NI sahihi kabisa nikisema kuwa Klabu ya Bongo Movie Unity ndiyo jicho la mashabiki wengi wa filamu za nyumbani. Wasanii waliopo ndani ya umoja huo, wengi wao ndiyo mastaa wakubwa ambao mashabiki hupenda kuwafuatilia ili kujua maisha yao.
Na Imelda Mtema
NI sahihi kabisa nikisema kuwa Klabu ya Bongo Movie Unity ndiyo jicho la mashabiki wengi wa filamu za nyumbani. Wasanii waliopo ndani ya umoja huo, wengi wao ndiyo mastaa wakubwa ambao mashabiki hupenda kuwafuatilia ili kujua maisha yao.
Makundi hayo yanasadifu kabisa aina ya maisha ya kundi husika kwa maana ya ndege wanaofanana huruka pamoja. Ndiyo maana Wema Sepetu amekuwa akishindwa kufiti kwenye kundi husika kwa kuwa hana ndege anayefanana naye. Akiwa na kundi huwa hachelewi ‘kuharibu’.
Kuna wakati ukitaka kujua ishu ya msanii fulani na kuulizia kwa wasanii wenzake, utaambiwa mtafute fulani au akina fulani ndiyo watu wake.
Makundi hayo unaweza kuyachambua katika staili ya ‘kushea’ vitu vyao, kupeana siri na mambo mengine mengi. Hapa chini nakupa orodha ya makundi hayo jinsi yalivyo;
ODAMA, RECHO
Jennifer Kyaka ‘Odama’ na Rachel Haule ‘Recho’ wana kundi lao ambalo pia huusisha chipukizi. Odama na Recho ni marafiki wakubwa ambao mara nyingi wanakuwa pamoja. Hushirikiana katika kazi nyingi na si tu wakiwa ndani ya Bongo Movie bali hata wanapokuwa majumbani au kwenye bata ndefu utawakuta pamoja.
Cathy.
MAYA, CATHY, CHUCHUUkimwona Mayasa Mrisho ‘Maya’, pembeni yake watakuwepo Sabrina Rupia ‘Cathy’ na Chuchu Hans. Hawa ni marafiki sana, mambo mengi wanafanya pamoja na kila likitokea tatizo hujaribu kulitatua wakiwa watatu. Hata kama kutakuwa na msiba au sherehe sehemu yoyote lazima timu hii ikamilike, wenyewe wanajiita ‘Wanyama’.
TIKO, MERRY, ANITHA
Hawa huwa wanajiita ‘Watoto wa Mbwa’. Wana timu kama ya wasanii watano hivi. Hawa ni Tiko Hassan, Merry Mawigi, Anitha na Kunguru. Mara nyingi hupenda kutembea pamoja kwenye shughuli mbalimbali na bata ndefu. Hata mavazi yao huwa wanapenda kushona sare.
WOLPER, LAMATA
Jacqueline Wolper hana historia ya kuwa na rafiki wa kudumu zaidi ya kuongea na kila mtu lakini kama ulikuwa hujui, ni rafiki mkubwa sana wa meneja wake, Leah Mwendamseke ‘Lamata’ ambao hao wamedumu muda mrefu. Ukweli ni kwamba Wolper huwa hapendi kufanya jambo lolote bila Lamata hata kama ni la siri kiasi gani.
Uwoya.
UWOYA, JOHARI, MARIAMIpo kolabo ya Irene Uwoya, Blandina Chagula ‘Johari’ na Mariam Ismail. Siku zote wasanii hao huwa hawaachani, ni marafiki ambao kamwe hawatengani na kama ukitaka kuamini hilo mmoja wao awe na kitu kama sherehe na kadhalika, hapo ndipo utagundua umoja wao. Ni marafiki wa muda mrefu sana na hata hivi karibuni Uwoya na Johari walitimkia nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ katika masuala ya filamu.
USHAURI WA BURE
Ushauri wangu kwao wajue kwamba siku zote umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, waungane kwa pamoja ili waweze kusaidiana kwa sababu bado kuna wengine ambao wanahitaji kuchomoza ndoto zao lakini haiwezekani kwa sababu ya makundi madogomadogo.
No comments:
Post a Comment