho ndio kitu kilichopelekea nikapelekwa polisi. 

Mitego ameendelea kusema kuwa baada ya kukaa sero kwa dakika kama 15 mkuu wa kituo alikuja na kusikiliza tatizo hilo na ndio aliachiwa huru baada ya kutoa maelezo kuhusu tukio hilo na sare hizo kuoneknaA uraiani. 


Ney aliwekwa sero Kwenye kituo cha polisi Urafiki kilichopo Manzese na wiki ijayo video hii itaonekana kwenye vituo vya televison Tanzania


MWANAMUZIKI WA INJILI WA NIGERIA APIGA PICHA ZA UCHI NA KUSAMBAA MTANDAONI...CHEKI HAPA


Mwimbaji wa nyimbo za injili toka nchini Nigeria  ajulikanaye  kwa  jina  la  Maheeda  amejikuta  akitengwa  na  kanisa  baada  ya  picha  zake  za  uchi  kuvuja….



Taarifa  zinadai  kwamba kabla  ya  kuanza  kuimba  nyimbo  za  dini, mrembo  huyo  alikuwa  akijihusisha  na  mziki  wa  kidunia ambao  kwa  tanzania  unajulikana  kwa  jina  la  Bongo Fleva

DIAMOND ATOA SIRI 5 ZA KUMRUDIA WEMA


Stori: Shakoor Jongo na Musa Mateja


MKALI wa songi linalotamba runingani na redioni ndani na nje ya Bongo la Number One, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ amefunguka na kuanika siri tano za kurudiana na Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.

Wiki mbili zilizopita, wakiwa Hong Kong, China, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii viliripoti kurudiana kwa Diamond na Wema waliomwagana takriban mwaka mmoja uliopita ambapo staa huyo wa Bongo Fleva aliibuka na kukanusha vikali akidai kuwa picha zinazomwonesha yuko na Wema ni za Filamu ya Temptations.

Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa dakika ishirini katika mahojiano maalum jijini Dar mara tu baada ya kutua kutoka China Jumatano iliyopita, Diamond alikiri kufaidi penzi la Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006.

Diamond alisema kuwa, Wema ndiye aliyetangulia kwenda China ambapo yeye aliungana naye siku kadhaa baadaye akitokea kwenye shoo nchini Malaysia.

SIRI YA KWANZA
Akianika siri za kujikuta mikononi mwa mwigizaji huyo mwenye mashabiki wengi zaidi katika tasnia ya filamu za Kibongo, Diamond alisema kwanza ni ukarimu aliopewa na mrembo huyo.

Alisema kuwa alipotua Hong Kong alishangaa kukutana na mapokezi ya Wema kwenye uwanja wa ndege jambo ambalo hakulitegemea.

“Alinionesha ukarimu wa hali ya juu mno. Wakati tulipokuwa hapa Bongo tulikuwa hatusalimiani.
“Kuna vitu vingi vya ajabu vilitokea huko nyuma kati yangu na Wema. Sikufikiria wala kuwaza kama anaweza akawa mkarimu kwangu kiasi kile.

Akaongeza: “Kwa mazingira yalivyokuwa, kwa namna yoyote lazima mwanaume aliyekamilika arudishe moyo nyuma na kuacha mambo mengine yaendelee.


“Kiukweli nisema tu kuwa hata tungekutana Morogoro au Dodoma kwa ukarimu ule mwisho wa siku tungerudisha uhusiano wetu.”

SIRI YA PILI
Diamond alisema baada ya mapokezi ya nguvu, Wema alimpeleka kwenye hoteli ya nyota tano (five stars) ambapo huko alipatiwa huduma ‘klasiki’ na kujiona kama yupo kwa mama Nasibu vile.

SIRI YA TATU
Alifunguka kuwa kitendo cha Wema kuwa mwenyeji wake China ambako alikuwa mgeni hadi akapazoea nacho ni siri nyingine iliyochangia wao ‘kukumbushiana’.

SIRI YA NNE
Alisema kuwa mwanadada huyo alimuonesha mapenzi mazito (yaani kutekwa kimapenzi) hivyo haikuwa rahisi kumchomolea kwani waliishi kama ndiyo penzi jipya linachipuka, akajikuta akiogelea naye. 

