POLISI wa kike wa Kituo cha Magomeni, jijini Dar es Salaam aliyejulikana
kwa jina moja la Anisa, ametimuliwa kazi kwa madai ya kupiga picha ya
utupu iliyosambaa mitandaoni.
Chanzo makini ndani ya jeshi hilo
kilisema Anisa alifukuzwa kazi wiki iliyopita baada ya kuhojiwa na
mabosi wake wa makao makuu ya jeshi hilo na kukiri kuwa picha hiyo ni
yake.
“Anisa aliitwa makao makuu, mabosi wakamuonesha picha yake
akiwa mtupu kitandani, akakiri ni yeye. Alijitetea eti alifanya hivyo
kwa sababu siku ya tukio alikuwa amelewa sana,” kilisema chanzo.
Chanzo
kiliendelea kudai kwamba baada ya afande huyo mwenyeji wa Tanga kukiri,
viongozi wa jeshi hilo walimwambia amekiuka kanuni na kulidhalilisha
jeshi hilo hivyo hataendelea kuwa mtumishi.
Picha ya afande huyo
imeenea mitandaoni na kwenye baadhi ya simu za mikononi za watu kitendo
kulicholifanya jeshi hilo kufanya uchunguzi na kubaini kuwa ni yake.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina, Suleiman Kova
alipoulizwa juzi alikiri kufukuzwa kwa askari huyo na kumtaka mwandishi
wetu kufuatilia zaidi kwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP
Camilius Wambura ambaye naye alipoulizwa kuhusu tukio hilo alikiri.
‘‘Tunahitaji
askari wenye maadili mema ndani ya jeshi letu, yule atakayefanya mambo
bila kufuata kanuni na sheria hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Askari muda wote anatakiwa awe mfano bora kwa jamii,’’ alisema Afande
Wambura.
Taarifa zaidi zinadai kwamba kwa sasa Anisa anaishi uraiani kama raia wa kawaida.
No comments:
Post a Comment