POOL PARTY

POOL PARTY

Friday, June 7, 2013

Majambazi yaliyo Vaa Kike na Kupaka Wanja Yauwawa na Wananchi


WATU wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi waliokuwa wamevaa kikekike wameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kuwakurupusha wakivunja duka usiku.
Mauaji hayo yalitokea eneo la Nyegezi Kijiweni, Kata ya Mkolani, wilayani Nyamagana jijini Mwanza, majira ya usiku, Mei 29, mwaka huu wakiwa katika harakati za kuvunja maduka matatu yaliyopo eneo hilo.
Watu hao ambao ni wanaume wanadaiwa siku ya tukio wakiwa na silaha ya moto (bunduki) walivunja nyumba tatu na duka moja katika eneo hilo kwa kutumia vifaa mbalimbali vya jadi.
Imedaiwa kuwa wakati majambazi hayo manne yakifanya uhalifu huo, mawili yalivaa makoti meusi marefu na yaliyobaki yalijitanda ushungi na kujifunga kanga na kujipaka wanja usoni ili yasitambuliwe.
Chanzo hicho kilieleza kuwa majambazi wawili waliokuwa na silaha ya moto, baada ya kukurupushwa walikimbia na kutokomea kusikojulikana.
Wananchi kuona hivyo waliwadhibiti waliovaa mavazi ya kike na kuwashambulia kwa kuwakatakata kwa mapanga hadi kuwaua.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna (DCP) Ernest Mangu (picha ndogo), alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea.

No comments:

Post a Comment