SIRI YA TANO
Diamond alisema kuwa bado ana ndoto ya kupata mtoto kupitia kwa Wema ambaye anajua kuwa alishamwambia lengo lake juu ya kupata naye uzao hivyo katika nyakati za kukutana kwao anaamini ndoto itatimia.

HAKUNA CHA FILAMU
Alipoulizwa juu ya madai kuwa walikuwa wakirekodi filamu, Diamond alifunguka kuwa hakuna cha filamu wala sinema na kama kuna mtu anasubiri filamu atakaa sana.

“Naomba nikiri kuwa kweli zile picha hazikuwa za filamu wala nini bali ndivyo hali halisi ilivyokuwa kati yangu na Wema kule China.
“Pia naomba niseme kuwa uhusiano wetu wa kimapenzi uliishia China na sasa hivi tumebaki kama kaka na dada na ni ruksa kila mtu kumtumia mwenzie katika kazi mbalimbali kama ataona kuna ulazima wa kufanyika hivyo,” alisema Diamond.
Hii ni mara ya kwanza kwa Diamond au Sukari ya Warembo kukiri kuwa kweli alirudisha penzi lake kwa Wema walipokuwa nchini humo wakijiachia.

PENNY HANA CHAKE?
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Diamond, ukifuatisha simulizi hiyo ya mapenzi kati ya msanii huyo na Wema, ni dhahiri kuwa mpenzi wa sasa wa jamaa huyo, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ hana chake kufuatia usaliti huo.


Hata hivyo, jitihada za kumtafuta Penny ziligonga mwamba kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa lakini juzi wanahabari wetu walipofika nyumbani kwa Diamond, Sinza-Mori, Dar waliambiwa mrembo huyo alilala hapo na kuondoka asubuhi.

AMANDA:SIWEZI KURUDIA MATAPISHI HATA SIKU MOJA


Stori: Gladness Mallya

STAA wa sinema za Kibongo, Tamrina Poshi  ‘Amanda’ amefunguka kuwa hawezi kurudia matapishi yake kwa kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake, Joseph Rashau ‘Bwana Misosi’.

Akichonga na paparazi wetu muda mchache baada ya wadau kibao kumtaka mwanadada huyo arudiane na mpenzi wake huyo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, Amanda alisema tayari ameshapenda kwingine hivyo hapendi kumzungumzia mtu aliyeachana naye pia hana tabia ya kurudia matapishi yake.


“Siwezi kurudiana na Misosi kwani nikishaachana na mtu basi ninamtoa moyoni mpaka mdomoni nikiwa na maana sina muda wa kukaa na kumzungumzia ndiyo maana hata wadau waliokuwa wakinitaka nirudiane naye sijawajibu chochote,”alisema Amanda.

PICHA YA JOKATE YAMPONZA LULU


Stori: Mwandishi Wetu

ELIZABETH Michael ‘Lulu’ amejikuta akiambulia maneno makali kutoka kwa mashabiki baada ya kuposti picha ya Jokate na kumsifia katika mtandao wa Instagram.

Lulu aliiposti picha hiyo kwa nia njema kabisa ambapo kuonesha kuwa anamkubali Kidoti, alimwagia sifa kuwa ana uzuri wa ziada ndipo wafuasi wa mtandao huo walipotema mbovumbovu.


“Anampiga vijembe Wema huyu, mtoto mswazi sana huyu…mnafiki huyu mimi nishamjua hanipi shida siku hizi,” walichangia wadau tofauti mtandaoni.

SHEDDY CLEVER:PRODUCER WA MY NUMBER ONE ALIYE VICHOCHORONI USWAZINI


Ukiingia ndani ya studio ya Burn Records iliyopo Tabata, jijini Dar es Salaam, huwezi kuamini kama ndiyo sehemu ‘zinakopikwa’ kazi za baadhi ya wasanii zinazowafanya kuwa maarufu na kuwaingizia kipato, kupitia shoo na mialiko ya ndani na nje ya nchi.

