Wema ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Endless Fame, anadaiwa kuwa
beneti na kijana aitwaye Robby lakini mwenyewe amesema kwamba hakuna
anayeweza kumtenganisha na wanaume.
Habari zinasema kuwa, Wema na Robby wamekuwa wakipiga picha za kimahaba
na mnyange huyo kuziingiza kwenye mtandoa wake na kumtambulisha kijana
huyo kwa jina la ‘Honey’
Risasi Jumamosi lilifanya juu chini na kumsaka Wema ili kumtaka ajibu tuhuma za kuwa katika mahaba na kijana huyo.
Mei 22 mwaka huu, mwandishi wa gazeti hili alifika ofisini kwa mrembo
huyo, Mwananyamala Komakoma jijini Dar es salaam na kumbana kwa maswali
juu ya kuvuja kwa picha zake hizo akiwa na Robby na nyingine akiwa na
wanaume wengine tofauti.
“Watu wamekuwa wakinizungumzia kila kukicha, tena maongezi yao yamekuwa
yakianzia kwenye baadhi ya picha zangu, kila mtu ana namna ya
kutengeneza ‘laifu’ yake na miye huwa sioni shida mwanaume asiye hawara
yangu kunikisi au miye kumkisi,” alianza kujitetea.
“Ukifuatilia historia yangu mara nyingi utagundua marafiki zangu wengi
ni wanaume kuliko wanawake na wengi wao wanakuja kwangu, tunakunywa na
wanaondoka mida mibovu, kwa asiyenijua anaweza kuhisi ni mabwana zangu
kumbe siyo, hata kwenye mitandao huwa sioni tabu kuweka picha za mtu
akinikisi au nikimkisi,” aliendelea kusema.
“Siwezi kubadilika hii ni life style yangu. Siwezi kuacha kuwa karibu na
marafiki wa kiume, hivyo ndivyo nilivyoumbwa watu wasinishangae, suala
la kukutana na mtu na kupiga naye picha siyo ishu kwangu, ningekuwa mtu
wa ajabu sana kama ningekuwa nawakisi midomoni au wao kunikisi mdomoni,”
aliongeza.
Wema amesema kuwa watu wana hisia mbaya juu yake na Robby jambo ambalo
siyo sahihi kwa kuwa, katika maisha yake anawapenda marafiki wa kiume
zaidi ya wanawake.
No comments:
Post a Comment