Rapper Ney wa Mitego, kupitia wimbo wa "Nasema nao" alifanikiwa kupata
tuzo ya wimbo bora wa hiphop, ambao umesababisha malalamiko kwa baadhi
ya wasanii wengine ambao wnaona hakustahili kuchukua tuzo hiyo kwa wimbo
huo, huku wengine wakidai Fid q anastahili na wengine kudai Stamina
ndio anastahili....leo hii Ney mwenyewe kafunga juu ya swala hilo
"aah wasanii ndio wanaolalamika na wameandika kwenye mitandao, lakini
mwisho wa siku lazima tukubali matokeo kwamba mziki unabadilika kila
kukicha, mi nawaambia wasanii wenzangu kwamba mkiendelea kung'ang'ania
huko mtakufa njaa, halafu mwisho wa siku wataendelea kulia tu kila siku
kwamba kuna hili mara lile,mi naimani kwamba mashabiki wangu ndio
wamenikabidhi tuzo, media zinazosapoti kazi yangu ndio zimenisaidia
mpaka mimi nimezungumza na mshabiki wangu popote walipo mpaka juzi
nimepata tuzo ya wimbo bora wa hiphop. mi nastahili kupata tuzo,
kwasababu kwanza sijui wao wanafanya hiphop gani, wakae waeleze mziki
wao wao ni hiphop kwasababu hii na hii na hii na wangu sio hio hiphop
kwasababu hii na hii na hii. bwana hiphop ni ukweli na unabadilika kila
siku kila kukicha. Mi nawashauri tu kitu kimoja, sitaki kubishana na
msanii yoyote, wana njaa, wakiendelea kung'ang'ania huko watakufa njaa,
kwanini watu wamemsapoti Ney, kwanini watu wamemsapoti Kala
Jeremiah,angalia mashairi ya Kala yako wazi, lakini we unaweka sijui
mafumbo ya dizaini gani nani atakuelewa...........
halafu tuzo sio lazima upate tuzo, sio lazima ulaumu, kuna wasanii
wakali hawajawahi kupata tuzo lakini hawajawahi kulalamika, kuna wasanii
kama Juma Nature, nani anaweza kusimama stage na Nature? sijawahi
kumsikia anaongea.....
category moja tu nimewekwa nimetusua wao wanalia, shauri yenu shauri
yenu, jipangeni mwakani, mi staki kubishana nao, am the best, halafu
wasipoangalia nawatengenezea kiwanda kwa ajili ya kuwaajiri
wanapoendelea kuwana na hali ngumu, natengeneza kiwanda ambacho
ntawaajiri wasanii wanaofeli wote kwasababu hawana shughuli za
kufanya." amesea Ney.
Msikilize Hapa akiongea:
No comments:
Post a Comment