Studio hii iliyopo maeneo ya ‘uswahili’ imezingirwa na nyumba nyingi kiasi cha kushindwa kuijua njia kwa uharaka zaidi pale mtu anapotaka kufika kwa prodyuza huyo. Studio hii ni ndogo yenye vifaa vichache tu vya kimuziki lakini yenye prodyuza makini na mwenye kipaji.


Shadrack Willced Mongi maarufu ‘Sheddy Clever’ ndiye prodyuza wa studio hii iliyotengeneza wimbo wa ‘My Number One’ unaomilikiwa na mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’, wimbo uliofanya vizuri katika levo za kimataifa.


Hata hivyo sehemu ya mahojiano na mwandishi wa Starehe ni kama ifuatavyo;


Swali: Mbona Studio yako ipo uchochoroni hivi?


Jibu: Unasema uchochoroni!  Wasanii wengi wamekuja hapa na wanatumia muda mwingi kuwepo ndani ya studio hii huku wakitumia vyakula vya hukuhuku kwetu uswahili, si jambo la ajabu. Lakini ni mazoea tu kwetu tunaona sawa na kwa upande wangu inanipa hamasa kwani najisikia huru kufanya kazi nikiwa maeneo haya.


Swali: Ndiyo kusema Diamond alikuja kurekodi kwenye studio hii?


Jibu: Ndiyo alikuja kurekodi katika studio hii na alikuwa akikaa hapa kutwa nzima. Yule jamaa anafanya kazi sijawahi ona kutoka kwa wasanii wengine akija hapa anatumia muda mwingi kujenga mashairi, hata hivyo anatumia akili kubwa sana katika kufanya kazi si sawa na vile watu wanamwona. Korasi ya wimbo wa My Number One tulitumia zaidi ya saa 12 kuitengeneza na saa nyingine 12 kuirekebisha, yupo makini sana. Ilichukua miezi sita kukamilika.


Swali: Ilikuwaje akapajua hapa?


Jibu: Diamond alinitafuta yeye mwenyewe, ilikuwa saa mbili asubuhi akanipigia na kunifahamisha jina lake akasema anakuja, kwa kuwa namba niliyokuwa nayo alishaacha kuitumia nilidhani si yeye lakini baada ya muda nikashangaa amefika. Alinitaka nimsikilizishe midundo nami nilifanya hivyo hatimaye akapenda mmoja wapo, basi tulipeana mikakati kazi ikafanyika.


Swali: Kazi uliyoifanya imeweza kumwingizia kitita kikubwa cha pesa mwanamuziki huyo vipi kwa upande wako inakuneemesha vipi?



Jibu: Hapana nilimfanyia kazi akanilipa ujira wangu mzuri tu, hivyo huko mbele ni kazi yake. Lakini katika upande wa hatimiliki hivi sasa tupo mbioni kuhakikisha chama chetu cha maprodyuza  cha Tanzania TSPA kinasajiliwa ili kuweza kutetea kazi zetu na hatimiliki.

Swali: Umechukua hatua gani kwa prodyuza aliyechukua biti ya wimbo wako na kuichakachua kwa kutengeneza kazi feki?


Jibu: Huyo mtu namtafuta sana tena sana, sijapata tu mahala anapofanyia kazi.


Swali: Tuambie uhalisia wa kazi zako ulianzia wapi?


Jibu: Nilianza mwaka 2005, nikiwa mkoani Tabora katika studio za rafiki zangu. Lakini studio yangu ya kwanza ilikuwa ni pale Student Center kulikuwa na mzungu mmoja aliitwa Father Clombi ndiye aliyekuwa mmiliki. Nikiwa huko nimepata kutengeneza vibao kadhaa vilivyofanya vizuri katika redio mbalimbali mkoani hapo. Niliamua kuondoka huko mwaka 2008 wakati huo nilikuwa nimeshapata jina kidogo. Nilifika jijini na kuanzisha studio pale Liwiti. Mtu aliyenisaidia sana ni Mbishi Real na kunipa uzoefu mkubwa katika kazi hii baadaye nikahama na kufika hapa Da West.


