MSANII wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ hivi karibuni alijikuta akipandwa na kushukwa na presha mara baada ya kwenda hospitali kupimwa Ugonjwa wa Ukimwi.
Kikizungumza na Exclusive chanzo makini ambacho kilishuhudia tukio zima katika Hospitali ya Dokta Mvungi, Kinondoni, jijini Dar kilisema baada ya Amanda kupewa majibu ya vipimo na daktari, alianza kuhaha huku na kule kama mtu aliyechanganyikiwa, kisha presha ikampanda baadaye ikashuka.…
MSANII wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ hivi karibuni alijikuta akipandwa na kushukwa na presha mara baada ya kwenda hospitali kupimwa Ugonjwa wa Ukimwi.
Kikizungumza na Exclusive chanzo makini ambacho kilishuhudia tukio zima katika Hospitali ya Dokta Mvungi, Kinondoni, jijini Dar kilisema baada ya Amanda kupewa majibu ya vipimo na daktari, alianza kuhaha huku na kule kama mtu aliyechanganyikiwa, kisha presha ikampanda baadaye ikashuka.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Amanda na kumuuliza juu ya tukio hilo ambapo bila hiyana alitiririka:
“Ile ilikuwa ni mara ya tatu kupima ngoma yaani wakati nikisubiri majibu, presha ilipanda ghafla mpaka daktari akawa na wakati mgumu wa kunipa majibu.
“Nilienda kuchukua majibu na sikutaka kuyaangalia, nilimpelekea daktari ambaye aliniambia niko safi yaani sikuamini nilitoka nikiwa naongea peke yangu, nilikuwa sijiamini si unajua tena ujana ni maji ya moto sasa presha ,” alisema Amanda.
No comments:
Post a Comment