Swali: Kazi yako ya kwanza kabisa kuitoa na ikafanya vizuri ilikuwa ipi?


Jibu: Nivute Kwako wa Dayna aliyomshirikisha Barnabas. Wimbo huu ulinitambulisha katika ramani ya muziki wa kizazi kipya, tangu hapo walianza kumiminika wasanii maarufu wakitaka niwatengenezee kazi.


Swali: Ni kazi zipi maarufu ulishawahi kuzifanya?


Jibu: My Number One wa Diamond, Marry Me wa Rich Mavoko, Zilipendwa wa Matonya, Yatakwisha wa Ben Pol ft Linah, Mtoto Amekuwa wa Pasha, Swaga wa PNC na Ney wa Mitego na nyingine nyingi tu.


Swali: Una mikakati ya kuhama eneo hili na vipi kuhusu vifaa vya kisasa?


Jibu: Ninamalizia kujenga nyumba yangu huko Kinyerezi, hivyo nikimaliza tu studio yangu itakuwa nyumbani kwangu na huko ndiko nitafunga vifaa vya kisasa tofauti na hapa.


Swali: Unafanya shughuli gani tofauti na kazi yako ya utayarishaji wa muziki? Umepata faida gani kutokana na kazi yako?



Jibu: Mimi ni  mjasiriamali nina duka linalouza CD, nina banda linaloendesha shughuli za michezo ya tv kwa watoto, bodaboda na vinginevyo. Nimeweza kujenga nyumba yangu mwenyewe, namiliki gari langu binafsi, nimekuwa na marafiki wengi na kujuana na watu mashuhuri kupitia kazi yangu.

-Mwananchi

PROFESA JAY AKANUSHA TAARIFA ZA KWAMBA ATATUMBUIZA KESHO FIESTA



Kupitia  account  yake  ya  facebook, Profesa  Jay amewataka  mashabiki  wake  watambue  kuwa  kuna  wabaya  wake  wali hack  account  zake  za  twitter  na  facebook  na  kutangaza  kwamba  kesho  atatumbuiza  katika  tamasha  la  Serengeti  Fiesta...


Taarifa  sahihi  ni  kwamba, yeye  hatahudhuria  tamasha  hilo  na  waliotangaza  taarifa  hizo  ni  adui wa  mafanikio  yake  ambao  walitumwa  na  vibosi  wao  ili  wamchafue.

FLORA LYIMO "NIMEFUNGA TO BLOG AND FACEBOOK FOR ONE WEEK FROM TODAY MONDAY 21/10/2013 ''KWA AJILI YA KWENDA KUSALI ROZARI "


BY:FLORA LYIMO~ BREAKING NEWS! TO ALL MY FANS AND MY READERS ' DUE TO OCTOBER MWEZI WA ROZARI 'NIMEFUNGA TO BLOG AND FACEBOOK FOR ONE WEEK FROM TODAY MONDAY 21/10/2013 ''KWA AJILI YA KWENDA KUSALI ROZARI 


HAPA NAIMBAJE 'JAMANI NAJISIKIA KAMA NIPO KULE MOSHI KILEMA KANISANI'' NAIMBAAAA ,NAFURAHIIIIII,'NA TUSALI ROZARI NA TUIMBENI PAMOJA  MY DEARS' WAPENZI(FANS) WANGU PAMOJA NA WANAOITEMBELEA BLOG HII'' AGAIN POLENI KWA KUTOKUKUWEPO KUWARUSHIENI MAPOCHOPOCHO YA UKWEE'' ONLY SIPO KWA MUDA WA WIKI MOJA TU'NAKWENDA KUSALI ROZARI KUANZIA JUMATATU 21/10/2013 MPAKA JUMATATU IJAYO 28/10/2013KAMA MNAVYOJUA HUU NI MWEZI WA BIKIRA MARIA KWETU SISI WA KATOLIKI'' NA HASA WALE WANAO MPENDA MAMA YETU BIKIRA MARIA  NA KUMUAMINI NA VILE VILE KUMTEGEMEA KAMA MAMA YETU NA MAMA WA ULIMWENGU MZIMA KAMA MIMI HAPA 'NI MWEZI MZURI SANA WAKUKAA NA KUSALI NA KUONGEA NA MAMA YETU KIUNDANI NA KIUPOLE ZAIDI ''I LOVE HER SO MUCH '' CHAMESHA MAE KANYI''

Friday, October 25, 2013

KAMA WEWE NI MSANII CHIPUKIZI WA BONGO MOVIES BASI HII KAULI YA NISHA INAKUHUSU


Muigizaji wa filamu mwenye jina kubwa ndani ya bongomovies  Salma Jabu Nisha amemwaga chozi la huruma kutokana na jinsi wasanii wachanga wa filamu wanavyohangaika ili watoke huku wakipuuzwa na baadhi ya wasanii wenye majina makubwa. Akizungumza na tovuti ya  Swahiliworld planet ,Nisha ameahidi kuendelea kuwasaidia wasanii hao kwa kufanya usaili mara kwa mara pindi anapokaribia kutaka kutengeneza filamu mpya kupitia kampuni yake ya Nisha's Film Production ambayo tayari imeanza kufanya kazi na wasanii wachanga katika filamu yake mpya ambayo ilimalizika shooting hivi karibuni.

 Nisha alisema kuwa hata yeye alipitia msoto kama huo kabla ya kuto hivyo anajisikia huruma na industry hii ili izidi kukua ni lazima mastaa wa sasa wawaandae wasanii chipukizi ambao ndiyo watakaotingisha siku za mbele na kuzipeleka filamu za Tanzania katika level za kimataifa. Hii ina maana kuwa baada ya filamu hii mpya ya Nisha kuingia sokoni hivi karibuni atafanya usaili mwingine wa wasanii wachanga amabo atafanya filamun mpya nao. "nawapenda sana wasanii chipukizi nikiwaona huwa nasikia uchungu mpaka machozi hunitoka kwa wanavyohangaika kila siku kutafuta sanaa naahidi kuwasaidia" alisema Nisha


Hongera sana Nisha kwa hilo. Kazi kwenu wenye vipaji kuanza kumsaka Nisha alipo.
-Bongomovies.com

ANNA MAKINDA"WABUNGE WASTAAFU WANA HALI NGUMU-HUJA OFISINI KUOMBA OMBA


Akiongea na Spika wa Bunge la Uswisi, Maya Graf, Spika Anne Makinda amenukuliwa akisema kuwa Wabunge wengi Wastaafu wana hali ngumu kiuchumi pindi wanapomaliza muda wao.
Yumkini Wabunge wetu wastaafu huwa na hali ngumu kiuchumi baada ya kustaafu, lakini, tafsiri zaweza kuwa nyingi. Si kwamba Waheshimiwa hao hawakuwa wabunifu walipokuwa Mjengoni. Yawezekana baadhi yao wanahangaika sasa kwa vile walikuwa waadilifu sana. Hawakuiba senti za Wananchi.
Kwa kuwasengenya hata waliokuwa waadilifu yaweza walio Mjengoni sasa na wanaojitahidi kuwa waadilifu nao kuanza kukata tamaa. kwamba, hakutakuwa na tuzo ya wao kuwa waadilifu, bali masimango.(P.T)
Kwamba wameitumikia nchi bila kufanya ujanjaujanja na hivyo mitaani kuonekana wako hoi. Maana, kwa mshahara wa kawaida wa Mbunge, kwa kweli kuwa na magari na nyumba za kifahari ni jambo gumu.
Tukumbuke Wabunge hao wana familia zao za watoto wa kuwasomesha , wana pia ndugu na jamaa wanaowategemea. Achilia mbali wananchi wa majimbo yao wenye kuwataka misaada kila kukicha.
Hapa Mbunge mwadilifu kwa kiwango kikubwa hawezi kumaliza kipindi chake akiwa tajiri.
Haya, kwa masengenyo haya, Spika Makinda hatawaona tena Wabunge wenzake Wastaafu wakifika kwa wingi ofisini kwake. Maana, hata wale waliokuwa wakitaka kupita tu kumsabahi Spika, na hata kumpa ushauri wa hapa na pale, nao huenda wataogopa kuonekana ni 'omba omba'.
Na kwa Wabunge hao wastaafu nitawakumbusha wimbo wa kwenye Lizombe, ngoma ya Wangoni, na wanaweza kuingiza maneno yao wakipenda, usikike hivi; ...
" Tulipokuwa Mjengoni wee, Spika hakutusemaa..
Tumeondoka kidogooo, nyuma anatusengenyaa... Weee!"
Naam, dhiki haina mwenyewe!
Maggid.

Dar es Salaam.


AMMY NANDO APEWA NAFASI YA KIPEKEE KUSHIRIKI TENA BIG BROTHER AFRICA YA MWAKANI 2014


After being disqualified from the recently concluded BBA The Chase show, Nando Khan (also known as Ammy Nando) has gotten himself another chance at the game!

Word reaching us right now is that, he will be representing Tanzania in the 9th season of the Big Brother Africa show, tagged BBA Stars.

Reliable sources also reveal that he has accepted the offer and will be back in the house come next year.

The Tanzania rep got disqualified shortly after his fight with Ghana's Elikem.

Nando is rumored to have apologized to Elikem during the finale party.


This is a developing story, please check back for updates.

STAGE YA KISASA YA SERENGETI FIESTA 2013 IKIWA BADO KWENYE MATENGENEZO


 Jukwaa la kisasa kwa ajili ya Fiesta Serengeti Fiesta 2013 likiwa kwenye matengenezo ikiwa leo ni siku ya 9 likiwa kwenye matengezo ni jukwaa la kisasa lenye mashine za kisasa ambazo zitakuwa zikifanya kazi mbalimbali. Katika viwanja vya leaders club kutakuwa na screen kubwa ambazo zitakuwa zikionyesha matukio mbalimbali yanayoendelea, Serengeti Fiesta 2013 ni JUmamosi 26 Oktoba 2013 huku zaidi ya wasanii 300 wakitarajwa kutoa burudani hawa wakiwa ni wasanii wakali kutoka Tanzania na wasanii wa kimataifa ni wanne ambao ni mkali Mohombi, Iyanya,Davido na Alaine - Serengeti Fiesta 2013 Noma Saana Twenzetu!!


"KIOO KILINIFANYA NIMVULIE NGUO SAJUKI KWA MARA YA KWANZA" WASTARA


Wastara   amefichua  siri kwamba kioo ndicho kilisababisha aanzishe uhusiano wa mapenzi na marehemu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki Januari 2, mwaka huu.

Wastara aliweka bayana kuwa marehemu Sajuki ambaye alikuwa mumewe, hakuwahi kumtongoza lakini kioo ndiyo kilikuwa chanzo kilichosababisha wajikute wameingia dhambini kwa mara ya kwanza.


Akizungumza na gpl, Wastara alisema kuwa siku hiyo walikuwa wakifanya mazoezi ya filamu moja (hakutaja jina) nyumbani kwake na Sajuki alikuwa muongozaji wa sinema hiyo.

“Ilikuwa ni usiku wa manane tukiwa nyumbani kwangu tukifanya mazoezi ya filamu moja, sasa ilikuwa ni scene ya mapenzi tukawa mbele ya kioo huku tumekumbatiana.




“Tukaendelea hivyoo, mmh! Sasa tulivyokitazama, tukahisi tunaendana. Tukaendelea kujifanyia tathmini na ghafla tukajikuta tunafanya kweli, kioo kilisababisha tukajikuta tunafanya mapenzi,” alisema Wastara kwa uso wa aibu

PHOTOS:HUDDAH MONROE WITH JUST A ROBE AND NOTHING ELSE


Huddah Monroe is a lass that loves to court controversy. She loves to smash societal etiquete on the floor and trounce on it. And today she has something for you that should tease and tantalize you……

 She shared these new photos that show how she would look the morning after you bed her and wake up to find she has already taken a bath


KWA MARA YA KWANZA MZEE MAJUTO AUTAJA MSHAHARA WAKE ANAOPATA KWA KUIGIZA KWA MWEZI


Ni nadra sana kwa Mastaa wengi wa Tanzania kukubali kusema kiwango anachopata kwa mwezi kutokana na kazi yake ya umaarufu ila kwa Mzee Majuto ni kinyume, amekubali kusema kila kitu kwenye kipato cha movie zake za vichekesho ambazo mpaka sasa ndio zinashika namba 1 kwa mauzo Tanzania?
Kwa sababu ni kiapo cha millardayo.com kuhakikisha chochote ambacho ni stori unakipata, imempata Mzee huyu Mbembe kutoka Kigoma akiwa ni mzaliwa wa Tanga umri ukiwa miaka 65 na kukubali kuzungumza kwenye hii Exclusive interview.
Akiwa ni baba wa watoto tisa, anakwambia ‘kwenye movie za kuigiza sasa hivi kama mtu akitaka kunishirikisha ni lazima unilipe milioni nane kutoka milioni 2 au tatu nilizokua nazikusanya mwanzoni, hii bei nimeibadili kuanzia mwezi September 2013, mimi kadri ninavyocheza movie nyingie za kushirikishwa ndio nazidi kujipunguzia kipato changu kwa mwezi kutoka kampuni ya STEPS iliyoniajiri’
‘Mpaka sasa nimecheza movie zaidi ya 600 toka nimeanza kuigiza za kushirikishwa na zangu mwenyewe, nilianza kulipwa zaidi ya milioni moja kwenye movie toka mwaka 2007/2008 baada ya kuwa na kampuni ya Ally Riyami ambae alikua ananilipa shilingi laki sita kwa kila movie ya Comedy kwa hiyo kwa mwezi napata mpaka kwenye milioni 6 au saba kutokana na idadi ya movie nitakazoigiza’ – Mzee Majuto
‘kwa sasa hapa Steps nalipwa kuanzia milioni 17 mpaka 20 kwa mwezi, ni malipo mazuri sana ambayo napata kila mwezi na nimepangiwa kucheza movie 9 kwa mwaka lakini kule Ally Riyami kwa mwezi ndio nilikua nacheza hizo movie 10, yani unacheza movie mpaka unasikia kizunguzungu…. kwa sababu nilitakiwa kucheza movie 1 kila baada ya siku tatu ila kwa sasa kwenye mkataba wa Steps nacheza movie moja ya kampuni na moja ya nje ya kampuni, maisha mazuri’ – Mzee Majuto

DOGO JANJA"NAJUA YATASEMWA MENGI KUTOKA KWA OSTAZ JUMA....ILA NIMEKUWA MKUBWA NA SASA KUPELEKWA PELEKWA TENA SITAKI"

Janjaro msanii kutoka Arusha lakini makazi yake yapo Dar amefunguka na DJCHOKAblog kuwa hajafukuzwa na Ostaz Juma Namusoma kwenye kampuni yake ya Mtanashati bali amejitoa mwenyewe kwa hiari yake. Janjaro amesema amechoka na matendo tu ya Ostaz na alikuwa tu akiyavumilia lakini kwa sasa ameshakuwa mkubwa so nataka nikae kivyangu vyangu nifanye mambo yangu kama wasanii wengine ambao hawana meneja na wanafanya poa. Namnukuu Janjaro akisema....

 "Najua yatasemwa mengi kutoka kwa Ostaz Juma ila mimi ndio uwamuzi wangu, kuna watu wanasema sina utovu wa nidhamu lakini hao watakuwa wananijua sasa hivi hawajanifuatilia kutoka nyuma. Hata mtoto mdogo atakuwa mtundu ila akiwa mkubwa hunyooka na kuwa mtoto mzuri sasa nimekuwa mkubwa na kupelekwa pelekwa tena sitaki, kwa maelezo zaidi Ostaz Juma aongee na wazazi wangu asiongee na mimi"

BATULI AFUNGUKA KUHUSU MADAI KUWA IRENE UWOYA ANAMUENDEA KWA WAGANGA ILI AMPOTEZE KWENYE FILAMU



Siku za Hivi karibuni kumekuwa na tetesi zisizo rasmi kuwa mastaa wawili wa filamu Swahiliwood Yobnesh Yusuph(Batuli) na Irene Uwoya hawana maelewano mazuri chanzo kikidaiwa ni Irene Uwoya kutaka kumpoteza Batuli kwenye tasnia ya filamu ili asifurukute. Habari hizo zinaenda mbali zaidi zikidai kuwa kuna kipindi Batuli alikuwa anaumwa maeneo ya kifuani lakini baadhi ya watu wakiwemo wasanii wenzake wakiamini Uwoya ndiye kamfanyia mambo ya kilozi(ushirikina). 

 Tetesi hizo tulizipuuza mwanzoni lakini zinaonekana kurudi tena kwa kasi hivyo tuliamua kuwatafuta mastaa hao wawili ili watoe ufafanuzi wao wenyewe na wa kwanza kuulizwa alikuwa Uwoya hata hivyo namba yake ilionekana kutokuwa hewani alipotafutwa juzi na jana alipotumiwa ujumbe namba yake ilionekana bado haipo hewani. Batuli nae alitumiwa ujumbe juzi kuhusu issue hiyo lakini hakujibu mpaka jana usiku ndiyo alijibu akisema alikuwa busy sana. Batuli alisema "sina ubaya na msanii yeyote na moyo wangu ni mweupe na nina mapenzi na wasanii wenzangu wote, nawapenda sana anayeniwinda kwa ubaya Mungu atanipa ulinzi wake, sipendi uadui na mtu namuachia Mungu atanilipia yote"

Thursday, October 24, 2013

JAMANI TUWASAIDIE,WEMA NA JOKATE WASHIKANA MASHATI KUHUSU SURA ZAO,KILA MMOJA ANAJINADI KUWA YEYE NI MZURI ZAIDI YA MWENZAKE...


Hawa wote  ni wasanii maarufu  wanaojulikana  kimataifa na wenye sura  zenye  mvuto...

Ni  wasichana  jasiri  na  wajasiliamali  wanaojua  kuisaka  pesa  na  wasio penda  kuwa tegemezi.Hapa  nawazungumzia  Wema Sepetu  na Jokate  Mwegelo 


Kumekuwa  na  ushindani  wa  chini chini  kati  yao  kuhusu  sura  zao  kiasi  cha  kuzua  mjadala  wa  nani  ni  mzuri  zaidi  ya  mwenzake....

Mmoja  akivaa  nguo  hii leo, mwingine  naye  ni  lazima  aitafute  nguo  kama  hiyo  hiyo  kesho aivae  na  kuitupia  mtandaoni ili mashabiki  walinganishe  na  kutoa  hukumu.

Hizo  ni  picha  zao  2  wakiwa  ndani  ya  vazi  la  pundamilia. Na hapo wako   mbele  yako  wakiomba  UWAHUKUMU ili  kuukata  mzizi  wa  fitina..


Hukumu  yako  inaombwa  izingatie  kigezo    cha  SURA    tu na  siyo Tabia  zao....Je, nani  ni  mkali  zaidi  ya  mwenzake?


Professor Jay akabidhiwa BARCODE itakayomfanya kuuza kazi zake kimataifa na hata kuingia katika chart kubwa duniani kama Billboard

Kampuni ya GS1 (TZ) National Limited iliyoko Msasani karibu na hospitali ya CCBRT, leo hii imemkabidhi Rapper Professor Jay Barcode itakayokuwa ikitumika katika kazi zake za muziki na kumuwezesha
kuuza kazi zake online na hata kuingia katika chart kubwa duniani kama Billboard na zinginezo na kumfanya aweze kutanua soko la kazi zake duniani kote.




GSI imeanzishwa kwa kusudio kubwa la kuweza kutoa huduma za Barcodes na teknologia nyingine zinazotewa na taasisi GS1 ulimwenguni, za kuendeleza biashara kimataifa na kitaifa. 

Imedhibitika kwamba chombo hiki, kabla ya kusajiliwa nchini,  wafanyabiashara wengi wa Tanzania walikuwa wakizifuata huduma za barcodes kutoka nchi za Kenya na Afrika ya Kusini. Chombo hiki kinasimamiwa na Mkutano Mkuu wa mwaka na Bodi ya Wakurugenzi.